Tetesi: Mgomo wa Daladala kesho tarehe 14/09/2016

Tetesi: Mgomo wa Daladala kesho tarehe 14/09/2016

Yaaan wagome ili vyeti vizidi hawana akil kabisa hao na tatizo kubwa tanzania kufundishana wenyewe magar watu shule ya udereva hakuna kichwan, wacha mtu akasome apate maarifa na awe na uchungu na ada yake. Unamfundisha mtu udereva halafu anakosa kazi kesho kwa bosi wako unagoma mshahara mdogo anakuambia acha gar ukiacha anakuja mwanafunzi wako asiye na uchungu na ada anakwenda safar unabaki unaduwaa, polen madereva wa tz kwa kutojitambua
 
Nimepanga kesho niwah sana kazini,sasa hawa daladala wasilete ngendembwe,kwanza SUMATRA wanawalea sana,huduma za daladala ni mbovu sana,mabas mengi machakavu,mengine machafu sana ndani,wanapaswa kusimamiwa tena kikamilifu ili watoe huduma bora
 
Habari wakuu,
nimeipata hii taarifa ambayo sio rasmi kuwa kesho tarehe 14/09/2016 daladala za Daressalaam zinatarajia kugoma. Madai ni kukithiri kwa faini za barabarani au wengine wanaita vyeti au kifurushi cha wiki pia kitendo cha madereva wanapelekwa selo kwa kosa la barabarani kila kukicha.
Madereva wanahamasishana kwa SMS kutotoa gari kesho na endapo dereva akijifanya kukaidi gari lake litavunjwa vioo kwa kupigwa na mawe.

Haya wale wenzangu na mimi watumiaji usafiri wa uma nawaasa kuwahi kutoka ili kuepuka usumbufu.
Wathubutu kuvunja gari waone, huu msimu mwingine.
 
Kuvaa ndala ni kosa kwa dereva, labda avae sandles zenye mkanda wa nyuma, kwa sababu ndala inaweza kuteleza kwenye brake wakati amekanyaga na kusababisha ajali.
 
Back
Top Bottom