MGOMO: Wafanyabiashara Kariakoo kufunga biashara zao kuanzia 24/6/2024 mpaka changamoto zao zitakapotatuliwa'

MGOMO: Wafanyabiashara Kariakoo kufunga biashara zao kuanzia 24/6/2024 mpaka changamoto zao zitakapotatuliwa'

toriyama

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2014
Posts
1,139
Reaction score
2,223
Wafanyabiashara wote wa viunga vya Kariakoo mnatakiwa kufunga biashara zenu zote ikiwemo maduka yenu, ofisi zetu na chochote unachokifanya kuanzia Jumatatu ya Juni 24, 2024 bila ukomo hadi pale changamoto zetu zote za kibiashara zitakapoweza kutatuliwa.

Mikoa ya Mbeya, Iringa, Mwanza, Arusha, Ruvuma, Kagera na Rukwa mtaanza kufunga biashara zetu kuanzia siku ya Jumanne ya Juni 25, 2024 bila ukomo.

Kuanzia siku ya Jumatano ya Juni 26, 2024 wafanyabiashara wote nchini tutaungana kufunga biashara zetu hadi pale changamoto zetu zote zitakapopata ufumbuzi wa kudumu.

Kutakuwa na kikosi kazi cha kupitia ili kukagua ofisi au biashara ambazo hazijafungwa ili kuhakikisha wote tunaungana kupambana na udhalimu huu wa kodi kandamizi.

----
Pia soma
Tetesi: - Wafanyabiashara Kariakoo kugoma muda wowote kutokana na madai yao kupuuzwa

20240622_155010.jpg
 
Wajinga hao, ngoja soko la Ubungo likamilike, mchina analeta mzigo moja kwa moja, wafanyabiashara wanachukua bila udalali. Ni ujinga wa watu wa kariakoo kuwashawishi wafanyabiashara wa kigeni wasichukue risiti, baadae wakitoka nje ya kariakoo wanakamatwa, wakikamatwa hao wafanyabiashara wanawaruka. Pumbafu sana, na ndio inafanya wageni wakimbie

Serikali itengeneze karikoo zaidi ya nne hapo jijini, hii itaondoa hali ya monopoly kama ilivyo kwenye sukari.
 
Ubungo Siyo Tanzania pale 😃😃
 
WAFANYABISHARA KARIAKOO WATOA TAMKO KUFUNGA BIASHARA ZAO kuanzia Jumatatu 24/6/2024

Mikoa mingine pia yatajwa.

Wafanyabiashara wote wa viunga vya Kariakoo mnatakiwa kufunga biashara zenu zote ikiwemo maduka yenu, ofisi zetu na chochote unachokifanya kuanzia Jumatatu ya Juni 24, 2024 bila ukomo hadi pale changamoto zetu zote za kiabishara zitakapoweza kutatuliwa.

Mikoa ya Mbeya, Iringa, Mwanza, Arusha, Ruvuma, Kagera na Rukwa mtaanza kufunga biashara zetu kuanzia siku ya Jumanne ya Juni 25, 2024 bila ukomo.

Kuanzia siku ya Jumatano ya Juni 26, 2024 wafanyabiashara wote nchini tutaungana kufunga biashara zetu hadi pale changamoto zetu zote zitakapopata ufumbuzi wa kudumu

Kutakuwa na kikosi kazi cha kupitia ili kukagua ofisi au biashara ambazo hazijafungwa ili kuhakikisha wote tunaungana kupambana na udhalimu huu wa kodi kandamizi.

ANGALIZO
Wafanyabiashara watakaokaidi agizo hili mshale wa jicho utakuwa haki yake

----
Pia soma Tetesi: - Wafanyabiashara Kariakoo kugoma muda wowote kutokana na madai yao kupuuzwa

View attachment 3023083
Hiyo ndiyo dawa.
 
Huu ni mkakati mahususi na umekuwa ukifanyika kila wakati kiongozi wa nchi anapokuwa Muislamu ili kuhakikisha utawala huo unakosa utulivu na kuleta chuki baina ya wananchi na utawala uliopo madarakani.
Wakati wa utawala wa Magufuli wafanyabiashara walionewa sana ikiwa ni pamoja kufunguliwa kesi za uhujumu uchumi na kuporwa pesa kwenye akaunti zao benki lakini hatukushuhudia hata kunguni kuandamana au kugoma,
Huu ni unafiki na tukae tukijua kwa unafiki tulionao Watanzania hatutofanikiwa kujinasua kutoka kwenye makucha ya utawala dhalimu wa ccm.
 
Kwa Hali ilivyo kariakoo kunachochea sana watu kukwepa kutoa risiti na serekali kupoteza mapato, fikiria Hali ya eneo Zima kutopitika, biashara kuuzwa barabarani, uwepo wa magari kuziba barabara, baiskeli, na fujo zote mtu Hana pa kupita je Mkuu wa Mkoa unajua maana ya CBD au umeweka siasa mbele!? Fanya kitu mheshimiwa otherwise inaonekana Jiji limekushinda!! Kwani siasa zako zimefanya watendaji wa Jiji kuwa wapenzi watazamaji
 
Back
Top Bottom