Leo asubuhi nimefika kariakoo kwenye biashara zangu lakini nimekutana na mgomo wa maduka kutofunguliwa
Nilikuwa bungeni kwa wiki kadhaa hivyo sikufuatilia sana mambo ya biashara nikiwaachia vijana
Maduka yamefungwa ingawa baadhi ya wamachinga wanaouza matunda wanaendelea
Sijajua sababu ya msingi zaidi ya ile ya TRA kututaka tuorodheshe store zetu tunazohifadhia mali
Hakuna mfanyabiashara ambaye yupo tayari kwa jambo hilo ,Jambo lilihitaji mjadala mpana
Hakuna fujo ingawa polisi ni wengi wanatembea tembea bila uelekeo
View attachment 2622352