Naona kama serikali imechelewa sana kufuta hii gharama inayozidi kumuongezea machungu mgonjwa pindi anapoamua kwenda kutafuta tiba hospitali.
Ni kijambo kidogo lakini huwezi jua pengine kimewahi hata kusababisha vifo.
Huenda ilishatokea mtu aliumwa sana na akatamani aende hospitali lakini akajikuta hata pesa ya kumuona daktari hana, pengine ikapelekea akasusa hata baadae maradhi yakamzidi na akafariki kwa kuchelewa kupata matibabu!
Nimewaza sana na kujiuliza kuna uhalali gani wa malipo haya? Si hospitali ya serikali si private, yaani hata daktari hajasema chochote anaku chaji pesa ambayo imeshapangwa wewe na yeyote yule atakayeingia chumba hicho atoe kwanza kabla ya gharama zingine za matibabu.
Tuombe serikali iondoe gharama hizi kutupunguzia mzigo wa maisha angalau tuwe tunalipia vipimo na dawa tu.