Mgonjwa kulipia 'Kumuona Daktari' Hospitali si sahihi

Mgonjwa kulipia 'Kumuona Daktari' Hospitali si sahihi

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Naona kama Serikali imechelewa sana kufuta hii gharama inayozidi kumuongezea machungu mgonjwa pindi anapoamua kwenda kutafuta tiba hospitali.

Ni kijambo kidogo lakini huwezi jua pengine kimewahi hata kusababisha vifo.

Gharama anazolipa mgonjwa ili kumuona daktari kabla hata ya matibabu ni kaandamizi kwa wagonjwa na utaratibu huo ni maumivu hasa kwa wale wagonjwa wenye hali duni kimaisha

Huenda ilishatokea mtu aliumwa sana na akatamani aende hospitali lakini akajikuta hata pesa ya kumuona daktari hana, pengine ikapelekea akasusa hata baadae maradhi yakamzidi na akafariki kwa kuchelewa kupata matibabu!

Nimewaza sana na kujiuliza kuna uhalali gani wa malipo haya? Si hospitali ya serikali si private, yaani hata daktari hajasema chochote anaku chaji pesa ambayo imeshapangwa wewe na yeyote yule atakayeingia chumba hicho atoe kwanza kabla ya gharama zingine za matibabu.

Tuombe serikali iondoe gharama hizi kutupunguzia mzigo wa maisha angalau tuwe tunalipia vipimo na dawa tu.
 
Umeleta jambo jema sana.

Na sio kwa government hospital tu hii inapaswa kuondoka hata kwa hizo private hospital.

Kuna hospitali zinachaji hadi 40,000/= kumuona daktati tu.

Huu ni wizi kabisa, unalipia hela hiyo na unalipia vipimo na baadae unaambiwa hakuna tatizo au una malaria na matibabu yake ni mseto ya shilingi 3,000/=

Serikali angalieni hili au tutaamini wahusika wanakata posho?
 
Kila mkoa lazima kuwe na hospitali ya bure, atleast kumwona dokta tuu
 
Tafsiri yake kila mtu anapaswa achunge Afya yake Kwa umakini ili Kupunguza gharama Kama hizo.

Pili, Gharama ya kumuona Daktari haipaswi kuondolewa Ila inatakiwa kuwa Affordable kulingana na Hali za Watu husika.
Hospital ziwekwe kulingana na hadhi za watu.

Kumuona Daktari lazima ulipie ili ujue umuhimu wa kutunza Afya yako mwenyewe.

Kama unaona gharama kumuona Daktari basi yakupasa uzingatie sana mambo ya Afya ili kuepuka Gharama.

Magonjwa mengi yanatokana na uzembe, na siku zote uzembe ni gharama.
 
Mkuu kumuona mganga wa kienyeji tu unalipia sembuse mtu alie ingia na kusota darasani miaka 6 au zaidi ? Itabidi hata tukiwapigia simu tulipie maana tunawasumbua mno .
Kwahiyo umewaweka kundi la waganga wa kienyeji, lkn ndio wasomi wetu na wanaona umewatendea haki.
Lkn ni ukweli kuwa hii gharama unachangia vifo. Kwanini kumuona iwe hela na hapo mgonjwa amezidiwa? Hii gharama ITOLEWE KABISA

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom