Mgongano: Serikali Vs. Mwanahalisi - Mipaka ya Maoni?

Mgongano: Serikali Vs. Mwanahalisi - Mipaka ya Maoni?

kumbe kiswahili unajua sasa hivi vibroken inglish vya nini aua tukuone msomi sisi tusio na shule


Kumbe huna shule,nilikua nakulaumu bure tu.Maanke hata mkato hujui kuweka wala alama ya kushangaa.kazi kuchonga vyeti tuu.


I'm so sorry.
 
Zanaki,

Mimi ni mfuatiliaji wa mijadala hii ya siasa TZ lakini nina wasiwasi sana na ukweli kamili wa habari hii. Ningelikuwa na muda ningeichambua mstari kwa mstari lakini kwasasa nitaandika machache.

Moja huyo kijana wa JK ni mpiga debe wa huyo mgombea wa UVCCM tokea wakati Lowassa ni waziri mkuu, unaweza kurudi nyuma kusoma maandishi mbalimbali hapa JF na utalikuta hilo.

Pili mfano wa Zuma na Mbeki ni tofauti kabisa na mfano wa JK na Lowassa. Kwanza Mbeki hakuwahi kuwa rafiki yake Zuma, in fact Zuma na kundi lake muda wote walikuwa wanamwona Mbeki kama wa kuja ambaye hana historia ya mapambano ya SA. Sioni chuki yoyote ya wazi kati ya JK na Lowassa.

Tatu, mtu kama Mulla wa Mbeya ni mtandao kwa muda mrefu na hata kwenye uchaguzi wa mwaka jana wakati Lowassa bado ni PM alikuwa ni mtu wao. Sijaona nyendo zozote tofauti za Mulla kwamba sasa kaanza kumsaliti JK kwa ajili ya Lowassa.

Nne, hao wenyeviti watatu wa CC ni idadi ndogo sana katika CC na mwenyekiti wa CCM ana nguvu kubwa kwenye CC kiasi kwamba sio rahisi ongezeko la hao watatu kuweza kuleta maasi. Pia kuna wazee wa chama hasa Mwinyi na Kawawa ambao wana nguvu kubwa mno kwenye hicho chama na dalili zote zinaonyesha wanamuunga mkono JK.

Ukisoma kwa makini unagundua mwandishi anatumia info ambayo iko kwenye public kutaka kujenga chuki kati ya Lowassa na JK. Kubenea ni stakeholder kwenye hili maana kwa yeye angetaka kwa nguvu zote kuona Lowassa na JK wanakosana.

Mimi naona hii habari ni kama ile ya JK na Prof. Mwandosya ambayo watu wanatumia ukweli mdogo kujenga tatizo kubwa. Baada ya kushindwa kule kwa prof sasa wanaanza kuhamia kwa Lowassa.

Binafsi simtaki Lowassa tokea enzi za Nyerere na naamini hana nafasi tena ya kuwa rais au PM wa Tanzania. Anaweza kurudi kwenye baraza la mawaziri lakini sio kuwa rais au PM. Pamoja na hayo, pia sipendi kulishwa sumu na hawa waandishi ambao chuki zao binafsi zinakuwa mbele kuliko ukweli wa habari.

Ningeshangaa sana usingemtaja Mwandosya hapa. Wewe tatizo lako ni lile lile. USILOLIJUA wewe siku zote HALINA UKWELI! WEWE ni nani hadi ujue kila kitu NCHI hii! Rudi kwenye HOJA alizododosa Mwanakijiji! Makala hiyo ya Kubenea ina TAATHIRA gani hadi Serikali KUIVIMBIA kiasi kile? Wanaomsakama Mwandosya ni hao hao MAfisadi. Tuletee makala ambayo umewahi kusikia Mwanahalisi limemsakama Mwandosya! Hakuna mtu ambaye amekuwa akiufahamisha umma kuhusu Mwandosya kusakamwa na Wanamtandao kama Kubenea na gazeti lake! Lakini sasa unapoteza MAANA nzima ya mjadala huu kwa kumuingiza huyo Profesa Mnyakyusa! HATUTAKI kumsikia humu kwa sababu hahusiki. Sio NEWS kabisa kwenye hii tread! Sawa!
 
Kulikuwa na taarifa za awali kuwa Kubenea anatafutwa kwa nguvu na Polisi hapa JF, kwa sasa taarifa zinazoingia zinadai polisi wamefika ofisi za MwanaHalisi na kukuta gari lake ilhali yeye (Kubenea) akiwa hayupo ofisini hapo.

Awali polisi walimtaka ajisalimishe kwao na hakutekeleza hilo hivyo wakachukua hatua za kumfuata wao (uvamizi?) ofisini kwake.

Polisi wanaendelea na msako wa kumpata, taarifa zaidi tutawafahamisha kadiri muda unavyokwenda. Kuna dokezo kuwa kuna wengine zaidi watafuata katika msako huu.

Just an alert!

*****UPDATE*****

Kubenea atinga polisi Makao Makuu
 
............NOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOooooooooo!!!! Pls GOD forbid; Hiii ibakie kuwa tetesi!!! 🙁
 
............NOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOooooooooo!!!! Pls GOD forbid; Hiii ibakie kuwa tetesi!!! 🙁

Si tetesi, hayupo nyumbani, ofisini na polisi wanahaha kumtafuta. Alitakiwa toka jana aende na leo wanataka aende, inaonekana yuko nje ya Dar, anadai atakwenda polisi leo akiwa na mwanasheria wake, lakini alipo bado ni kitendawili
 
Something very fishy, gari lake lime onekana ofisini lakini mwenyewe katoweka lets pray for his safety....
 
Tusaidie invisible, ametoweka au ametoweshwa?
Mimi ni mjumbe tu, nina bahati mbaya kuwa sipo maeneo yangu ya kawaida, nilitarajia kuwa huko kesho lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu siendi hata kesho...

Taarifa nilizozipata 'za uhakika' ni kuwa 'katoweka' na kama ulisoma awali MMKJJ alisema 'walimshauri' asiende polisi. Vyombo vya nje vimetumiwa taarifa juu ya hili na wameahidi ushirikiano wa karibu sana.

Still an alert!
 
Jamani Mungu amlinde alipo Kubenea, mimi nadhani mambo haya yalikuwa yakitokea Russia tu....sasa Tanzania tena!! Uhuru wa kujieleza uko wapi?
 
Taarifa nilizozipata 'za uhakika' ni kuwa 'katoweka' na kama ulisoma awali MMKJJ alisema 'walimshauri' asiende polisi. Vyombo vya nje vimetumiwa taarifa juu ya hili na wameahidi ushirikiano wa karibu sana.

Still an alert!

For or against Kubenea?
 
Jamani Mungu amlinde alipo Kubenea, mimi nadhani mambo haya yalikuwa yakitokea Russia tu....sasa Tanzania tena!! Uhuru wa kujieleza uko wapi?
Uhuru?

Tz1, wameahidi protection against journalists like Kubenea.
 
Labda ameenda kwa nyumba ndogo yake katika ile kesi yake si walisema anatembea na mke wa mtu ? Huwezi jua jamani
 
Back
Top Bottom