Mgonjwa aidai TMJ, Hindu Mandal fidia ya shilingi milioni 500

Mgonjwa aidai TMJ, Hindu Mandal fidia ya shilingi milioni 500

Ile nyie madaktari hatari sanaa...
Kuna mmoja aliniambiaga Nina bacteria wa vidonda tumbo ndio maana tumbo linauma sanaa.

Akanipa dawa, kufika nyumba nikawazaaa nikaona ninywe dawa ya asili ya tumbo la typhoid.

Aisee nilikunywa siku 3 nikapona.

Mpaka leo dawa za Dokta mwenzako ninazo na kila kitu nakula na sijawahi pata maumivu tumboni Wala pilau, pilipili na vyengine kuzingua.

#YNWA
Sasa hata mdudu wa typhoid ni bacteria pia .. S.Typhii. Vile vile wa vidonda vya tumbo ni bacteria pia ila aina ya H. Pylori..

Na huenda hiyo dawa ya asili ina ingredients za antibiotics..

Kwa hiyo hata ungekunywa ya dokta ungepona pia.

Tatizo mmekariri kuwa madaktari wanasoma dawa na. Magonjwa kama matching items..

Kwamba Septrin ni dawa ya tumbo... Na dokta akikuandikia ukiwa unaumwa homa ya mapafu.. Unaona kakosea.
 
We unasema hayajakukuta, juzi kati kuna mtoto wa dada yangu, mkewe alifanyiwa upasuajo, kumbe walitoboa utumbo, wakashona mtu vinyesi vinavujia ndani tu, kuja kumkimbiza hospital, dk chache kavuta.

Hii ni kama vile tunaposema usipige mwizi, halafu kuna mtu anatokea na kukwambia bado hujaibiwa wewe😂
Madaktari tusiwashitaki kaka.
 
We ni mpuuzi kweli. Daktari ana immunity gani asishitakiwe?

Yaani afanye uzembe kwenye maisha ya watu, tumwachie Mungu?

Watanzania sample yenu hii, ndio inatufanya tuonekane wajinga & primitive.
Nikuache tu kwa leo inaonekana uke wenza unakutesa ila usirudie.
FB_IMG_1653776094092.jpg
 
Uko kwa wenzetu wangekua na mawazo kama haya yakwako kamwe wasingefikia level walizozifika kwenye sekta zote wanazozifanya.
Wenzetu kina nani?
Backgrounds ya madaktari wao ikoje? Na ya hawa wa kwetu ikoje?

Sheria zetu zinasemaje? Je wao pia wana shida ya madaktari? Wana shida ya vifaa tiba? Wana upungufu wa hospital?
 
Sasa kama ametoka familia ya shida au amesoma kwa shida ndio asiwajibike kwa makosa ya uzembe wake?
Walimu huwa wanakosea sana na ni wengi mnoo mitaani huwa mnawawajibishaje?

akisusa mwalimu mmoja tunao elfu 1 mtaani je akisusa daktari?
 
Million 500 chache sana, maana wamemsababishia kilema cha maisha
 
Sasa waendelee tu kufanya kazi kwa mazoea
Alaf baada ya kufanya kosa mtu ametulia tu akiangalia mtu anadhoofika
Kwani ni makosa ya mara kwa mara? Na tiba ya kinachomsumbua mgonjwa wapi imeandikwa kuwa akipewa ni lazima iwe sahihi?

Unaweza kuumwa kichwa wakakupima ukapewa painkillers na zikakudhuru na ulifata maelezo ya physician ipasavyo utaenda kushitaki ushinde?
 
Kushatakiwa ni lazima maana kampa mtu ukilema kwa uzembe wake sasa alisomea nini ? Kama hata kumpima mtu tu ni shida? Alipe pesa na hospitali iliyomwajiri ilipishwe full stop maana hana sifa ya udaktari kama anampa mtu ukilema wa bure tu.

Kila kiungo cha binadamu kina kazi maalum sasa kwenda kuondoa kitu kizima aisee .
Ukienda hospital una uvimbe wa koo na madaktari baada ya kukufanyia uchunguzi wakagundua ni thyroid cancer wakaamua kukufanyia tiba baadae ukaenda Nairobi wakagundua ni uvimbe wa kawaida utarudi kuwashitaki ushinde?

Na wakati mwingine ukiumwa nani atakutibu?
 
Unaleta huruma kwenye roho ya mtu? Alisoma kwa shida so what? Amemaliza masomo salama why asiwe makini na kazi zake?
Imeandikwa wapi ni lazima awe sahihi kwa kila tiba anayoitoa?
 
Anhaa miungu yako ? Maana mimi Mungu wangu mmoja tu hana sifa yeyote ya kiumbe chochote halali, hali, hajazaa wala hakuzaliwa , hamtegemei yeyote katika alivyoviumba bali sisi viumbe ndiyo tunamtegemea yeye, alikuwepo na atakuwepo daima.
Pumba mfate mwamposa akakutibie sasa
 
Kesi kama hizi zinatakiwa kua nyingi sana..umasikini wa mtu au kusoma kwa shida hauna uhusiano wowote ule katika kutoa professional advice na kutekeleza majukumu hayo, ukitoa ushauri wa kitaalamu kimakosa unatakiwa uwajibike..miezi kadhaa nyuma humu ndani kuna jamaa alipoteza mtoto wake kwa uzembe wa hospitali kwaio kesi zikikomaa zikawa nyingi mtu atajikita katika kufanya tafiti kuliko kuanza kubahatisha...
Ni tafiti gani iko sahihi kwa 100%
Kila tiba na dawa zina side effects umepata tiba kimakosa unaruhusiwa kumuwajibisha Daktari ni sawa ila kiungwana tu tusiwashitaki.

Hatutoshinda
 
Fidia alitakiwa Adai 5 billion. Tezi ya thyroid ni kuhimili mkuu kwenye mwili wa binadamu. Madaktari hivyo na Hospital ya Hindumsndal ni hivyo mno. Serikali imulikeni. Nilitibiwa pale na nilipoona wataniharakisha siku za kuishi nikaachana nao. Napambana kivingine.
 
Dar es Salaam. Mfanyakazi wa Wizara ya Kilimo, Frorence Samwel anadai fidia ya Sh500 milioni Hospitali za TMJ na Hindu Mandal za jijini Dar es Salaam na daktari Moirice Mavura kwa kile anachodai kuwa ni uzembe katika kumtibu.

Pia amedai alipwe Sh53 milioni kwa ajili ya gharama mbalimbali, ikiwemo ya matibabu na usafiri.

Frorence amefungua kesi hiyo dhidi ya Dk Mavura pamoja na hospitali hizo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidai kuwa hospitali hizo zilifanya uzembe alipokwenda kupata huduma ya matibabu.

Akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhan Rugemalira huku akiongozwa na wakili wake Norbert Mlwale alidai kuwa Juni 27, 2018 alienda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na alifanyiwa uchunguzi wa koo ndipo alielezwa amuone Dk Moirice Mavura.

Alidai baada ya kumuona Dk Mavura alimwelekeza kuwa aende katika hospitali ya Hindu Mandal kwa kuwa ina vifaa vya kisasa kwa ajili ya upasuaji na anafanya kazi katika hospitali hiyo.

Shahidi huyo aliieleza mahakama hiyo kuwa Julai 9, 2018 Dk Mavura alimfanyia upasuaji katika koo lake na alitoa sampuli za tezi la kushoto zikapelekwa katika hospitali ya TMJ kwa ajili ya uchunguzi.

Alidai baada ya kufanyiwa uchunguzi wa sampuli hiyo hospitali ya TMJ ilitoa ripoti yake ikidai kuwa alikuwa na ugonjwa wa Rapillary Carcinoma of Thyoid ambayo alikabidhiwa Dk Mavura.

Baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo Dk Mavura alimfanyia upasuaji wa pili na kuiondoa tezi iliyoambukizwa ugonjwa huo.

Anaeleza kuwa baada ya kufanyiwa upasuaji huo zilichukuliwa sampuli za tezi zenye ugonjwa huo na zilipelekwa katika Hospitali ya TMJ kwa ajili ya uchunguzi mwingine ambapo ripoti ilionyesha kuwa tezi hizo zipo sawa hazina ugonjwa wowote. Mdai huyo alipopewa majibu hayo alienda nayo hadi katika hospitali ya Hindu Mandal na alipofika aliambiwa akamuone daktari aliyetajwa kwa jina moja la Mavunda ambaye alimweleza amekutwa na kansa ya Thyroid hivyo anatakiwa aende katika hospitali ya Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa ajili ya kuanza matibabu ya mionzi.

Anaeleza kuwa alipofika katika hospitali Ocean Road aliomba apimwe tena ili kujua kama ana tatizo hilo, ndipo walimwambia hawapimi upya kwa kuwa huwa wanategemea taarifa za mgonjwa kutoka hospitali husika.

“Nilipewa barua kutoka hospitali ya Hindu Mandal ili niende nayo hadi katika hospitali ya Ocean Road ili nianze matibabu ya mionzi,nilipofuatilia sikufanikiwa nikawa ninazunguushwa huku afya yangu ikiendelea kudhoofika huku ngozi yangu ikisinyaa kama mzee huku nywele zangu zikinyonyoka,” alidai Frorence.

Alidai baada ya kuikosa huduma ya mionzi alichukua uamuzi wa kukopa fedha benki na kuuza kiwanja chake huku ndugu zake wakimchangia fedha ili aweze kwenda hospitali ya Apollo iliyopo nchini India kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Baada ya kupata fedha hizo akaenda katika hospitali ya Hindu Mandal ili apewe barua pamoja na sampuli za tezi hizo aweze kwenda nazo katika hospitali ya Apollo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

“Nilipewa sampuli ambazo zilifungwa kama nilivyokabidhiwa, nilizipeleka moja kwa moja hadi katika hospitali ya Apollo iliyopo nchini India, zilifanyiwa uchunguzi na ilionekana sikuwa na kansa ya Thyoid,” alidai Frolence.

Anasema madaktari wa hospitali ya Apollo walibaini tezi yote ya Thyoid ya kushoto inayosaidia kutengeneza homoni imeondolewa wakati alipofanyiwa upasuaji huo katika hospitali ya Hindu Mandal, jambo ambalo limemsababishia ngozi yake kusinyaa na nywele kunyonyoka.

“Mimi nilikuwa najua nimefanyiwa upasuaji wa goita na sikuwahi kuambiwa na hospitali ya Hindu Mandal kama wamenitoa tezi, nimekuja kujua baada ya kuelezwa na hospitali ya Apollo ya nchini India kuwa kinachonisumbua ni upungufu wa homoni na siyo kansa.

Anadai hospitali ya Apollo ilimuandikia dawa za kuongeza homoni ambapo alielezwa katika maisha yake yote atakuwa anatumia dawa hizo, hatakiwi kuacha na asipofuata masharti hayo ngozi yake itasinyaa na nywele zitanyonyoka.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Rugemarila aliahirisha shauri hilo hadi Septemba 13,,2022 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mdai.

Source: Mwananchi, July 24

=========

NB:NDO MAANA VIONGOZI NA MATAJIRI HAWATAKI KUTIBIWA NCHINI PIA HIYO FIDIA NAONA NI NDOGO SANA MAANA TEZI YA THYROID INA UMUHIMU MKUBWA MNO KWA MWILI WA BINADAMU NI KAMA WAMEPUNGUZA SIKU ZAKE ZA KUISHI
Mbona amedai hela kidogo namna hiyo ,Ningekuwa mimi ningeanza na bilioni .
 
Mkuu endelea kumtazama Mama yako usije ukawa kama mimi nilisema hivyo hivyo baadae akaja kupata stroke kwa ubishi wangu. Dr alinambia japo ni mara ya kwanza lakini presha yake ni kubwa mno na inaonekana ilikuwepo muda mrefu. Nikasema aah wapi. Leo mama hatembei hawezi chochote. Be careful acha kiburi cha uzima.
Wewe alivyorudi akakutana na Dr mwengine alishangaa kwanini ameanzishiwa dozi wakati ndio mara ya kwanza tuu ameumwa kuna dawa za pressure hazina madhara makubwa
 
Ebu acheni Roho za chuki na makasiriko hakuna Daktari anayetoka nyumbani anasema anaenda kuua au kumdhuru mteja wake hii ni bahati mbaya na inatokea hata huko ulaya mnapo pasifia Kuna mistakes nyingi kama hizi pamoja na wao kuwa na technology ya juu sana, just Google medical legal cases uone,huyo Dr Mavura ametoa sampuli ya ugonjwa amepeleka kupimwa majibu yamerudi ni Capillary Carcinoma ambayo tiba yake ni kuwahi kutoa uvimbe wote sasa yeye kosa lake lipo wapi?
Nakuona mganga mkuu mpiga ramli umekuja tetea
 
Back
Top Bottom