Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,904
- 1,064
1. Mara zote mfanye mwalimu mwoga kwa chama na serikali.
2. Mlaghai kwa wito na si kipato.
3. Mfundishe kuwa mpole asidai haki.
4. Mfanye asiajiriwe sekta nyingine ili umtumie.
5.Mlipe kidogo atumike milele.
6. Mtumie kwenye chaguzi na sensa, ajione bora.
7. Msifie kila siku, avimbe kichwa.
8. Weka viongozi wa CWT asifurukute.
9. Mtumie kama ubao wa matangazo kwa t-shirts za chama.
10. Mara zote wagawe na kuwatawala.
1. Mara zote mfanye mwalimu mwoga kwa chama na serikali.
2. Mlaghai kwa wito na si kipato.
3. Mfundishe kuwa mpole asidai haki.
4. Mfanye asiajiriwe sekta nyingine ili umtumie.
5.Mlipe kidogo atumike milele.
6. Mtumie kwenye chaguzi na sensa, ajione bora.
7. Msifie kila siku, avimbe kichwa.
8. Weka viongozi wa CWT asifurukute.
9. Mtumie kama ubao wa matangazo kwa t-shirts za chama.
10. Mara zote wagawe na kuwatawala.
Huu si udhalilishaji kwa Chama tawala? Maana naona kila joke ina Siasa... Au mnaichukulia utani? Kwa wale ambao wanaona hii inakidhalilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) tafadhali tutumie malalamiko na hii topic itafungwa na kuondoshwa MARA MOJA!Mijinga ndivyo iliwavyo !!!!! kanga na pilau na t.shirt na vijikofia, wanauza uhuru kwa bei ya kutupa halafu kesho wa kwanza kulalamika, na bado.
Habari zilizo fika sasa hivi ni kwamba COURT OF APPEAL imefuta hukumu ya HIGH COURT na walimu sasa ruksa kugoma!
Sijui kama tutafika, hebu kumbuka migomo na migogoro ya NMB, wazee wa EAF, TRL, Wanafunzi vyuo vikuu, sasa walimu na walivo wengi kila kona ya Tz, nao.... hivi kutakalika?
Taratibu naona ile AMANI NA UTULIVU VINA YOYOMA...!
(Mod, p/se waweza iunga kwa ile ya zamani)
Naomba wana JF mnieleweshe mgomo huu unawahusu waalimu wote hata wa Sekondari na Vyuo?
Ni walimu wa primary and secondary schools...
Malipo bado yanahakikiwa
Bwana uturehemu...
Ni walimu wa primary and secondary schools...
Malipo bado yanahakikiwa
Bwana uturehemu...
Yana hakikiwa kwa myaka mingapi? kwani madai haya hayaja anza leo...
Hawa walimu wetu waliotufikisha hapa tulipo pamoja na kufanya kazi katika mazingira magumu, hawathaminiwi kabisa, wakati bila wao hata sisi hizi keyboard tungeona herufi juu yake ni maua, kweli serikali haiwatendei haki!
Hichi kisingizio cha kuhakikiwa hadi lini? na kwanini hiyo kazi isifanyike huko huko halmashauli ama wilaya husika na badala yake inafanywa makao makuu kuliko jaa wajanja ambao huishia kujilipa hela hizo kwa kughushi badala ya wahusika? kwa kweli sielewi, sielewi utendaji wa serikali yangu!
yaani ni kama ngoma ya mdundiko kila anaye jisikia na popote alipo anaibuka na kuserebuka, mara wa kuzuia migomo mahakami kinyume cha sheria, mara wa kutishia watu na kunyamazisha vyombo vya habari, mara wa kufukuza wanachuo, mara wakutishia kwamba mafisadi wakikamwatwa nchi haitawaliki, kila mmoja na lwake kwa kwenda mbele!
Nashukuru sana kwa taarifa. Sasa tuone mambo yatakwendaje? Walimu na watu wengine lazima wapewe uhuru wa kutumia haki yao ya kikatiba kuibana serikali iwalipe madai yao.