Mleta mada una tafsiri potofu kuhusu gharama ya kumuona Daktari. Kiuhalisia ile sio gharama ya kumuona Daktari bali ni gharama ya kutibiwa na Daktari. Kuonana na Daktari kwa lengo la kutibiwa ndio msingi wa huduma zote za matibabu kwa mgonjwa, na pesa unayolipa ndio inalipia muda wake, juhudi zake na akili yake itakayo tumika kutambua ugonjwa wako na kupangilia matibabu ya ugonjwa wako na wagonjwa wengine. Gharama hizo hutofautiana baina ya hospitali na hospitali au Daktari na Daktari. Kwa hospitali za umma (serikali) ile pesa inaingia kwenye mapato ya serikali na kwa hospitali za binafsi ile pesa inaingia kwenye hospitali husika, Daktari yeye hulipwa na taasisi husika kwa mapatano binafsi.