DATAZ

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2012
Posts
3,799
Reaction score
10,196
Hadi Sasa ni saa 2:24 asubuhi maduka mengi hayajafunguliwa.


Your browser is not able to display this video.
Licha ya Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila, kuwasisitiza Wafanyabiashara wa Kariakoo kuendelea na shughuli zao kama kawaida, hadi Saa 9 Asubuhi Wafanyabiashara wengi wamefunga Biashara zao katika Mitaa ya Kariakoo, leo Juni 24, 2024

Awali, Chalamila akizungumzia taarifa za mgomo wa Wafanyabiashara wa #Kariakoo alisema "Yawezekana Wafanyabiashara wana Malalamiko ya dhati kabisa lakini Masuala ya mgomo yasichukuliwe kuwa ni jambo la pamoja."

Taarifa ya mgomo ilianza kusambaa kupitia vipeperushi ambavyo havikuwa na jina la Mwandishi, Juni 22, 2024 na sababu zilizotajwa ni kupinga masuala ya Kodi Kandamizi.

========
Pia, soma






==============

Majira ya Saa 4:40 Asubuhi (Saa Nne Asubuhi)

 
Robert

Tafuta machinga unayemjua muulize kafungua? Kama alikuambia, alikuambia kukufurahisha.

Hukuona zile siku tatu?
 
Nasubiri Mida ya saa nne. Ndio tutapata majibu.
Robert

Wale wa kwenye meza huwa wanahifadhi mizigo katika stoo kubwa pale Kariakoo, na stoo zile huwa chini ya viongozi. Sidhani kama wanaweza kuruhusu kutoa mizigo wakati tumekubaliana kwamba leo tuna jambo moja.

Na vilevile wenye vimeza muda mwingine wanapewa mzigo na watu wa kwenye fremu kuuza mzigo ambao umekaa muda mrefu na mzigo mpya ushaingia hivyo bado kuna kutegemea kwa kiasi fulani.
 

Ni kweli kabisa
Na hata baadhi ya machinga(wenye vimeza) mizigo ya kuuza wanapewa na wenye maduka kwa mali kauli.

Ngoja tuone
 

Kiongozi wa wafañyabiashara wa Kariakoo lakini kakanusha.
Sasa hilo tangazo la kuwa kutakuwa na mgomo lilitolewa na nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…