Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kujibu maswali ya wananchi watumiao mitandao

Uchaguzi 2020 Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kujibu maswali ya wananchi watumiao mitandao

Mimi swali nataka kujua vipi kuhusu mawakala wa upinzani kutokuapishwa maana ndio mchezo wa ccm waliojipanga nao hadi sasa? Chadema wamejipangaje
Hili niswali ambalo hata mimi ningeli liuliza je wasipo apishwa chadema watachukua hatua gani
 
Hivi saa 2 hadi 4 haijafika bado? Au ni masaa ya kidhungu?
Huyu ni mgombea wa kiti cha uraisi na sio balozi wa nyumba kumi. Ni jambo la kawaida ratiba kuingiliana kutokana na situation anayo i-face

Majibu atayajibu japo sio katika ule muda alioutegemea, lakini maswali karibia yote yaliyoulizwa hapa alikwisha yatolea majibu kiundani kabisa kwenye mahojiano yake na waandishi wa habari
 
Kamwene mnyalukolo ila achaga ujinga nacho amini wahehe hawapo hivyo au we ni akina mapembelo kama ni hao ntakuwa sina shida na we we kabisa
Hahahaaaa....... Mapembelo ni wabunge wetu maarufu mchungaji Msigwa na Sugu!
 
Lisu aje ajibu sakata la yeye kutaka ndoa za jinsia moja ?

Ulaji wa ruzuku chadema?

Kuwa kibaraka wa wazungu?

Kupanga mauaji ya watanzania kwa kuwaweka barabarani wakati yeye akijificha ?

USSR
Nenda katoe ushaidi wa ulaji wa ruzuku za chama. Na maandamano yapo pale pale uchaguzi usipokua wa haki
 
Huyu ni mgombea wa kiti cha uraisi na sio balozi wa nyumba kumi. Ni jambo la kawaida ratiba kuingiliana kutokana na situation anayo i-face

Majibu atayajibu japo sio katika ule muda alioutegemea, lakini maswali karibia yote yaliyoulizwa hapa alikwisha yatolea majibu kiundani kabisa kwenye mahojiano yake na waandishi wa habari
Kwa hiyo kama maswali yote yalishajibiwa hii thread ni ya nini na matangazo yenye muda mahsusi yalikuwa ya nini?
 
Swali 1.Wale ambao wanavaa nguo za polisi na kuvamia wagombea wa aina zote popote pale je hao siyo magaidi. 'What is you opinion and cause of action, because this is agroup of unknown criminals'
Swali 2.Sitashangaa mapolisi wa aina hii tarehe 28-10-2020 kufanya matukio ya ajabu zaidi ya haya, mtachukua hatua gani kama chama 'are you ready to retaliate'
Swali 3.Gaidi anapokuvamia nyumbani kwako kavalia nguo za polisi sheria za Tanzania zinasemaje maana kwasasa imekuwa kawaida watu waliovalia nguo za polisi kuvamia makazi ya watu kibabe
 
Kwa hiyo kama maswali yote yalishajibiwa hii thread ni ya nini na matangazo yenye muda mahsusi yalikuwa ya nini?
Hakuna sehemu nimesema maswali yote yalishajibiwa

Umeninukuu vibaya
 
Naomba kuuliza maswali mawili kuhusu ILANI ya uchaguzi Mkuu ya CHADEMA 2020 kuhusu sera yao ya MAJIMBO au Dby D

(1) CHADEMA wanainadi sera yao ya Majimbo lakini kuna MIKOA/HALMASHAURI ambazo zina makusanyo yake yapo chini, wanashindwa hadi kuwalipa Madiwani wao, Je,serikali yake ya itawezaje kuweka mazinginra sawa ya PATO la Taifa kwa Nchi nzima ila upendeleo wowote kama inavyoelekezwa na Katiba ya Tanzania ibara ya 9(h-i); Mfano Mkoa wa Singida pato lake kwa Mwaka linaloochangia GDP ya Taifa haliwezi hata kuwalipa walimu na Madaktari/manesi hata kwa miezi miwili tofauti na Mikoa kama Dar,Arusha na Moshi zenye sekta kubwa za Kitalii;

(2) Nataka kujua nini msimamo wa CHADEMA kuhusu AJIRA serikalini na upatikanaji wa Viongozi kama Makatibu Wakuu,Wakurugenzi wa Wizara, wao watatumia Njia/model gani kuandaa na kuwapata Viongozi wa kuendesha serikali bila upendeleo wa Kisiasa au Kikabila?

(3) Napenda kujua Msimamo wa CHADEMA kuhusu Mapambano ya Rushwa serikalini-mbona hili sijalisikia hata mara1 au rushwa imeshai kabisa Tanzania?


Nitafurahi kupata majib
u
 
Katika kampeni ya mwaka 2015 mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Nyehunge nape nauye ali-declare kua ccm itashinda kwa bao la mkono (kinyume na sheria)
Kwahiyo neno"kasema"ndo fact ya kutolea ushahidi?
alafu unajua alimaanisha nini aliposema bao lamkono?
nyinyi mlikimbilia kwenye wizi wakati yeye hakumaanisha wizi.
 
Kushindwa na kushinda si aibu ni matokeo ya shindano. Hivyo hata team yenu na mgombea wenu auzoee mchezo .

Uwizi wa kura upo na hata wa kikanuni na kisheria upo. Mfano ni sasa Ccm imeshazawadiwa majimbo 20 na wilaya kama ya misungwi kutakuwa na kura moja ya urais. Huu ni uwizi
Uwizi anao Mbowe alietafuna pesa za michango ya wabunge wa Chadema na michango ya rambirambi za marehemu mawazo wa Geita.
 
Umesema *karibia yote*
"Karibia yote" ni tofauti sana na kauli yako ambayo ulitaka kunilisha kwa kuniwekea maneno mdomoni kua nimedai "yalijibiwa yote"
 
Kwahiyo neno"kasema"ndo fact ya kutolea ushahidi?
alafu unajua alimaanisha nini aliposema bao lamkono?
nyinyi mlikimbilia kwenye wizi wakati yeye hakumaanisha wizi.
Leo hii nikitoa kauli mbele ya hadhara kua NAWATAFUNA nitakuua, halafu baada ya masaa kadhaa kupita ikagundulika umeuawa basi mtu wa kwanza kukamatwa nitakua mimi niliyetoa kauli ya vitisho

Lakini hata usipokufa, pia sheria inasema ni kosa kutishia kuua au kutishia mvunjiko wa amani hivyo nitawekwa nguvuni na vyombo vya serikali kwa kosa la kutoa kauli yenye mlengo wa kuhatarisha maisha ya mtu japo kua huyo mtu bado mzima

Kwani mtu akiwa anahutubia changamoto za mavuvi wanazokumbana nazo wakiwa ziwani, utasema kua huyo mtu hakumaanisha ziwa kama ni "lake" bali alimaanisha ziwa yani "breast"?

Huyo nape nauye alikua kwenye shuguli za kampeni na alitamka kua ccm itashinda hata kwa goli la mkono, kwaiyo ccm walikua kwenye harambee za umitashunta mpaka nape katamka kauli ile?
 
Kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi kumuuliza maswali Mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Ndg. Tundu Lissu; imebidi apate muda kuyapitia maswali yote (takriban 200) ili kila mmoja ajibiwe. Maswali hapa JF yaliulizwa kupitia > Uchaguzi 2020 - EXCLUSIVE: Maswali kwa Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kutoka kwa Watanzania watumiao mitandao ya kijamii

Aidha, takribani maoni 600 yamekusanywa toka Facebook na mengine takribani 165 toka Instagram; mengine 66 ya Twitter pamoja na wale waliotuma SMS, DM na barua pepe(Email).

Tunatarajia kufikia kesho atakuwa ameyapitia maswali hayo na yote yatajibiwa.

Shukran kwa wote walioshiriki; tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza
Pamoja
 
Back
Top Bottom