Mgonjwa aidai TMJ, Hindu Mandal fidia ya shilingi milioni 500

Mgonjwa aidai TMJ, Hindu Mandal fidia ya shilingi milioni 500

Hiyo ni kesi au ni hukumu?! Wabongo vichwa vyetu ni hopeless kabisa.

Mahakama ndio itaamua kama kweli kuna kosa la kulipiwa fidia.

Kwa maoni yangu, mfungua kesi atashindwa vibaya sana. Kwanza sampuli za viungo hazisafirishwi kiholela kwenda nje ya nchi. Lazima upate vibali maalumu vya kufanya hivyo.

Kwahiyo Apollo watakuja kama mashahidi wake?! Hii kesi imefeli mapema sana.
 
Sasa kama una-ashiria sampuli za pili hazikuwa na tatizo baada ya kuwa ‘malignancy’ iliondolewa na procedure ya kwanza, ni kwanini basi walifanya procedure ya pili ya total ‘thyroidectomy’? Na baada ya kumtoa hiyo tezi, kwanini hawakumpa dawa za kubalance thyroid hormones kiasi akaanza kunyonyoka nywele na ngozi kusinyaa? On top of that wakadai tena ni kansa ndio inaleta hiyo hali, hivyo akapigwe mionzi?!!! What the f*uck??!!!
Thank you Mr Don.

Ukigundulika na papilarry thyroid carcinoma ( Thyroid cancer) ata upasuaji wa mwanzo ( partial surgery au lobectomy ) iliweza kuondoa ugonjwa wote bado inatakiwa kufanya procedure ya pili ( Total thyroidectomy). Hii procedure ya pili ni mihumu sana ili wakati wa kumfatilia mgonjwa baada ya tiba basi kuwa na uwezo wa kung'amua kama saratani inataka kurejea mapema kwa kutumia vipimo vya damu ( Serum thyroglobuln).

Sasa ukishafanya total thyroidectomy lazima utakuwa na upungufu wa homoni ya thyroxine na lazima upewe tiba ya homoni.Ukifanya partial surgery bado kunakuwa na tezi lilibakia ambalo inaendelea kutengeneza hiyo homoni na hakuna haja ya tiba ya homoni.

Nadhani kuna mkanganyiko na ukweli wa taarifa za mgonjwa na huenda ni kweli mgonjwa ana saratani ila bado hajakubalina na huo ukweli ( In denial stage) na hakuwa tayari kutibiwa.

Are we together??? 😳
 
Thank you Mr Don.

Ukigundulika na papilarry thyroid carcinoma ( Thyroid cancer) ata upasuaji wa mwanzo ( partial surgery au lobectomy ) iliweza kuondoa ugonjwa wote bado inatakiwa kufanya procedure ya pili ( Total thyroidectomy). Hii procedure ya pili ni mihumu sana ili wakati wa kumfatilia mgonjwa baada ya tiba basi kuwa na uwezo wa kung'amua kama saratani inataka kurejea mapema kwa kutumia vipimo vya damu ( Serum thyroglobuln).

Sasa ukishafanya total thyroidectomy lazima utakuwa na upungufu wa homoni ya thyroxine na lazima upewe tiba ya homoni.Ukifanya partial surgery bado kunakuwa na tezi lilibakia ambalo inaendelea kutengeneza hiyo homoni na hakuna haja ya tiba ya homoni.

Nadhani kuna mkanganyiko na ukweli wa taarifa za mgonjwa na huenda ni kweli mgonjwa ana saratani ila bado hajakubalina na huo ukweli ( In denial stage) na hakuwa tayari kutibiwa.

Are we together??? 😳
Sasa je, ni kwanini baada ya kuondoa hiyo tezi moja kwa moja, hawakumoa hizo dawa za homoni ya thyroxine? Badala yake wakamdanganyabkwamba kusinyaa kwa ngozi na kunyonyoka kwa nywele ni sababu ya cancer?
 
Kesi inayotaka kufanana na hiyo iliwahi kumtokea dada mmo hapo hapo Dae group alienda kusafishwa baada ya mimba kuharibika kufika nyumbani kesho yake tumbo limejaa kumbe walitoboa kizazi.
Jamani [emoji849][emoji15]
 
Dar es Salaam. Mfanyakazi wa Wizara ya Kilimo, Frorence Samwel anadai fidia ya Sh500 milioni Hospitali za TMJ na Hindu Mandal za jijini Dar es Salaam na daktari Moirice Mavura kwa kile anachodai kuwa ni uzembe katika kumtibu.

Pia amedai alipwe Sh53 milioni kwa ajili ya gharama mbalimbali, ikiwemo ya matibabu na usafiri.

Frorence amefungua kesi hiyo dhidi ya Dk Mavura pamoja na hospitali hizo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidai kuwa hospitali hizo zilifanya uzembe alipokwenda kupata huduma ya matibabu.

Akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhan Rugemalira huku akiongozwa na wakili wake Norbert Mlwale alidai kuwa Juni 27, 2018 alienda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na alifanyiwa uchunguzi wa koo ndipo alielezwa amuone Dk Moirice Mavura.

Alidai baada ya kumuona Dk Mavura alimwelekeza kuwa aende katika hospitali ya Hindu Mandal kwa kuwa ina vifaa vya kisasa kwa ajili ya upasuaji na anafanya kazi katika hospitali hiyo.

Shahidi huyo aliieleza mahakama hiyo kuwa Julai 9, 2018 Dk Mavura alimfanyia upasuaji katika koo lake na alitoa sampuli za tezi la kushoto zikapelekwa katika hospitali ya TMJ kwa ajili ya uchunguzi.

Alidai baada ya kufanyiwa uchunguzi wa sampuli hiyo hospitali ya TMJ ilitoa ripoti yake ikidai kuwa alikuwa na ugonjwa wa Rapillary Carcinoma of Thyoid ambayo alikabidhiwa Dk Mavura.

Baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo Dk Mavura alimfanyia upasuaji wa pili na kuiondoa tezi iliyoambukizwa ugonjwa huo.

Anaeleza kuwa baada ya kufanyiwa upasuaji huo zilichukuliwa sampuli za tezi zenye ugonjwa huo na zilipelekwa katika Hospitali ya TMJ kwa ajili ya uchunguzi mwingine ambapo ripoti ilionyesha kuwa tezi hizo zipo sawa hazina ugonjwa wowote. Mdai huyo alipopewa majibu hayo alienda nayo hadi katika hospitali ya Hindu Mandal na alipofika aliambiwa akamuone daktari aliyetajwa kwa jina moja la Mavunda ambaye alimweleza amekutwa na kansa ya Thyroid hivyo anatakiwa aende katika hospitali ya Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa ajili ya kuanza matibabu ya mionzi.

Anaeleza kuwa alipofika katika hospitali Ocean Road aliomba apimwe tena ili kujua kama ana tatizo hilo, ndipo walimwambia hawapimi upya kwa kuwa huwa wanategemea taarifa za mgonjwa kutoka hospitali husika.

“Nilipewa barua kutoka hospitali ya Hindu Mandal ili niende nayo hadi katika hospitali ya Ocean Road ili nianze matibabu ya mionzi,nilipofuatilia sikufanikiwa nikawa ninazunguushwa huku afya yangu ikiendelea kudhoofika huku ngozi yangu ikisinyaa kama mzee huku nywele zangu zikinyonyoka,” alidai Frorence.

Alidai baada ya kuikosa huduma ya mionzi alichukua uamuzi wa kukopa fedha benki na kuuza kiwanja chake huku ndugu zake wakimchangia fedha ili aweze kwenda hospitali ya Apollo iliyopo nchini India kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Baada ya kupata fedha hizo akaenda katika hospitali ya Hindu Mandal ili apewe barua pamoja na sampuli za tezi hizo aweze kwenda nazo katika hospitali ya Apollo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

“Nilipewa sampuli ambazo zilifungwa kama nilivyokabidhiwa, nilizipeleka moja kwa moja hadi katika hospitali ya Apollo iliyopo nchini India, zilifanyiwa uchunguzi na ilionekana sikuwa na kansa ya Thyoid,” alidai Frolence.

Anasema madaktari wa hospitali ya Apollo walibaini tezi yote ya Thyoid ya kushoto inayosaidia kutengeneza homoni imeondolewa wakati alipofanyiwa upasuaji huo katika hospitali ya Hindu Mandal, jambo ambalo limemsababishia ngozi yake kusinyaa na nywele kunyonyoka.

“Mimi nilikuwa najua nimefanyiwa upasuaji wa goita na sikuwahi kuambiwa na hospitali ya Hindu Mandal kama wamenitoa tezi, nimekuja kujua baada ya kuelezwa na hospitali ya Apollo ya nchini India kuwa kinachonisumbua ni upungufu wa homoni na siyo kansa.

Anadai hospitali ya Apollo ilimuandikia dawa za kuongeza homoni ambapo alielezwa katika maisha yake yote atakuwa anatumia dawa hizo, hatakiwi kuacha na asipofuata masharti hayo ngozi yake itasinyaa na nywele zitanyonyoka.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Rugemarila aliahirisha shauri hilo hadi Septemba 13,,2022 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mdai.

Source: Mwananchi, July 24

=========

NB:NDO MAANA VIONGOZI NA MATAJIRI HAWATAKI KUTIBIWA NCHINI PIA HIYO FIDIA NAONA NI NDOGO SANA MAANA TEZI YA THYROID INA UMUHIMU MKUBWA MNO KWA MWILI WA BINADAMU NI KAMA WAMEPUNGUZA SIKU ZAKE ZA KUISHI.
Huyo Mavura ni kimeo kabisa..Yaani yeye ishu ndogo tu anakimbiliaga operesheni. sijui analipwaga commision per procedure au!! alimfanyiaga operation ndugu yangu licha ya vpimo kutoonyesha tatizo. Just by guessing! mpaka waleo jamaa kapata permanent damage
 
Dr Mavura ni jina maarufu sana, sasa kwa nini hawakukutana na huyo mgonjwa nje ya mahakama wakaomba msamaha
huyu jamaa mm namfahamu, kukurefer opereshen hata kwa issue ndogo ni kitu cha kawaida, tena hospital anayopenda kufanya operesheni ni hindu mandal. Nadhan kuna commission anapataga per procedure. Hata kama kipimo kikowa negative ila ukawa na dalili zinashabihiana atakufanyi operesheni tu
 
Kuna shemeji yangu, Mamayake alilazwa pale Hindu....... wakasema wanamkata mguu maana kidonda chake kwenye ugoko hakitaweza kupona. Shemeji akampeleka Mama yake Narobi kidonda kikatibiwa mpaka kikapona
hindu mandal ni wasenge sana
 
Sio vizuri sana kuwashitaki madaktari
What the HL! Umeandika Nini hapa? Hakuna aliyeko juu ya Sheria! Hii ninsawa na kuuwa! Wenginea madaktarin wetu wa Tanzania Wana tabia ya kuamua bila kushirikisha madaktarin wenzao kuhakiki ugonjwa Fulani kama ndio.
Sasa hapa yeye mwenyewe atoe rufaa na aende mwenyewe kufanya upasuaji!
Ifike mahali waitwe kweli maDr's.
 
Ule upasuaji wa kuchukua sampuli ya awali, ungetumika pia kufanya assessment ya hizo thyroid glands (exploratory surgery) kuona kama zipo kwenye normal morphology au abnormal morphology, Je, zimevimba kijumla, au kuna uvimbe au vivimbe ambavyo vimejitokeza ambavyo vinaashiria kwamba majibu ya vipimo yanaendana na kile alichokiona wakati wa kuchukua sampuli. Vinginevyo kama kulikuwa na kiuvimbe angekiondoa na kuachana nazo huku akiendelea kufuatilia hali ya mgonjwa. Jambo jingine la kujiuliza, je, hakuna kipimo kingine labda cha damu kuweza ku confirm thyroid cancer ambacho angefanya kabla ya kwenda kwenye operation ya pili ya kuziondoa tezi zote?​
Yaani inasikitisha na kuumiza kichwa,yaani unanifanyia total thyrodectomy kweli,bila kuchukua tahadhari hata kusita husiti?Naanza kunyonyoka nywele unasema kansa,wakati ushaondoa thyroid glands zote ambazo zinamonitor ukuaji wangu,tena ni biology ya O-level huko,aisee
 
Sasa je, ni kwanini baada ya kuondoa hiyo tezi moja kwa moja, hawakumoa hizo dawa za homoni ya thyroxine? Badala yake wakamdanganyabkwamba kusinyaa kwa ngozi na kunyonyoka kwa nywele ni sababu ya cancer?
Kama nilivyoeleza awali mgonjwa inaoneka hakuwa tayari kuanza tiba kwa maana ata alivyopewa rufaa kuanza tiba ya mionzi baada ya kufika kule akata apimwe tene ili kuthibitisha ana mionzi.Hivyo hakukuwa na fursa ya kuanza tiba ya thyroxine nadhani mpaka alivyoenda India
 
Mkuu mmatumbi hata mkishitakiana hatushtuki na hatubadiliki. Maisha yetu mengi yako mikononi mwa Mungu. Ni Mungu peke yake anatulinda na nakuturehemu. Tunafanya mambo kwa uzembeuzembe na kubahatisha bahatisha tu hatuangalii fyuchaa. Hatujali. Ni vigumu sana sisi kubadilika kwasababu tabia zetu zinazididi tu kuwa mbaya afadhali ya jana.
Hapo ndipo na kumbuka Raisi wa Marekani wakati huo, Donald Trump his exllence, "wafrika ni manyani".
 
Hospital za bongo tabu sana.

Kuna siku nilienda hospital naumwa vibaya sana dalili zote za malaria ninazo DR akasema eti vipimo vinaonesha siumwi kitu.

Alinipiga kule maabara alikujaga timuliwa kwa vyeti feki.

Nikaona huu huu ufala Hali yangu inazidi kuwa mbaya.

Nikazama famasi nikachuka mseto nikameza nilipomaliza nikawa safi kabisa.

Hizi hospital wanaangalia pesa tu Wala sio matibabu sahihi
 
Hospital za bongo tabu sana.

Kuna siku nilienda hospital naumwa vibaya sana dalili zote za malaria ninazo DR akasema eti vipimo vinaonesha siumwi kitu.

Alinipiga kule maabara alikujaga timuliwa kwa vyeti feki.

Nikaona huu huu ufala Hali yangu inazidi kuwa mbaya.

Nikazama famasi nikachuka mseto nikameza nilipomaliza nikawa safi kabisa.

Hizi hospital wanaangalia pesa tu Wala sio matibabu sahihi
Soma tena ulichokiandika kaka.
 
Back
Top Bottom