Zanaki,
Mimi ni mfuatiliaji wa mijadala hii ya siasa TZ lakini nina wasiwasi sana na ukweli kamili wa habari hii. Ningelikuwa na muda ningeichambua mstari kwa mstari lakini kwasasa nitaandika machache.
Moja huyo kijana wa JK ni mpiga debe wa huyo mgombea wa UVCCM tokea wakati Lowassa ni waziri mkuu, unaweza kurudi nyuma kusoma maandishi mbalimbali hapa JF na utalikuta hilo.
Pili mfano wa Zuma na Mbeki ni tofauti kabisa na mfano wa JK na Lowassa. Kwanza Mbeki hakuwahi kuwa rafiki yake Zuma, in fact Zuma na kundi lake muda wote walikuwa wanamwona Mbeki kama wa kuja ambaye hana historia ya mapambano ya SA. Sioni chuki yoyote ya wazi kati ya JK na Lowassa.
Tatu, mtu kama Mulla wa Mbeya ni mtandao kwa muda mrefu na hata kwenye uchaguzi wa mwaka jana wakati Lowassa bado ni PM alikuwa ni mtu wao. Sijaona nyendo zozote tofauti za Mulla kwamba sasa kaanza kumsaliti JK kwa ajili ya Lowassa.
Nne, hao wenyeviti watatu wa CC ni idadi ndogo sana katika CC na mwenyekiti wa CCM ana nguvu kubwa kwenye CC kiasi kwamba sio rahisi ongezeko la hao watatu kuweza kuleta maasi. Pia kuna wazee wa chama hasa Mwinyi na Kawawa ambao wana nguvu kubwa mno kwenye hicho chama na dalili zote zinaonyesha wanamuunga mkono JK.
Ukisoma kwa makini unagundua mwandishi anatumia info ambayo iko kwenye public kutaka kujenga chuki kati ya Lowassa na JK. Kubenea ni stakeholder kwenye hili maana kwa yeye angetaka kwa nguvu zote kuona Lowassa na JK wanakosana.
Mimi naona hii habari ni kama ile ya JK na Prof. Mwandosya ambayo watu wanatumia ukweli mdogo kujenga tatizo kubwa. Baada ya kushindwa kule kwa prof sasa wanaanza kuhamia kwa Lowassa.
Binafsi simtaki Lowassa tokea enzi za Nyerere na naamini hana nafasi tena ya kuwa rais au PM wa Tanzania. Anaweza kurudi kwenye baraza la mawaziri lakini sio kuwa rais au PM. Pamoja na hayo, pia sipendi kulishwa sumu na hawa waandishi ambao chuki zao binafsi zinakuwa mbele kuliko ukweli wa habari.