Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Waalimu wengi uchaguzi wa 2005 walionyesha mwamko wa mageuzi, wengine wakaenda kugombea udiwani kupitia vyama vya upinzani. Walitiwa moyo sana na waalimu wenzao.
Tunachokiona leo ni kulipiza kisasi. Nasikia JK ni bingwa wa visasi.
.
si mara ya kwanza injuction order kutolewa nje ya muda wa kazi, katika ile kesi ya kusimamisha ucgaguzi wa meya kitwana kondo ilifanyika hivyo hivyo, jawabu nikuwa je mtu wa kawaida anaweza kupata huduma hii chaP CHAP KAMA SERIKALI ILIVYOIPATA HATA BAADA YA MASAA YA KAZI?
![]()
Rais wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT, Gratias Mukoba
akikwepa mawe kutoka kwa waalimu waliojawa na jazba akikimbilia
gari la polisi , mkutano wa maandalizi ya mgomo ulivunjika, Makakama
Kuu Divisheni ya Kazi ilizuia mgomo wa walimu.
Tunawahitaji sana walimu katika vita dhidi ya mafisadi kwani wanatumiwa sana kusimamia uchaguzi na kuwaingiza mafisadi katika madaraka. Ni high time kwao kujua kwamba this time imekula kwao na wakipewa dhamana ya kusimamia uchaguzi tena wasimamie haki na kuhakikisha mafisadi hawana nafasi tena.
ni miaka mi3 tu iliopita haya hhayakuweza kutokea au watu tulikuwa hatuna muamko.. the pace is good tusikate tamaa kila mtu akanyage mguu mahali pake na kuyakataa haya na kupreach kwa wengi wizi wa CCM naamini mpaka 2010 mambo yatakuwa ktk level nzuri na tutakuwa tumeshawazika kabisa CCM.. kama kunamtua ameangalia taarifa ta habari ya leo saa moja asbh chanel tena atanielewa ninaposimulia kuwa sikuamini macho yangu wazee watarime walivokuwa na mwamko mkubwa na naashilia kusema kuwa muamko wao ni mkubwa kiliko vijana wengi wa mjini
Mi nadhani hata kama mahakama imetoa zuio la mgomo wao waendelee kugoma tu kwani watawafanya nini? Najua hata jeuri ya kuwafukuza kazi hawana kwani hao walimu wa kuziba hizo nafasi hata nusu yake hawatapatikana......Walimu wana hali mbaya sana jamani tuache utani nadhani hata ile morali ya kazi hawana tena.
Migomo ni suluhisho la matatizo? Je haki za walimu zitapatikana kwa migomo? Nimesikiliza vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na sakata la madai ya walimu. Ninashindwa kuelewa madai ya walimu ni ya haki au la? Sidhani kama walimu ni wajinga wadai kitu ambacho si haki yao. Kilimanjaro nimesikia wahusika wa malipo ya walimu walikuwa wakihaha kuhakikisha walimu wanalipwa ili wasigome. Na pia kutishiwa wasigome. Ina maana serikali ni lazima iamshwe ndio ilipe haki za walimu?
Umefika wakati sasa wa kuwa na utaratibu wa kuhakiki haki ya kila mfanyakazi wa serikali na kulipwa kwa wakati na kwa haki yake. Kwa technologia iliyopo sidhani kwamba ni vigumu kutatua haki za walimu. Unajua mwalimu akienda likizo anatakiwa kulipwa nini na nini halipwi. Itengenzwe programme amayo ukiikomand inatoa kiasi cha kila mwalimu. Wanaofanya mahesabu ya malipo ya walimu kazi yao ni ipi.
Swali: Migomo ina madhara kwa nchi na kidunia?