GE2025 Mgombea Urais Zanzibar Kupitia ACT, Othman Masoud kujuimuisha WALIMU WA MADRASA Katika Mfumo wa Malipo ya Serikali

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,776
Reaction score
42,933
FB_IMG_1759747759802.jpg
Nitaweka historia mpya kwa kuwajumuisha walimu wa madrasa katika mfumo wa malipo ya Serikali, kuwapa mishahara, bima ya afya na hifadhi ya jamii.

Walimu hawa ndio msingi wa maadili, dini na malezi ya taifa, hivyo lazima wapewe heshima na thamani yao. Serikali isiyowajali wao ni Serikali isiyojali mustakabali wa nchi.

source: Official Page Yake
 
C&P from FB

MAONI YANGU:

Ahadi ya kuwajumuisha walimu wa madrasa katika mfumo wa malipo ya Serikali ni hoja yenye mvuto mkubwa wa kijamii, lakini kikatiba na kisheria inahitaji tafakuri ya kina. Serikali ya Zanzibar si serikali ya kidini, bali ni serikali ya wananchi wote bila kujali dini au imani zao. Fedha za umma haziwezi kuelekezwa kwenye kundi moja la waumini bila utaratibu wa kikatiba unaolinda usawa wa dini zote.

Swali kubwa hapa ni: fedha hizo zitapitia bajeti ipi? Na je, walimu wa dini zingine kama Wakristo, Wahindu, Wayahudi, au wenye imani za jadi nao watajumuishwa? Ikiwa jibu ni hapana, basi sera hiyo itakuwa na harufu ya ubaguzi wa kidini, jambo linalopingana na misingi ya Katiba ya Zanzibar, Ibara ya 12(2) inayokataza ubaguzi wa aina yoyote.

Ni vyema tukakumbuka kuwa hata kama Zanzibar ina zaidi ya asilimia 98 ya Waislamu, wale wachache wa dini nyingine bado ni raia kamili wenye haki sawa mbele ya Serikali. Haki si hesabu ya idadi, bali ni thamani ya utu.

Maandiko Matakatifu yanatufundisha mipaka kati ya mamlaka ya kiroho na mamlaka ya kiserikali. Yesu alisema, “Toeni kwa Kaisari yaliyo ya Kaisari, na kwa Mungu yaliyo ya Mungu” (Mathayo 22:21). Vivyo hivyo Qur’an inasisitiza: “Kwenu dini yenu, kwangu dini yangu” (Surat Al-Kafirun 109:6).
Hapa tunafundishwa kuheshimiana bila kuchanganya mamlaka ya serikali na imani binafsi.

Kwa hiyo, kama dhamira ni kuwatambua walimu wa maadili na dini, basi iwe kwa mfumo wa haki unaowagusa wote — iwe kwa Mfuko wa Maadili ya Taifa au mpango wa bima ya kijamii usio na ubaguzi.

Serikali isiyowatambua walimu wa madrasa haina maono ya maadili, lakini Serikali itakayolipa walimu wa dini moja pekee haina mizani ya haki.

Zanzibar mpya tunayoitaka si ya upande mmoja wa imani, bali ni ya watu wote, dini zote, na vizazi vyote.

Haki ya mmoja ni mizani ya haki ya wote.

#ZanzibarYaWote #UsawaWaDini #MaadiliNaKatiba

Dr Nagaikaya Thomas M
Dar es salaam
TANZANIA 🇹🇿
@followers
 
Usawa wa dini kwa watu 99 percent na one percent ya wageni?
 
Katiba ya Bunge la Nyerere na Magufuli wako Tokea lini nchi ilitungwa katiba ya Bunge huru lililochaguliwa na wananchi?
Hebu tuambie hiyo biblia uliyonukuu ni biblia ipi kati ya maelfu ya biblia tofauti?
 
Hao ndio tjnategemea waivushe nchi..
Then chakushangaza huko fb wazenji wanampongeza hatari
Hao wazenji siwezi kuwashangaa sana maana ni dini yao, ila kiukweli wanaihalibu nchi kwa mikono yao, leo hii watangaze maasikofu na wachungaji watapata mkate wao kutoka serikalini nikishabikia nitakuwa ni zwazwa tena zumbukuku wa mwisho.
 
Tuwacheni na nchi yetu . Nyinyi nendeni mkaandamane tarehe29
 
Nitaweka historia mpya kwa kuwajumuisha walimu wa madrasa katika mfumo wa malipo ya Serikali, kuwapa mishahara, bima ya afya na hifadhi ya jamii.

Walimu hawa ndio msingi wa maadili, dini na malezi ya taifa, hivyo lazima wapewe heshima na thamani yao. Serikali isiyowajali wao ni Serikali isiyojali mustakabali wa nchi.

source: Official Page Yake

..Na waalimu wa Sandei skul watalipwa?
 
Back
Top Bottom