Tetesi: Mgomo wa Daladala kesho tarehe 14/09/2016

Tetesi: Mgomo wa Daladala kesho tarehe 14/09/2016

Kwa hiyo wanataka wasikamatwe na kupigwa faini au kuwekwa ndani wakifanya makosa ya barabarani, kwa hili nipo upande wa serikali
Uko Dar mkuu? Umeisha ona jinsi polisi walivo wengi barabarani? Wanakukamata hata kama body imebonyea kidogo, sijui indicator, sijui break, sijui triangle na mbaya zaidu unakamatwa hapa, unaenda km 2 unakutana na wengine same thing
... utaratibu huu unaboa, unapoteza muda sana pia hata kama nia ni njema....
 
Tatizo kubwa waTZ ni waoga hata kwenye haki zao za msingi huo mgomo ni Maneno tuu
 
Wapewe nafas waseme ni kosa gani si kosa linalowafanya wawekwe ndani na faini tujue kama trafiki wanawaonea ili wananchi tupaze sauti, lakini kugoma hatari, ila yasipuuzwe haya maneno
 
Ila kiukweli polisi wa trafic wamezidisha hizo ticket
 
Kwa kweli Inabidi ufike wakati watanzania tuweke mazoea pembeni..ivi kama huna kosa,gari liko sawa kila kitu huyo trafic akukamate tu.Ingekuwa amri yangu ningepiga matufuku daladala zote maana hakuna hata moja iliyokamilika..iki tuanze upya na asiyetaka aache.pambafuu

Huna uzoefu na magari mkuu ndo mana povu linakutoka tuu!
Trafiki wa dar akilikamata gari hasa haya ya makapuku-daladala haliachwi bila kuandikiwa kosa.
Imekua too much mana hii kamata kamata inafanywa kwa namna ambayo ni hila za wazi kabisaa
 
AVATAR yangu....
Avatar yangu....
Avatar yangu....
 
Kwa kweli Inabidi ufike wakati watanzania tuweke mazoea pembeni..ivi kama huna kosa,gari liko sawa kila kitu huyo trafic akukamate tu.Ingekuwa amri yangu ningepiga matufuku daladala zote maana hakuna hata moja iliyokamilika..iki tuanze upya na asiyetaka aache.pambafuu

Nadhani hii ni effect ya mkuu wa kaya, baba akivuta sigara ht watoto wanatamani kua Kama baba! Kwa hiyo unaona kuvipiga 'matufuku' ndio suluhisho? Alafu watoto wetu wataendaje shule, na sisi vibaruani tutafikaje! Waza hata kdg usiwe mvivu hivi!!
 
Nashauri traffic polisi waongeze mapato kwa kukamata tu,kuna wamiliki wa daladala wameruhusu magari yao kuwekewa ngao nzito mbele na nyuma ambapo ilishakatazwa.
Hizi ngao zinawafanya madereva wa daladala na wengine kutokuwa waangalifu wakijua gari zao hazitadhurika katika ajali ndogo ndogo.
Nashauri kuanzia sasa polisi wakamate hizo gari zenye ngao,kuna mapato mengi sana hapo.
 
Nadhani hii ni effect ya mkuu wa kaya, baba akivuta sigara ht watoto wanatamani kua Kama baba! Kwa hiyo unaona kuvipiga 'matufuku' ndio suluhisho? Alafu watoto wetu wataendaje shule, na sisi vibaruani tutafikaje! Waza hata kdg usiwe mvivu hivi!!
Uvivu???hahaa kwa hiyo maovu yaendelee sababu tu tutafikaje kazini?kwani babu yako mzaa babu alikuwa anaenda shamba na gari lililopo km 50 kutoka kwake?wewe ndo mvivu..kama umenisoma vizuri nilimaanisha zifutwe zote then zianzishwe upya na mpya zenye utaratibu chanya..usikurupuke soma uelewr
 
Hizi issue nyingine wtu mnataka jela,huu uzushi haun tofauti na wale wanaotafutwa kwa kuzua Makamu wa Rais Samia ajiuzulu,ndio hii.
Driver wa brother wangu yeye anasema hana taarifa na anashangaa kusikia hii taarifa na ameuliza driver wenzie Pale Buguruni ila na wao wanasikia tu

Hapa napata Picha kwamba wengi wa Drivers wanaendesha kwa mazoea ila Shule kuhusu Udereva ni Zero kabisaa.Maana kila kosa wanalipitisha kuwa ni haki yao.
Traffic wakiamua kuna gari kibao Dar zitalala.
Wangekuwa kama huku Zanzibar naona wangepiga kelele mpaka basi,maana huku ni Level Seat,ukisimama unalambwa faini.Lakini huko Dar mnajazana ili mradi mlango ufungwe tu,hilo tu ni msaada mkubwa sana Drivers wanapata kwa traffic kuregeza sheria hiyo.
 
Akili za dereva wa daladala haina tofauti na bodaboda,tofauti ipo kwenye vyombo wanavyoendesha
 
Uko Dar mkuu? Umeisha ona jinsi polisi walivo wengi barabarani? Wanakukamata hata kama body imebonyea kidogo, sijui indicator, sijui break, sijui triangle na mbaya zaidu unakamatwa hapa, unaenda km 2 unakutana na wengine same thing
... utaratibu huu unaboa, unapoteza muda sana pia hata kama nia ni njema....
Mimi pia lazima niseme jaman,makosa yote hayo ukiwa nchi za wenzetu gari hiyo hairuhusiwi kuwa barabarani
 
Back
Top Bottom