Mgomo wa wafanya biashara ni wa kipuuzi kuwahi kutokea! Wao inawahusu nini mlaji akipandishiwa bei bidhaa? Wao ni wapeleka kodi tu anayelipa ni mlaji

Watumishi mnawachukulia wafanyabiashara kiwepesi sana ndo maana ni ngumu kuelewana.

Mfanyabiashara kwenye faida yake analipa kodi aina zote, analipa mishahara inayolipa kodi na % ya michango ya jamii, analipa manispaa, analipa fire, yote yanatoka kwenye faida yake. Akimaliza kulipa ni wakala wa kutuma ripoti za TRA kuwa kodi zake zimelipwa na akichelewa kutuma dk moja fine inaingia. Huu uwakala gharama zinatoka kwenye faida yake.

Huo mshahara wako ukipewa wote ukalipe PAYE mwenyewe kila mwezi na ufanyiwe ukaguzi na TRA, manunuzi yako ukalipe VAT zako mwenyewe na afanyiwe ukaguzi na TRA unaona ni kazi nyepesi kwako?

Kila ela inayoingia kwenye akaunt yako uambiwe uitolee maelezo au uilipie kodi unadhani ni jambo jepesi?

Mtumishi akishalipa PAYE yake anasumbuliwa na nani? Anafanya nini tena?
 
mpumba
nilivyosoma sentesi ya kwanza nikagundua you have no idea biashara zainafanyaje kazi. Ni bora ungeuliza kwanza kabla ya kuandika chochote
 
We ni nani? Declare interest kwanza tukujue, Kiongozi wa serikali? CCM kigogo? CCM chawa tawi la mtandaoni? Mfanyabiashara? ZAKAYO? Au mlaji wa mwisho?

Huwezi ongelea masuala ya wafanyabiashara kama wewe si mfanyabiasha, ni ujuha kudhani watu maelfu walioweka mitaji yao kwenye maduka hawana akili ila wewe ndio mwenye akili.....
 
Akili yako ni ndogo,,,,,,unaijua efd risit? Ukipandisha Bei tax unalipa according to mauzo yako
 
Punguza jaziba, anza upya kusoma na uelewe mada!

mlaji ndio mlipa kodi zote na kazi ya mfanyabishara ni yeye kuwa mwaminifu kupeleka kodi mahali husika

Anayeumia pindi bidhaa zikipanda, ni mfanyabishara au mlaji?
 
Mleta uzi ana hoja, asikilizwe na ajibiwe kitaalamu na si kijingajinga kama wengi wenu mnavyomjibu.
Hoja yake imenza na mfanyabiashara halipi kodi hapo ndipo hoja yake inakuwa ya kijinga.

Mfanya biashara A, kachukua mkopo M100. Akaajiri watu B na C.

Akapiga kazi akapata faida 20M, akilipa kodi, akawalipa watu B na C mshahara, akawakata kodi kwa niaba ya serikali.

Kwa kupitia mkopo wa huyu mfanyabiashara, Serikali imepata kodi yake na kodi ya wafanyakazi B na C.

Hapo sijagusa makodi mengine anayolipa.

Mleta mada ana hoja mpaka hapo?
 
Kwani wao "hawali"/siyo walaji?Mbona unateseka?
 
Bei zikipandishwa mauzo yanashuka huku Kodi za fremu, service levy,bima nk zipo pale pale achilia mbali marejesho ya mikopo ya Benki.
Sasa Logic ndogo kama hii anashindwa kuelewa, vipi simulteneous equation atatoboa kweli?
 
Mauzo yakishuka maana yake kuna mtu hataweza kula, kuvaa, kujenga na kushindwa kabisa kujikimu kimaisha, na hapo ndipo kutakapotokea hasira za wananchi kudai haki zao

Wao wafanyabishara inawahusu nini maumivu ya walaji?
NAHISI KUNA KUNDI LINAMHARIBIA MAMA.MAANA ISSUE YA SUKARI BADO HAIJAPOA,ISSUE YA BANDARI ILIPOA KIDOGO,NA SASA ISSUE YA WAFABIASHARA.NA BADO ISSUE YA WAFANYAKAZI ,NA KIINUA MGONGO.VYOTE VINAKUJA KIPINDI TUNAELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA UCHAGUZI MKUU.KUKIWA NA TUME HURU CCM INAWEZA KUANGUKA ASUBUHI SANA
 
Mmmhh!

Kichwani uko sawa sawa kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…