Prince Luanda
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 2,255
- 2,825
Habari wakuu nipo mtaa wa mchikichi huku kariakoo maduka hayajafunguliwa hadi muda huu kuna nini kwani?
Ngoja niangalie na mitaa mingine.
UPDATES...
Muonekano wa maduka mbalimbali katika soko la Kariakoo hadi saa 8.23 asubuhi huku kufungwa kwa maduka hayo kukihusishwa na uwepo wa mgomo wa wafanyabiashara wa soko hilo kongwe na maarufu Afrika Mashariki.
Wafanyabiashara wa Kariakoo wanafanya mgomo wa kufunga maduka wakishinikiza kupungua kwa kodi wanazotozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
WAFANYABIASHARA WAGOMA KUMFUATA WAZIRI MKUU DODOMA
Ni baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala kuwataka kupeleka malalamiko yao kwa Kassim Majaliwa ambaye anatarajiwa kukutana na uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mawaziri husika na Kamati ya Wafanyabiashara ili kutafuta suluhu ya mgomo huo
Makalla amefika katika Soko Kuu la Kariakoo baada ya Wafanyabiashara kugoma kufungua biashara huku wakitoa malalamiko kadhaa ikiwemo madai ya uwepo wa utitiri wa kodi.
Wakizungumza baada ya Mkuu wa Mkoa kuondoka eneo la Kariakoo, wafanyabiashara wamesisitiza kuwa wanahitaji kuonana na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kutoa kero zao huku wakisisitiza kuendelea kufunga maduka yao
.............
Takwa la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla la wafanyabiashara kumfuata Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa mjini Dodoma limepingwa.
Wafanyabiashara hao walioitisha mkutano mwingine baada ya Makalla kuondoka wamesema wanalipa kodi hivyo Waziri Mkuu Kama anataka kuonana nao awafuate kariakoo na sio wafanyabiashara kumfuata.
Azimio la wafanyabiashara hao endapo mfanyabiashara atakayefungua duka leo ni halali yao.
"Mwenyekiti usiogope tupo nyuma yako usiogope chochote," ameeleza mmoja wa wafanyabiashara hao aliyepanda jukwaani na kutoa muongozo alioudai ni wa kisayansi.