Mgonjwa aidai TMJ, Hindu Mandal fidia ya shilingi milioni 500

Mgonjwa aidai TMJ, Hindu Mandal fidia ya shilingi milioni 500

Nilisha wahi kusema humu Madaktari wote wa Tz Masters na Degree holders ni sawa na Diploma Ulaya.
Marekani Ili usome MD utahenya sana

Kwanza huwezi soma MD bila kuwa na professional yeyote.

Yaani Ili ukasome MD lazima uwe tayari ni graduand wa shahada Fulani.

Hawachukua frehsers form school ambao akili hazijakomaa.
 
huyu jamaa mm namfahamu, kukurefer opereshen hata kwa issue ndogo ni kitu cha kawaida, tena hospital anayopenda kufanya operesheni ni hindu mandal. Nadhan kuna commission anapataga per procedure. Hata kama kipimo kikowa negative ila ukawa na dalili zinashabihiana atakufanyi operesheni tu
Hahahaha daah aisee yeye ni mwendo wa operesheni tu
 
Ipo haja ya kuwafungulia mashtaka mahakimu pia kwa kuchezea watu mda wao kwa kuweka watu mahabusi bila ushahidi kisha baada ya miaka wanawaachia.
Mkuu hakimu hawez nasa
Prosecutionary machine ndio tatizo
 
Yaani inasikitisha na kuumiza kichwa,yaani unanifanyia total thyrodectomy kweli,bila kuchukua tahadhari hata kusita husiti?Naanza kunyonyoka nywele unasema kansa,wakati ushaondoa thyroid glands zote ambazo zinamonitor ukuaji wangu,tena ni biology ya O-level huko,aisee
Hakuna daktari anayeacha mgonjwa kizembe hivyo; kumbukumbu zilizomo kwenye mafaili ya hospitali zitasema ukweli.
 
Kama nilivyoeleza awali mgonjwa inaoneka hakuwa tayari kuanza tiba kwa maana ata alivyopewa rufaa kuanza tiba ya mionzi baada ya kufika kule akata apimwe tene ili kuthibitisha ana mionzi.Hivyo hakukuwa na fursa ya kuanza tiba ya thyroxine nadhani mpaka alivyoenda India
Huyo ni mgonjwa mtata sana. Hata kesi hatashinda. Tena baada ya hapo ni kumfungulia kesi ya defamation tu.
 
Mkuu umeongea kweli nakumbuka gego langu la kushoto la chini mwisho , lilipata carriers sasa wakala kidogo ikafika hatua likawa sensitive na maji baridi nikaenda kwa hao so called specialists wa meno jamaa akakazia niling'oe na wakati nilienda kwa nia ya kuziba pekee jamaa akakaza na mimi nikamkazia kwamba sing'oi jino abadani .

Alipoona nimekaza akaamua tu kufanya ninachotaka na mpaka leo namshukuru mungu nipo sawa kabisa na ile sensitivity wala haipo .

Sasa mtu kama huyo unamweka kundi gani?
Gharama ya kung'oa Jino na kuziba ipi kubwa?
 
Niliwahi kupimwa nikakutwa na vidonda vya tumbo katika Hospital mbili tofauti, nikaanza dawa Kama Mwaka mzima Kila siku nakunywa Hadi nikaanza kukojoa mkojo wa rangi tofauti na unanuka madawa

Ndipo nikaenda Hospital nyingine kubwa zaidi ya private wakanipima wakaniambia Sina vidonda na niache kumeza dawa Mara moja,nilipoacha nikapona mpaka leo,
Labda ulikua ushapona kwa hizo dawa ulizotumia
 
Ndio kilichobaki, tukianza kushitakiana kidoogo umakini utakuwepo, hatukatai kukosea ndio uwanadamu lakini ni too much.

Wale kenge wa dar group sijui, walifanya uzembe kiasi dada yangu akatolewa kizazi kabisa, ndugu zangu nawaambIa tuwashughulikie, wanasema mradi katoka salama, tuache tu., mtu kakosa mtoto na kizazi wametoa😠
Pole mkuu. Yaani bongo watu wanakariri makatasi wanatapika baadaye ndio wanaitwa watalamu. Ungemkomalia kimyakimya ,ameharibu dada yako Hana kazi amekuwa debe tupu
 
Vyuo vyenu vya kata hvo mara unasikia IMTU, mara sijui KAIRUKI mara moshi college of health nao wanatoa MD..

Mtu una div3 unaenda kusoma MD..? Tegemea mambo kama haya
Kuwa na div 3 na kusoma MD sio tatizo, huyo Dr mvula ukimfatilia CV yake sio mtu wa divion 3, Yule dakatari aliepasua kichwa badala ya mguu sio wa division 3, faults katika medical Fields hazihusiani na nini ulipata secondary school.
Learn the situation first, wengi wetu tumetibiwa na clinical officer (watu waliofail form six) na wengine wakajiendeleza kuwa MDs na wakawa madaktari Bora.
 
Vyuo vimeruhusiwa na vimefuata vigezo. Alaumiwe aliyeenda kusoma na kuhitimu akaja kufanya yasiyo.

Taja chuo chochote, practice na kujiendeleza inabaki mikononi mwa mhusika na ndiye anakula kiapo.

Kuna mtaalamu alisoma very reputable universality huko Uingereza lakini bado alifukuzwa huko. Haya matatizo bado yapo hata huko mbele na si issue ya vyuo. Sijui kama unakumbuka issue ya CPR ya Michael Jackson??

Hajui analosema, amekariri na matokeo ya sekondari, faults katika medical Fields hazikuanza Leo, ni tangu kipindi cha hypocrites (father of medicine)
 
It is confusing

It looks like this patient is on thyroxine replacement therapy following total thyroidectomy.It is not possible to have hypothyroidism following partial tryroidectomy.

It looks like the initial surgery was lobectomy (partial thyroiedectomy) where all the malignant tumor was removed and the second surgery was total thyroidectomy. It is unlikely to find malignant cells in the sample after second surgery if the initial surgery removed all the malignant tumor.

Question : Did he the take samples from first and secondary surgrery to India?
Or it could be a true cut biopsy, but In lay man language every inversive investment ni operesheni.

Swali ni je, aliandikiwa hiyo thyroxine? Au mgonjwa mwenyewe Ali ignore ? Au haikuwepo? Coz from the scenario alipoenda India alipewa tu thyroxine .
 
Hili la dr ku-google siyo ukilaza wala jambo geni. Nimeliona mpaka majuu. Anakuwa anatafuta kutaka kujua zaidi na siyo kwamba anategemea google kumtibu mgonjwa. Tusiwe kama watu wasio na shule ukimwambia kuwa umesomea computer anategema ujue kila kitu kwenye computer kichwani mwako. Halfu kuna nchi nyingine matibabu yanaaongozwa na protocal fulani walizojiwekea na ziko kwenye database ambayo dr yoyote anaweza kui-access kwa mwongozo zaidi wakati anatibu. Hata ma-pilot wanatembea na reference zinazoelezea hatua za kutatua changamoto fulani na hawatakiwi wazikariri zote.
Bongo wanataka hata ubongo wako uwe encyclopedia kisa ni daktari, tena ukiona doctor anagoogle shukuru Mungu asije akakuingiza chaka Kama hajagoogle.
 
Uhakika ni upi. ? Kwa nini aamini katika Majibu ya Appolo na si Tanzania,,?
Kwa nini amshitaki Daktari aliyemfanyia upasuaji na si aliyetoa majibu ya kwanza.
Je ikiwa majibu ya kwanza yalikua saratani tiba yake ni ipi?
Je saratani ilikua katika tezi lote au sehemu ya tezi?
Je anajua kuwa thyroid ni tezi?
Je alijaza karatasi ya kufanyiwa upasuaji au la?
Je anadhani mill 500 inatosha kwa ajili ya fidia?
Je anajua sababu nyingine za kuharibika ngozi na kutoka nywele zinaweza kuwa zaidi ya tezi alilolitoa?
Hayo sio maswali ya wewe kujiuliza hayo ni maswala ya mahakama...mkuu..
 
Dar es Salaam. Mfanyakazi wa Wizara ya Kilimo, Frorence Samwel anadai fidia ya Sh500 milioni Hospitali za TMJ na Hindu Mandal za jijini Dar es Salaam na daktari Moirice Mavura kwa kile anachodai kuwa ni uzembe katika kumtibu.

Pia amedai alipwe Sh53 milioni kwa ajili ya gharama mbalimbali, ikiwemo ya matibabu na usafiri.

Frorence amefungua kesi hiyo dhidi ya Dk Mavura pamoja na hospitali hizo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidai kuwa hospitali hizo zilifanya uzembe alipokwenda kupata huduma ya matibabu.

Akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhan Rugemalira huku akiongozwa na wakili wake Norbert Mlwale alidai kuwa Juni 27, 2018 alienda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na alifanyiwa uchunguzi wa koo ndipo alielezwa amuone Dk Moirice Mavura.

Alidai baada ya kumuona Dk Mavura alimwelekeza kuwa aende katika hospitali ya Hindu Mandal kwa kuwa ina vifaa vya kisasa kwa ajili ya upasuaji na anafanya kazi katika hospitali hiyo.

Shahidi huyo aliieleza mahakama hiyo kuwa Julai 9, 2018 Dk Mavura alimfanyia upasuaji katika koo lake na alitoa sampuli za tezi la kushoto zikapelekwa katika hospitali ya TMJ kwa ajili ya uchunguzi.

Alidai baada ya kufanyiwa uchunguzi wa sampuli hiyo hospitali ya TMJ ilitoa ripoti yake ikidai kuwa alikuwa na ugonjwa wa Rapillary Carcinoma of Thyoid ambayo alikabidhiwa Dk Mavura.

Baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo Dk Mavura alimfanyia upasuaji wa pili na kuiondoa tezi iliyoambukizwa ugonjwa huo.

Anaeleza kuwa baada ya kufanyiwa upasuaji huo zilichukuliwa sampuli za tezi zenye ugonjwa huo na zilipelekwa katika Hospitali ya TMJ kwa ajili ya uchunguzi mwingine ambapo ripoti ilionyesha kuwa tezi hizo zipo sawa hazina ugonjwa wowote. Mdai huyo alipopewa majibu hayo alienda nayo hadi katika hospitali ya Hindu Mandal na alipofika aliambiwa akamuone daktari aliyetajwa kwa jina moja la Mavunda ambaye alimweleza amekutwa na kansa ya Thyroid hivyo anatakiwa aende katika hospitali ya Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa ajili ya kuanza matibabu ya mionzi.

Anaeleza kuwa alipofika katika hospitali Ocean Road aliomba apimwe tena ili kujua kama ana tatizo hilo, ndipo walimwambia hawapimi upya kwa kuwa huwa wanategemea taarifa za mgonjwa kutoka hospitali husika.

“Nilipewa barua kutoka hospitali ya Hindu Mandal ili niende nayo hadi katika hospitali ya Ocean Road ili nianze matibabu ya mionzi,nilipofuatilia sikufanikiwa nikawa ninazunguushwa huku afya yangu ikiendelea kudhoofika huku ngozi yangu ikisinyaa kama mzee huku nywele zangu zikinyonyoka,” alidai Frorence.

Alidai baada ya kuikosa huduma ya mionzi alichukua uamuzi wa kukopa fedha benki na kuuza kiwanja chake huku ndugu zake wakimchangia fedha ili aweze kwenda hospitali ya Apollo iliyopo nchini India kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Baada ya kupata fedha hizo akaenda katika hospitali ya Hindu Mandal ili apewe barua pamoja na sampuli za tezi hizo aweze kwenda nazo katika hospitali ya Apollo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

“Nilipewa sampuli ambazo zilifungwa kama nilivyokabidhiwa, nilizipeleka moja kwa moja hadi katika hospitali ya Apollo iliyopo nchini India, zilifanyiwa uchunguzi na ilionekana sikuwa na kansa ya Thyoid,” alidai Frolence.

Anasema madaktari wa hospitali ya Apollo walibaini tezi yote ya Thyoid ya kushoto inayosaidia kutengeneza homoni imeondolewa wakati alipofanyiwa upasuaji huo katika hospitali ya Hindu Mandal, jambo ambalo limemsababishia ngozi yake kusinyaa na nywele kunyonyoka.

“Mimi nilikuwa najua nimefanyiwa upasuaji wa goita na sikuwahi kuambiwa na hospitali ya Hindu Mandal kama wamenitoa tezi, nimekuja kujua baada ya kuelezwa na hospitali ya Apollo ya nchini India kuwa kinachonisumbua ni upungufu wa homoni na siyo kansa.

Anadai hospitali ya Apollo ilimuandikia dawa za kuongeza homoni ambapo alielezwa katika maisha yake yote atakuwa anatumia dawa hizo, hatakiwi kuacha na asipofuata masharti hayo ngozi yake itasinyaa na nywele zitanyonyoka.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Rugemarila aliahirisha shauri hilo hadi Septemba 13,,2022 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mdai.

Source: Mwananchi, July 24

=========

NB:NDO MAANA VIONGOZI NA MATAJIRI HAWATAKI KUTIBIWA NCHINI PIA HIYO FIDIA NAONA NI NDOGO SANA MAANA TEZI YA THYROID INA UMUHIMU MKUBWA MNO KWA MWILI WA BINADAMU NI KAMA WAMEPUNGUZA SIKU ZAKE ZA KUISHI.
Yapo mambo nisiri kubwa sana ya mateso mwanadam anayapata. Ila ktk hali ya kawaida Mungu hapendi watu wake tuteseke au kUkutana na yale yana tukuta. Siri ni nzinto na mm wwcha nikae kimya
 
Huyu Dr Mavura si ni mfanyakazi wa Muhimbili Sasa ilikuwaje akapewa rufaa aende kwingine? Ina maana Muhimbili haikuwa na uwezo wa ku deal na matibabu ya huyu mgonjwa mpaka wampeleke private?
 
Back
Top Bottom