Mgomo wa Madereva na Wafanyakazi wa mabasi wafanya mgomo Morogoro na Dar

Hapa kwa Mathias upande wa barabara ya zamani kumepooza sana huwa wanatutimulia vumbi tu kutwa nzima hadi kero
 
Haiwezekani jitu limebeba watu 50 kwenye gari liendeshe kizembe bila kukatwa point, Tutakua wajinga sana.

Na sisi abiria tusimame na Serikali, Sheria za barabarani zipo kuwalinda abiria na watumiaji wengine wa barabara.
Punguza siasa na dharau kwenye mambo ya msingi.
 
Hii ndo Tanzania ninayo ifahamu mm,

Ukuwakuta sawa wanavo hubiri/Dai haki kutoka makundi mengine ya jamii kama utazani wao wanauwezo wa kuzifata.

Kuna wakati najiuliza hv ni kweli, watanzania hyo katiba mpya wanayoutaka wataiweza au wanafikiri itawabana viongozi tu 🤣
Katiba mpya imeingiaje hapa?. Madereva Wana madai mengi tu, ila wewe umekalia dai Moja pekee.
 
Wamemdharau Samia, hao dawa yao kuwafutia leseni. Serikali itow tangazo la tahadhari wakipuuzia waondoe mabasi yao hapo stendi wayapaki kwenye yadi zao serikali itumie mabasi haya ya majeshi na ya wale walio tayari. Nchi haiwezi kuendeshwa kwa migomo, tena bila aibu eti hawataki leseni zikatwe point wakifanya makosa! Ni ajabu, hawataki uwazi wanataka waendelee kutoa rushwa ili kuficha makosa yao! Hiyo njia ya kukatwa point ndiyo utaratibu unaotumika ktk nchi zilizoendelea. Hebu serikali iache kubembeleza wananchi kutii sheria. Ifikie mahali sheria iheshimiwe na kila mtu. Wamezoea wamejiongezea nauli.maeneo mengine mpaka mara 2 wanajua serikali inawaogopa maana watagoma, watanzania wanateseka sahv kwa nauli kubwa bado wanaongezewa mateso wakati nchi ina uongozi. Hebu serikali iwe kali.
Mh. Rais badilisha uongozi wa wizara kuanzia waziri, naibu, mkurugenzi mkuu wa LATRA, yule bwana amejisahau sana!
Samiah akifa kesho itakuwaje? Usiongeze vitu kwa kuangalia Leo, fikiria na kesho.
 
tuangalie mfumo wa point wenyewe upo na makosa yapi alafu, jamii yenyewe iseme kama dereva anaonewa au haonewi

View attachment 3680133

View attachment 3680134

hapo dereva leseni inakua na point 15 zikifika 0 , unakua suspended kwa miezi 6.

nchi hii kila mtu analilia katiba muda huu, hivi miongozo hii kwa dereva si ni vitu basic kabisa?
Sema kama hupendi katiba mpya. Usijifiche kwenye mgomo wa madereva.
 
Wamemdharau Samia, hao dawa yao kuwafutia leseni. Serikali itow tangazo la tahadhari wakipuuzia waondoe mabasi yao hapo stendi wayapaki kwenye yadi zao serikali itumie mabasi haya ya majeshi na ya wale walio tayari. Nchi haiwezi kuendeshwa kwa migomo, tena bila aibu eti hawataki leseni zikatwe point wakifanya makosa! Ni ajabu, hawataki uwazi wanataka waendelee kutoa rushwa ili kuficha makosa yao! Hiyo njia ya kukatwa point ndiyo utaratibu unaotumika ktk nchi zilizoendelea. Hebu serikali iache kubembeleza wananchi kutii sheria. Ifikie mahali sheria iheshimiwe na kila mtu. Wamezoea wamejiongezea nauli.maeneo mengine mpaka mara 2 wanajua serikali inawaogopa maana watagoma, watanzania wanateseka sahv kwa nauli kubwa bado wanaongezewa mateso wakati nchi ina uongozi. Hebu serikali iwe kali.
Mh. Rais badilisha uongozi wa wizara kuanzia waziri, naibu, mkurugenzi mkuu wa LATRA, yule bwana amejisahau sana!
Mnavyohemkwa ikiwa wananchi ndio wanatakiwa kutii sheria sasa! Ila ikiwa ni viongozi wa chama chenu mnawatetea. Mmeshaweka double standards acha ziitafune taifa.
 
Haiwezekani jitu limebeba watu 50 kwenye gari liendeshe kizembe bila kukatwa point, Tutakua wajinga sana.

Na sisi abiria tusimame na Serikali, Sheria za barabarani zipo kuwalinda abiria na watumiaji wengine wa barabara.
Wanaotumia Kodi zetu vibaya wanapelekea watu kufa hospitalini ama watt kupata huduma dunia na kufariki.pia wakatwe alama ama mnasemaje
 
Hali ilivyo Mbezi, Dar Es Salaam kwenye Stendi Kuu ya Mabus ambapo inaripotiwa kwa taarifa za awali kuwa kuna mgomo wa Madereva wa Mabus wakigomea kukatwa alama kwenye Leseni zao hivyo wamegoma kuanza safari hii leo.

Hali ya mgomo wa madereva na wafanyakazi wa mabasi imeendelea kushuhudiwa katika Kituo cha Mabasi Msamvu mkoani Morogoro, huku ITV ikikuta mabasi yaliyopangwa kuanza safari saa 12:00 kwenda mikoa mbalimbali yakiwa hayapakii abiria.

Mabasi yanayoonekana kuondoka kituoni ni yale yaliyowasili kutoka safari za masafa marefu na yanayomaliza safari katika kituo hicho.

Baadhi ya madereva na wafanyakazi waliokutwa kituoni wamekataa kuzungumza, huku waliozungumza kwa masharti ya kutorekodiwa wakisema wamelazimika kuwaruhusu abiria waliokuwa wanatarajia kuanza safari Msamvu kurejea nyumbani, kwa hofu ya magari yao kushambuliwa endapo wangeendelea na safari.

Wanasema wao ndio wenye dhamana ya magari hayo na usalama wao pamoja na mali walizokabidhiwa.

Madai makubwa ya madereva yanahusu faini wanazodai kutozwa na askari wa Usalama Barabarani, ambazo kwa baadhi ya makosa zinaweza kufikia hadi shilingi milioni moja kwa dereva, pamoja na hatua za kusimamishwa leseni kwa muda, kupunguziwa pointi na hatimaye kupokonywa leseni.

Madereva hao wanasema baada ya kurejeshewa leseni, baadhi yao hutakiwa kurejea shuleni kabla ya kuruhusiwa kuendelea kuendesha, hali wanayodai kuwaathiri kiuchumi kwa kuwa bila leseni hawawezi kutambulika kazini na wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa familia.

Madereva hao pia wanadai kuwa hata wale wanaoendesha mabasi ya masafa marefu wamekuwa wakisafiri kwa tahadhari, wakizingatia usalama wao, abiria na magari. Wamesema endapo hakuna uhakika wa usalama, wako tayari kusimamisha magari na kusubiri maamuzi ya uongozi wao baada ya kukutana na mamlaka husika katika vikao vinavyotarajiwa kujadili changamoto hizo.
Maafisa wa Polisi wameonekana katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli, Mbezi jijini Dar es Salaam, wakibandua namba za magari yaliyogoma kuondolewa katika stendi wakati wa mgomo wa madereva.

Hatua hiyo imechukuliwa wakati huduma za usafiri zikirejea baada ya mgomo wa madereva wa mabasi ya masafa marefu.

Mgomo huo ulihusishwa na malalamiko ya madereva kuhusu mfumo wa ukataji alama kwenye leseni za udereva.
#EastAfricaTv #TogetherTunawakilisha
 
Kwa hiyo magari tayari yameanza safari mkuu!?
 
mkuu wewe ni mzoefu wa haya mambo hutakiwi kusema hivi, huko ukanda wa sadc sijui taratibu zao zipo vipi labda mapaka nisome documentation zao

ila hapa nchini sheria ipo wazi naweka nukuu
View attachment 3680206
View attachment 3680208

maelezo hayo hapo, dereva anayeendesha chombo cha moto au trela lisilosajiliwa, na mmiliki wote wapo hatiani

kama umefanya kosa na faini inasema kiasi fukani, unatakiwa ulipe kiasi hicho kilichoainishwa tu. ukiona unalipa hela zaidi jua unamatatizo mengine yanayokufanya ukubali faini hiyo kubwa. kila la kheri
Kosa la nani hapo?
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Hali ilivyo Mbezi, Dar Es Salaam kwenye Stendi Kuu ya Mabus ambapo inaripotiwa kwa taarifa za awali kuwa kuna mgomo wa Madereva wa Mabus wakigomea kukatwa alama kwenye Leseni zao hivyo wamegoma kuanza safari hii leo.

Hali ya mgomo wa madereva na wafanyakazi wa mabasi imeendelea kushuhudiwa katika Kituo cha Mabasi Msamvu mkoani Morogoro, huku ITV ikikuta mabasi yaliyopangwa kuanza safari saa 12:00 kwenda mikoa mbalimbali yakiwa hayapakii abiria.

Mabasi yanayoonekana kuondoka kituoni ni yale yaliyowasili kutoka safari za masafa marefu na yanayomaliza safari katika kituo hicho.

Baadhi ya madereva na wafanyakazi waliokutwa kituoni wamekataa kuzungumza, huku waliozungumza kwa masharti ya kutorekodiwa wakisema wamelazimika kuwaruhusu abiria waliokuwa wanatarajia kuanza safari Msamvu kurejea nyumbani, kwa hofu ya magari yao kushambuliwa endapo wangeendelea na safari.

Wanasema wao ndio wenye dhamana ya magari hayo na usalama wao pamoja na mali walizokabidhiwa.

Madai makubwa ya madereva yanahusu faini wanazodai kutozwa na askari wa Usalama Barabarani, ambazo kwa baadhi ya makosa zinaweza kufikia hadi shilingi milioni moja kwa dereva, pamoja na hatua za kusimamishwa leseni kwa muda, kupunguziwa pointi na hatimaye kupokonywa leseni.

Madereva hao wanasema baada ya kurejeshewa leseni, baadhi yao hutakiwa kurejea shuleni kabla ya kuruhusiwa kuendelea kuendesha, hali wanayodai kuwaathiri kiuchumi kwa kuwa bila leseni hawawezi kutambulika kazini na wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa familia.

Madereva hao pia wanadai kuwa hata wale wanaoendesha mabasi ya masafa marefu wamekuwa wakisafiri kwa tahadhari, wakizingatia usalama wao, abiria na magari. Wamesema endapo hakuna uhakika wa usalama, wako tayari kusimamisha magari na kusubiri maamuzi ya uongozi wao baada ya kukutana na mamlaka husika katika vikao vinavyotarajiwa kujadili changamoto hizo.
FB_IMG_1790708197508.jpg
 
Back
Top Bottom