Mnamo siku ya tarehe 21 na tarehe 22 mwezi huu, yaani ijumaa na jumamosi, jiji la Arusha lilitikiswa na mgomo mkubwa uliofanyika katika eneo la stendi ndogo, mgomo ambao ulisababisha maduka yote karibia 400 kufungwa.
Mgomo huu ulituathiri sana sisi wafanyabiashara halisi ambao tunafanya biashara kwenye maduka haya, ambao tayari tumeshalipa kodi za pango kwa watu wanaoitwa "wajenzi" ambao kimsingi ni madalali ama watu wa kati wa vibanda hivyo ambavyo ni mali ya serikali. Tumeshangazwa sana na watu hao kuchukua fedha kwetu na kisha kumbe hawalipi fedha hizo jiji, hali iliyosababisha deni linalofikia zaidi ya bilioni.
Swala hili sio jipya, kila mara migogoro hutokea eneo hili,na husababishwa na madeni ambapo madalali hawa hukusanya kwetu fedha na hua wanazitumia kwa matumizi yao binafsi hivyo kusababisha migogoro ya mara kwa mara ambayo hutuathiri sisi moja kwa moja.
Mgomo huu pia ulileta kero kubwa kwa wananchi ambao walikuwa wanahitaji mahitaji na huduma mbalimbali ikiwemo huduma za choo pamoja na maliwato.
Kinachouma sana ni watu hawa kutuonea na kututisha. Kuna kipindi walitulazimisha kuweka leseni madukani mwetu zenye majina yao na hawakufanywa kitu, serikali ilinyamaza. Kuna wakati walitufungia maduka yetu na serikali ilikaa kimya. Kuna wakati tulishiriki tenda na tulilipa fedha yetu lakini tukaombwa tuwe nao na tuwe tunalipa laki nne, laki mbili wapewe wao laki mbili iende jiji lakini bado wanachukua hela nyingi. Hawalipi kodi popote wameingilia mpaka JWT (jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania) na kujipa vyeo Ili waendelee kutuumiza. Tumewalipa Kodi na hiyo fedha ya jiji hawajaioeleka zaidi ya mwaka bado serikali inawalea....Tukijaribu kuulizia tunafukuzwa, tunanyang'anywa mali zetu na serikali inawalinda watu hao kutukandamiza.
Tunaomba majibu sahihi kutoka serikalini, je ni nani yupo NYUMA ya hili sakata na tutaendelea kuonewa hadi lini?? Nani mnufaika wa haya maeneo??
Serikali itambue sisi wafanyabiashara halisi ni wengi tupo takribani 400, tuna wafanyakazi mathalan mmoja kila duka ni 400, maduka mengine kuna zaid ya mfanyakazi mmoja, hii inapelekea zaid ya kaya 900 ziwe zinategemea mahali hapa. Hao wawekezaji kwa idadi yao hawafiki 50, ni wachache ambao wamehodhi hapa, wapo wenye vibanda kumi, kuna yule maarufu ambae ni mwenyekiti wa halmashauri fulani anavyo zaidi ya thelathini, hata mwenyekiti wa chama fulani anavyo lakini hataki kuiambia serikali ukweli na kuisababishia serikali hasara.
Sisi wafanyabiashara halisi ndio walipa kodi zote, na hawa madalali hawalipii hiyo fedha kodi popote pale, JE KWANINI SISI TUNAUMIZWA NA MIGOGORO ISIYOISHA BAINA YA SERIKALI NA WATU HAWA?? MGOGORO HUU UTAISHA LINI??.
TUMEUMIA SANA KUSHURUTISHWA TUFUNGE MADUKA KWA MASLAHI YA WATU WACHACHE, NA IMEKUWA HULKA KUTISHWA SABABU TUKIKAIDI TUNAAMBIWA TUTAFUKUZWA NA KUNYANG'ANYWA MALI ZETU KAMA WENZETU WALIOJARIBU KUHOJI AMBAO WALIFUKUZWA NA KUNYANG'ANYWA MALI ZAO. NA SERIKALI ILIWALINDA KWA NGUVU KUBWA MADALALI HAWA. SERIKALI ITAMBUE TUMECHOKA NA HII KADHIA NA TUNATAKA MAJIBU SAHIHI NA UFUMBUZI WA HILI
NB: Tunafahamu wapo watu waliingia mkataba na manispaa ya wakati huo na walipewa ardhi wajenge vibanda na walipewa grace period ya miaka kumi na walikaa miaka kumi bure kurudisha gharama zao. Huo ulikuwa mwaka 1990. Mikataba ya namna hii sio migeni hata kariakoo wapemba wengi wamejenga magorofa kwa mikataba hiyo. Hapa Arusha gorofa lenye jengo lenye Equity Bank Ile ardhi ni ya NHC na waliingia mkataba na Justine Nyari wa hivyo. Je miaka zaidi ya thelethini watu hawa bado hawajarudisha faida na wanalipwa wastani wa shilingi million sita kwa mwaka?
Baada ya kipindi cha miaka kumi kuisha, maduka yalirudi jiji na walianza kulipa kodi..wengi wa wajenzi waliuza vibanda na kuhamia kariakoo na wengine kufanya mambo mengine. Waliopo sasa wengi ni wanunuzi hivyo hawana hata Ile mikataba ya wakati huo. Vibanda hivi ni mali ya halamashaur ya jiji kwa 100% lakini watu hawa walibatizwa jina la "wajenzi wawekezaji" na aliekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha ambae kwa sasa ni mbunge wa Arusha mjini. Na walichangia kila kibanda shilingi laki tano kama rushwa akakabidhiwa bwana huyo mnamo mwaka 2017 na kuamua kuwapa cheo hicho. Hivi sasa bado anawalinda na kuwatetea akisema eti ni viinua mgongo vilijenga vibanda kwamba Ile ni mali binafsi. Kwanini mkataba wa mwanzo haufatwi, unavunjwa na hata kama vibanda vilijengwa kwa kiinua mgongo inahusu nini?? SI walikaa bure miaka kumi?? Mbona masoko mengine pia ambayo yalijengwa na watu binafsi hayana migogoro ya hivi??