GE2025 Mgombea wa CCM hajaongea jipya lolote, ameshindwa kujinadi vyema

GE2025 Mgombea wa CCM hajaongea jipya lolote, ameshindwa kujinadi vyema

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Picsart_25-08-28_19-18-09-329.png
 
Hii si kweli, Uganda wana deni dogo kuliko Tanzania.


Pia Burundi na Rwanda zipo afrika mashariki, hivyo bila hata kumuuliza mtu yoyote unakua unajua kabisa lazima zina Deni dogo kuliko Tanzania
Anaowaambia wana muda wa kutafuta ukweli kama huu kwa kutumia akili zao?na kwanza hiyo elimu ya kufanya hivyo wanayo?

Anaokota wajinga wajinga wanashangilia ujinga hawayajui madhara yake.
 
kuna sehemu nimepita jioni hii kwenye kijiwe cha boda kuna jamaa anagawa hela kwa boda waliokuwa wameenda kawe, sasa kaja boda mwingine kutoka kijiwe cha jirani anaomba hela yake kaambiwa asubiri kule kwenye kijiwe chao ili ambao hawakwenda waone umuhimu wa kwenda kule...

Nilikuwa pembeni nimeishia kucheka
 
Amepata fursa ya kuzindua kampeni mbele ya umati uliosombwa ukasombeka halafu ameshindwa hata kujinadi vizuri. Anaonekana amechoka, ,kama kalazimishwa kuongea kama vila Bora liende watajua wenyewe.

Daa! Nawezaje kupigia kura mtu wa namna hiyo?

Kama ni hivyo, basi hii itakuwa mara ya nyingine tena CCM imeingia chaka.

Kama hiki kilichoelezwa kwenye ilani ya 2025-2030 ndo Watanzania watafanyiwa big no. Yaani majaribio ya bima kwa afya wazee, kuajiri wakunga na kununua matrekta. Haya watanzania walishaambiwa mno na hakuna kitu.

Mimi sioni kitu kipya na sioni kama yupo serious na nchi kwasababu hakuna hata jambo Moja la kimkakati zaidi kusikia gridi ya maji kitu ambacho kimeimbwa toka uhuru Hadi hapa tulipo.

Hakuna mega project yoyote kwenye ilani. Hakuna hakuna hakuna.

Mgombea ndo kabisa hata hupati hamu ya kumsikiliza.

Kazi kwenu watanzania October kuuza nchi au kubakisha nchi
Anasoma.tu
 
Back
Top Bottom