Habari zilizo fika sasa hivi ni kwamba COURT OF APPEAL imefuta hukumu ya HIGH COURT na walimu sasa ruksa kugoma!
Sijui kama tutafika, hebu kumbuka migomo na migogoro ya NMB, wazee wa EAF, TRL, Wanafunzi vyuo vikuu, sasa walimu na walivo wengi kila kona ya Tz, nao.... hivi kutakalika?
Taratibu naona ile AMANI NA UTULIVU VINA YOYOMA...!
(Mod, p/se waweza iunga kwa ile ya zamani)

sasa wakigoma si shule zinafungwa na wote wanaamriwa kurudi nyumbani hadi waandike barua ya kuomba msamaha na kuahidi kutoshiriki migomo mingine huko mbeleni?
Jana nimeona kwenye habari Pinda yuko huko dodoma kwa ziara.Wananchi wanaonekana bado wanazo zile Tshirts za CCM 2005 zenye picha ya Kikwete wakati wa uchaguzi zinaonekana bado mpyaaaa! Tunahitaji kuelimisha vijijini maana ndipo uliko mtaji wa CCM
Katibu Mkuu Kiongozi amewapiga mkwara mzito leo. Amesema kuwa hukumu ya mahakama ya rufani haifanyi mgomo wao kuwa halali. Anasema serikali inakamilisha malipo na hadi kufikia mwisho wa mwezi huu walimu watakuwa wamelipwa.
Amewaonya kuwa mwalimu atakayegoma, mshahara wake akachukue kwa yule aliyemtaka agome.
Serikali pia imekwenda mahakamani kutaka hukumu ya Mahakama ya Rufani ipitiwe upya.
Picha inaanza sasa
CCM watishika na migomo ya waalimu washawisi serikali kuikomesha
Na Jackson Odoyo
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeitaka serikali iwachukulie hatua za kisheria viongozi wa Chama cha Walimu nchini (CWT), kikidai viongozi hao wana agenda ya siri ya kutaka kuharibu utulivu na mshikamano wa nchi kwa kuhamasisha migomo ya walimu.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana ofisini kwake jijini Dar es Salam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itifaki na Uenezi, John Chiligati alisema Serikali inapaswa kuwashughulikia viongozi hao na kwamba, ina haki ya kufanya hivyo kwa sababu ndiyo mwajiri wao.
''Serikali kama mwajiri wao ina haki kuwashughulikia viongozi wa Chama cha Walimu wanaohamasisha mgomo huu kwa kuwa, wana agenda ya siri ya kuharibu utulivu na mshikamano wa nchi yetu, serikali isiwaonee huruma,'' alisema Chiligati.
Alisema CCM imeshangazwa na kauli ya Rais wa CWT ya kuitisha mgomo usio na ukomo wa nchi nzima, wakati uhakiki wa madeni ya walimu umekamilika na wataanza kulipwa kunzia leo.
Katika mazingira haya tunajiuliza mgomo huo una nia gani hasa wakati kile Walimu walichokuwa wanakipigania sasa kimepatikana, tunajiuliza mgomo wa nini na hao wanaopigania mgomo uanze kesho (leo) nia yao ni ipi?, alihoji Chiligati.
Hata hiyo Chiligati alisema CCM inawasihii na kuwashauri Walimu wenye nia safi kutojiingiza katika mgomo huo aliosema una nia mbaya na badala yake waendelee na kazi.
Aliongeza kuwa kitendo cha Walimu hao kuingia kwenye mgomo huo batili na haramu kwa kuwa malengo yake ni kuumiza watoto na kuingiza wasiwasi ndani ya nchi bila ya sababu za msingi.
Katika hatua nyingine Chiligati alisema kwamba, iwapo kuna mtu yeyote mwenye ushahidi kuwa Tanil Somaiya anahusika na tuhuma za rushwa ya rada pamoja na kukwepa kodi za Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) apeleke ushahidi huo katika vyombo vya dola.
''Somaiya alitoa Sh400 milioni kwa ajili ya kufanikisha Uchaguzi Mkuu na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM utakaofanyika Desemba 16 mwaka huu Mjini Dodoma. Tumepokea msaada huo kwa mikono miwili na ilifanyika hadharani pasipo kificho, wala si kweli kwamba CCM inapokea fedha zilizopatikana kwa njia haramu na wala si ishara ya kukumbatia ufisadi,'' Chiligati alisisitiza.
Wakati huohuo, Chiligati alisema CCM imesikitishwa na namna ambavyo viongozi wa vyama vya upinzani walivyokipaka matope chama hicho kupitia sakata la Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA)
Alisema ukweli ni kwamba, CCM haikuchukua fedha katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kuongeza kuwa iwapo katika orodha ya watuhumiwa wa EPA wapo wana CCM au wakereketwa wake, walifanya hivyo kwa maslahi yao wenyewe na wala hawakutumwa na chama hicho.
Source: Mwananchi.
Hivi kweli kiongozi (Chiligati) tena senior katika chama kutoa maoni, ushauri au maelekezo kama hayo kwa serikali si kuhatarisha amani nchini!! Walimu wanadai haki yao, leo hii kiongozi wa chama kinachoongoza serikali kutoa madai kama hayo ya kuwashughulikia viongozi wa CWT ni ukosefu wa busara na fadhila kwa walimu wetu. Na hii isiangaliwe kwa CWT pekee, kutakuwa na vyama vingine ambavyo vinawaunganisha wafanyakazi wengine nchini ambavyo navyo vitapewa vitisho vya namna hiyo ili visidai haki yao.
Kisieleweke kitu hadi haki itakapopatikana.
Kumshughulikia Mkoba (Rais wa CWT) hakitasaidia lolote bali itaamsha chuki zaidi ya walimu dhidi ya serikali. sasa hapa nani atakuwa auamia.....ni wanafunzi ambao wanapaswa kupewa haki yao ya msingi (ELIMU). Muda wa kutishiana umepitwa na wakati, serikali inawajibu wa kutoa haki kwa hawa walimu, waliokuwa wafanyakazi wa EAC na wengine. Tuache mambo ya kuburuzana na kupeana vitisho, kisa kudai HAKI.
mi nwashauri walimu wagome tu maana mimi ya EAC imenipa fundisho kubwa sana hii serikali yetu imezoea kutudanganya kama mtoto si unajua mtoto anavyolilia nguo dukani then unampa pipi asilie ndo hivyo wanavyofanya watawalipa vihela vidogo vidongo watadanganya wengine walikuwa vibaruana wengine vyeti vyao ni feki alimradi mchezo uishe kwa penati, sasa wao wagome tu baada ya muda na sisi wenye watoto wetu wanaosoma izi shule za kina kanumba tutaandamana mpaka ikulu kumuuliza rais watoto wetu itakuwaje kama atawaombea kwa muda Mzizimz au Almutazin, STmary's poa lasivyo tubaki nyumbani kufundisha watoto wetu tusiende kazini maana utendaji utakuwa hafifu na kufukuzwa kazi siku hizi ni kama kunywa maji, hapo basi uchumi utazidi kudidimia na watu wataamua kuingia msituni, wakirudi huko na wawekezaji mnaowaheshimu kama miungu watakimbia ahh hii movie ni nzuri mno
CCM watishika na migomo ya waalimu washawisi serikali kuikomesha
Na Jackson Odoyo
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeitaka serikali iwachukulie hatua za kisheria viongozi wa Chama cha Walimu nchini (CWT), kikidai viongozi hao wana agenda ya siri ya kutaka kuharibu utulivu na mshikamano wa nchi kwa kuhamasisha migomo ya walimu.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana ofisini kwake jijini Dar es Salam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itifaki na Uenezi, John Chiligati alisema Serikali inapaswa kuwashughulikia viongozi hao na kwamba, ina haki ya kufanya hivyo kwa sababu ndiyo mwajiri wao.
''Serikali kama mwajiri wao ina haki kuwashughulikia viongozi wa Chama cha Walimu wanaohamasisha mgomo huu kwa kuwa, wana agenda ya siri ya kuharibu utulivu na mshikamano wa nchi yetu, serikali isiwaonee huruma,'' alisema Chiligati.
Alisema CCM imeshangazwa na kauli ya Rais wa CWT ya kuitisha mgomo usio na ukomo wa nchi nzima, wakati uhakiki wa madeni ya walimu umekamilika na wataanza kulipwa kunzia leo.
Katika mazingira haya tunajiuliza mgomo huo una nia gani hasa wakati kile Walimu walichokuwa wanakipigania sasa kimepatikana, tunajiuliza mgomo wa nini na hao wanaopigania mgomo uanze kesho (leo) nia yao ni ipi?, alihoji Chiligati.
Hata hiyo Chiligati alisema CCM inawasihii na kuwashauri Walimu wenye nia safi kutojiingiza katika mgomo huo aliosema una nia mbaya na badala yake waendelee na kazi.
Aliongeza kuwa kitendo cha Walimu hao kuingia kwenye mgomo huo batili na haramu kwa kuwa malengo yake ni kuumiza watoto na kuingiza wasiwasi ndani ya nchi bila ya sababu za msingi.
Katika hatua nyingine Chiligati alisema kwamba, iwapo kuna mtu yeyote mwenye ushahidi kuwa Tanil Somaiya anahusika na tuhuma za rushwa ya rada pamoja na kukwepa kodi za Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) apeleke ushahidi huo katika vyombo vya dola.
''Somaiya alitoa Sh400 milioni kwa ajili ya kufanikisha Uchaguzi Mkuu na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM utakaofanyika Desemba 16 mwaka huu Mjini Dodoma. Tumepokea msaada huo kwa mikono miwili na ilifanyika hadharani pasipo kificho, wala si kweli kwamba CCM inapokea fedha zilizopatikana kwa njia haramu na wala si ishara ya kukumbatia ufisadi,'' Chiligati alisisitiza.
Wakati huohuo, Chiligati alisema CCM imesikitishwa na namna ambavyo viongozi wa vyama vya upinzani walivyokipaka matope chama hicho kupitia sakata la Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA)
Alisema ukweli ni kwamba, CCM haikuchukua fedha katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kuongeza kuwa iwapo katika orodha ya watuhumiwa wa EPA wapo wana CCM au wakereketwa wake, walifanya hivyo kwa maslahi yao wenyewe na wala hawakutumwa na chama hicho.
Source: Mwananchi.
1. Mara zote mfanye mwalimu mwoga kwa chama na serikali.
2. Mlaghai kwa wito na si kipato.
3. Mfundishe kuwa mpole asidai haki.
4. Mfanye asiajiriwe sekta nyingine ili umtumie.
5.Mlipe kidogo atumike milele.
6. Mtumie kwenye chaguzi na sensa, ajione bora.
7. Msifie kila siku, avimbe kichwa.
8. Weka viongozi wa CWT asifurukute.
9. Mtumie kama ubao wa matangazo kwa t-shirts za chama.
10. Mara zote wagawe na kuwatawala.