Elections 2015 Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Tunachosahau tu ni kwamba utake usitake unaposhika ile nafasi kuna tabia baadhi za mtu hubadilika sababu lile ni jukumu zito sana. Mara nyingi huwa kuna mazuri na mabaya ambayo mtu huweza kuwa nayo pindi tu anapopata ile nafasi.
 

..hivi kwa exposure ya Magufuli unataka kuniambia alikuwa hajui thamani halisi ya nyumba na viwanja kwa maeneo zilipokuwa nyumba za serikali?

..nakuhakikishia kwamba hawa waliamua kwa makusudi kabisa KUIBA nyumba zile na hakuna haja ya sisi wananchi kumung'unya maneno kuhusu nini kilitokea.

..Magufuli alikwenda mbali zaidi kwa kuwabeza waliokuwa wakipinga wizi ule na kutamka bungeni kwamba serikali itapata mapesa mengi na kuweza kujenga nyumba nyingi zaidi ya zile ilizouza.

..wa-Tz tunapaswa kubadilika na kukataa kuwa ABUSED na hawa tunaowaita viongozi. why put up with these ppl? kila mara wakiboronga basi tunatengeneza visababu[walikuwa na nia nzuri, tuangalie mema yao] vya kuendelea kuwahifadhi madarakani.

..binafsi sioni faida yoyote ile ya kuendelea kuwa na kiongozi ambaye tunajua kabisa ameisababishia nchi hasara inayoweza kufikia trillion of shillings.

NB:

..hivi Magufuli aliyeiba akiwa waziri wa ujenzi unategemea ataacha wizi tukimpa madaraka makubwa zaidi ya Uraisi?

..Magufuli huyu mwenye kiburi, dharau, na kauli za hovyo-hovyo akiwa waziri, unategemea atakuwa na staha na unyenyekevu akiwa Raisi?

cc Pasco
 
Last edited by a moderator:
Tunachosahau tu ni kwamba utake usitake unaposhika ile nafasi kuna tabia baadhi za mtu hubadilika sababu lile ni jukumu zito sana. Mara nyingi huwa kuna mazuri na mabaya ambayo mtu huweza kuwa nayo pindi tu anapopata ile nafasi.

..lakini ukiangalia kwa umakini utakuta wanabadilika kwa kupungukiwa kimaadili.

..Raisi wa Tanzania ana madaraka makubwa sana. yuko sawa na "mungu mtu."

..sasa ukimpa nafasi hiyo mtu asiye na maadili basi uwezekano mkubwa ni ku-abuse the office.

cc Pasco, tz2015, Kigogo
 

mkuu,wewe binafsi unadhani nani angeweza kuwa Rais bora kwa Tanzania baada ya Kikwete kumaliza muda wake kati ya hawa wagombea wanaotajwa au hata wasiotajwa?
 
Iwapo vetting ya viongozi ingefanywa na JF asingepita mtu labda aje malaika!
 
Iwapo vetting ya viongozi ingefanywa na JF asingepita mtu labda aje malaika!

..hatujasema tunataka Malaika.

..lakini pamoja na hayo hatuhitaji mtu ambaye tunajua ameshatutia hasara ya matrilioni kutokana na maamuzi yake.

..baya zaidi Dr.Magufuli haonekani kujutia uamuzi wake, na kufanya juhudi zozote zile kurekebisha makosa yake.

cc tz2015
 
Last edited by a moderator:
mkuu,wewe binafsi unadhani nani angeweza kuwa Rais bora kwa Tanzania baada ya Kikwete kumaliza muda wake kati ya hawa wagombea wanaotajwa au hata wasiotajwa?

..kwanza tunatakiwa tubainishe tunahitaji kiongozi wa aina gani.

..nini malengo yetu na vipaumbele vyetu ktk miaka 5, 10, 20, ijayo.
 
..kwanza tunatakiwa tubainishe tunahitaji kiongozi wa aina gani.

..nini malengo yetu na vipaumbele vyetu ktk miaka 5, 10, 20, ijayo.

mkuu mahitaji yetu ni mengi na yanajulikana,na hata wewe unayajua.Kwa kifupi sana,binafsi ningetamani tupate mtu wa kututoa hapa tulipo na kutupeleka pazuri zaidi kimaendeleo ya kijamii,kiuchumi na kisiasa kwa miaka mitano kwa kuanzia ie 2015-2020..kati ya hao wanaotajwa na wengine wasiotajwa,unadhani nani anafaa mkuu?naomba unitajie jina lake
 
Labda mkuu wewe tupe pendekezo lako la rais mtarajiwa 2015,unaweza ukawa unatumia sheria ya dawa ya moto ni moto,ikiwa na maana ya mahali palipoharibika weka aliyeharibika. Kama unatumia sheria hii basi Dr Magufuri hafai.
ieleweke kwamba naongelea chama tawala najua nje ya ccm wapo watu wenye uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko nchi hii.
 
Tumeisha waona wapole na wasikivu...wanavyoendesha nchi...tumejua faida zao na hasara zao...sasa tunataka tuwaone ambao ni wakali na si wasikivu linapokuja suala la kufuata sheria....kama hizo sheria wanazijua wao tu watafsri sheria (judiciary) na raia wengine zinawatatiza basi mfumo wa judiciary una matatizo makubwa...unahitaji kufumuliwa ili uweze kutuletea sheria upitia miswada ya sheria inyoeleweka kwa watu wote...maana sheria ni kwa ajili ya watu wote siyo wanasheria tu.

Apite Maghufuli.
 
NgumiJiwe, tz2015,

..mgombea ninayemtaka mimi sidhani kama atapatikana CCM.

..nasema hivyo kwasababu CCM wameshauhalalisha ufisadi.

..tunahitaji mtu ambaye atakuja kusimika namna mpya ya kuendesha nchi ambapo tutaongozwa kwa haki, maadili, na sheria.
 
Last edited by a moderator:
Nafanya tuu rejea!.

Pasco
 
Duuuuu!!!!!
Mkuu Pasco uliwaza mbali sana na kesho huenda yakatimia.
 
Last edited by a moderator:
Nafanya tuu rejea!.

Pasco

Huu uzi wako wako ni sawa na uzi mmoja wa Weston Songoro uliandikwa wiki moja iliyopita kuhusu mipango ya Nchimbi, Sophia Simba na Jerry Silaha kuleta MTITI endapo EL asipopitishwa alafu usiku wa kuamkia jana kina Kimbisa, Sophia Simba na Nchimbi wakaibuka kwa waandishi wa habari kupeleka kilio chao
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…