Umeandika usichokijua.
Fikra za kijamaa (huduma za kijamii ni bure!) huenda ndio zimekufanya kufikiri hivyo.
Consultation fee ipo katika professional zote dunia nzima wakati wa kutoa huduma. Haijarishi ni Daktari, Mpishi, Lawyer, Accountant, Pastor, Fundi nk kote huko utakutana na Consultation fee. Issue ni namna tu watakavyomlipisha mtu ndio inaweza kutofautiana, wapo wanaokulipisha directly na wengine indirectly, ama individual vs group. Mtu anapolipa Consultation fee maana yake analipia muda, akili na maarifa ya mtaalamu anayemhudumia.
Unapolipa pesa ili kumuona Daktari, kimantiki ni kwamba imeilipa hospitali husika itenge muda, nguvu kazi, akili na maarifa ya kuanzisha/kuendeleza mchakato wa kuhudumia afya yako, na kihospitali hilo jukumu kimsingi huwa ni la Daktari. Na hospitali huweka flat rate ya consultation fee kwa wagonjwa wote ili kufidia, maana wapo wagonjwa wenye kuhitaji muda mwingi, akili kubwa, maarifa mapana na nguvu kazi na pia wapo wenye kuhitaji mambo hayo kwa uchache.
Yote kwa yote unapaswa ufahamu tu, ile consultation fee ni pesa ya hospitali husika, ndio hiyo hiyo hutumika kulipa wafanyakazi mishahara, Posho, kulipa kodi, umeme, maji, ulinzi na kununua vifaa.