Tetesi: Mgomo wa Daladala kesho tarehe 14/09/2016

Tetesi: Mgomo wa Daladala kesho tarehe 14/09/2016

Habari wakuu,
nimeipata hii taarifa ambayo sio rasmi kuwa kesho tarehe 14/09/2016 daladala za Daressalaam zinatarajia kugoma. Madai ni kukithiri kwa faini za barabarani au wengine wanaita vyeti au kifurushi cha wiki pia kitendo cha madereva wanapelekwa selo kwa kosa la barabarani kila kukicha.
Madereva wanahamasishana kwa SMS kutotoa gari kesho na endapo dereva akijifanya kukaidi gari lake litavunjwa vioo kwa kupigwa na mawe.

Haya wale wenzangu na mimi watumiaji usafiri wa uma nawaasa kuwahi kutoka ili kuepuka usumbufu.

Shushushu yuko kazini
 
Siku hizi askari wamezidi, juzi kuna mtu kapigwa faini kisa kavaa ndala
Kisheria hutakiwi kuvaa kiatu cha wazi unapoendesha coz ikitokea dharula unaweza ukafa kiatu kikimbilia chini ya Pedal ya break.

Ila wanachofanya sasa traffic ni Kukomoana mradi tu pesa iingie serikalini ionekane kua serikali inakusanya pesa za kutosha, si hua mnamsikia Baba Jesca anasemaga hii nchi ni tajiri inapesa nyingi?

Yaani kinachofanyika ni kama vile wanapeana hesabu kwamba ukirudi jioni uje utoe Z-report iliyochangamka kidogo.
 
Waache kulalamika ni sawa kabisa kupigwa faini , kama leo hii serikali wakisema wakague leseni wengi wametoa rushwa kwa maaskari na kupelekewa leseni majumbani kwao bila kupitia shuleni, ww sasa unategemea nn waache wapigwe faini. Hapa home Kuna uwanja wa mpira wa miguu, madereva wa boda boda wanajifundisha pikipiki ndani ya wiki moja, baadaye unamuona road, sasa hapa unategemea nini?
 
Mtoa mada hii habari nimemsikia dereva ambaye nilipanda daladala yake akawa anatutahadhari kuhusu kesho nikawa siamini kumbe ni hakika na bayana,
Asante kwa taarifa acha kesho ije tuone tunatoka kwa style ipi!!

Sent from mTalk
 
Hata kiafya sio salama kuvaa kiatu cha wazi mmoja wenu anaweza kuwa na ugonjwa miguun mwake na akaacha ujiuji wa vidudu vyake hapo chini.
 
KWA TETESI ZA NAMNA HII NI VYEMA KAMA TUNA SEREKALI MAKINI / IZUIE SUALA HILI KUTOKEA KUANZIA MUDA HUU/
 
Kisheria hutakiwi kuvaa kiatu cha wazi unapoendesha coz ikitokea dharula unaweza ukafa kiatu kikimbilia chini ya Pedal ya break.

Ila wanachofanya sasa traffic ni Kukomoana mradi tu pesa iingie serikalini ionekane kua serikali inakusanya pesa za kutosha, si hua mnamsikia Baba Jesca anasemaga hii nchi ni tajiri inapesa nyingi?

Yaani kinachofanyika ni kama vile wanapeana hesabu kwamba ukirudi jioni uje utoe Z-report iliyochangamka kidogo.
kila traffick ana kitu kinachoitwa minus 3, maana yake akiwa kazin lazima akamate makosa matatu ndio akabidhi.
wengi wanakamatwa kwa kosa la kuambiwa gari mbovu, kungekuwa na utaratibu kama mtu hakubaliani na kosa apelekwe mahakamani na kuhukumiwa siku hiyohiyo,
miliki gari la abiria, Bajaji au pikipiki ndo utajua traffick noma
 
HATA UKIWA KWA GARI BINAFSI HUTAKIWI KUVAA NDALA AU KUENDESHA PEKUPEKU
Hairuhusiwi ni kwasababu za kiusalama kuwa zile kamba za open shoes zinaweza kunasa kwenye pedals na ikawa hekaheka. So kwa ujumla si ruhusa kuendesha ukiwa umevaa sandals
 
Hawa wanaogoma kisa wanakamatwa atokee mtu hapa aniambie ni lini ameona dereva na kondakta wa daladala kavaa uniform safi na amevaa inavyotakiwa?

Yale madaladala ya gongolamboto kweli likisimamishwa linakosa kasoro?

Kila siku tunaona daladala zinasimama katikati ya barabara hata kama kituo kipo leo hii ndio wagome eti wanaonewa?

Wanyooshwe tu maanake wameifanya ajira ya daladala imekuwa ya kishenzi wakati dereva anaweza kupata 50,000 per day, gari likisimama siku mbili tu hana hata nauli.
 
Maisha yangu yote nimekuwa nikipingana na takwimu zinazotolewa na institutes mbali mbali Duniani kwamba sisi Waafrika tuna lowest IQ Duniani, lkn kila siku zinavyozidi kwenda nadiriki kusema kwamba Sayansi haidanganyi kwamba ni kweli kabisa sisi tuna lowest IQ Duniani!

Fikiria Mtuhumiwa anagoma kwa sababu hataki Askari amkamate kwa kufanya kosa, na hii ni nchi ambayo ukiondoka nyumbani kurudi salama kama haujavunjika mguu kwa ajali unashukuru Mungu!
Cha kushangaza kabisa kuna kundi la watu hapa watafurahia na kuwaunga mkono daladala wakifikiri kwamba wanamkomoa Raisi Magufuli kwa kuwa hawampendi kumbe hata huyo Magufuli anajaribu tu kuwalinda hao hao wanaompinga, Raisi Magufuli anasafishiwa njia na gari la lake huchunguzwa kabla hajalipanda, hivyo hahitaji daladala ...
nakubaliana na wewe

na cha ajabu wakubwa ndio wamiliki, sisi wala!!

Namshangaa anamchukia JPM
 
Kwa kweli Inabidi ufike wakati watanzania tuweke mazoea pembeni..ivi kama huna kosa,gari liko sawa kila kitu huyo trafic akukamate tu.Ingekuwa amri yangu ningepiga matufuku daladala zote maana hakuna hata moja iliyokamilika..iki tuanze upya na asiyetaka aache.pambafuu
Shida ni kuwa kila Siku wapo barabrani na gari kila Siku zipo na kila siku wanazikamata yaani haina kikomo,wiki,mwezi,miezi,mwaka.ukichunguza sana daah,in afadhali ingetoka amri wenye kumiliki hizi dala dala walete brand new buses sijui
 
Back
Top Bottom