Mgonjwa kulipia 'Kumuona Daktari' Hospitali si sahihi

Mgonjwa kulipia 'Kumuona Daktari' Hospitali si sahihi

Basi kila sehemu ingekua hivyo tungefika? Mfano ukitaka kusafiri kwenda Morogoro ukiingia tu kwenye abood bus utoe pesa ya kumuona dereva wa basi then ulipie na nauli yako kwa konda
Ni dhuluma ya wazi kabisa , hata ukisahau documents kwenye chumba cha daktari kesho yake ukataka kurudi kuchukua huwezi kuruhusiwa kuingia lazima ulipe hela ya kumuona daktari.
 
Hapo issue siyo kumuona Daktari.

Unacholipia Ni consultation fee.

Yaani kupima vital signs ( pressure, air tract, Breathing rate na kumwelezea Daktari unavyojisikia, halafu akakupa USHAURI na matibabu yake kwa kukuandikia.

Akishakuandikia hiyo 'Kumuona Daktari inaishia hapo"
Inaitwa "consultation fees" na sio kumuona daktari.......
 
Naona kama serikali imechelewa sana kufuta hii gharama inayozidi kumuongezea machungu mgonjwa pindi anapoamua kwenda kutafuta tiba hospitali

Ni kijambo kidogo lakini huwezi jua pengine kimewahi hata kusababisha vifo
Huenda ilishatokea mtu aliumwa sana na akatamani aende hospitali lakini akajikuta hata pesa ya kumuona daktari hana..pengine ikapelekea akasusa hata baadae maradhi yakamzidi na akafariki kwa kuchelewa kupata matibabu!

Nimewaza sana na kujiuliza kuna uhalali gani wa malipo haya? Si hospitali ya serikali si private...yaani hata daktari hajasema chochote anaku chaji pesa ambayo imeshapangwa wewe na yeyote yule atakayeingia chumba hicho atoe kwanza kabla ya gharama zingine za matibabu.

Tuombe serikali iondoe gharama hizi kutupunguzia mzigo wa maisha angalau tuwe tunalipia vipimo na dawa tu.
Naunga mkono ziondolewe si halali kumuona tu mtu hela.
 
Kwahiyo umewaweka kundi la waganga wa kienyeji, lkn ndio wasomi wetu na wanaona umewatendea haki.
Lkn ni ukweli kuwa hii gharama unachangia vifo. Kwanini kumuona iwe hela na hapo mgonjwa amezidiwa? Hii gharama ITOLEWE KABISA

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
Mgonjwa aliezidiwa kuna 'fast track' au 'emergency' anahudumiwa kwanza malipo yanafuata.

Unachokiwaza leo mamlaka husika wanakifahamu kwa kina, na wanayo picha kubwa kuliko kuangalia upande mmoja tu wa maslahi yako binafsi.
 
Mkuu kumuona mganga wa kienyeji tu unalipia sembuse mtu alie ingia na kusota darasani miaka 6 au zaidi ? Itabidi hata tukiwapigia simu tulipie maana tunawasumbua mno .
Umeandika upumbavu. Ni bora ungeshauri wananchi wachukue bima.
 
Naona kama serikali imechelewa sana kufuta hii gharama inayozidi kumuongezea machungu mgonjwa pindi anapoamua kwenda kutafuta tiba hospitali.

Ni kijambo kidogo lakini huwezi jua pengine kimewahi hata kusababisha vifo.

Huenda ilishatokea mtu aliumwa sana na akatamani aende hospitali lakini akajikuta hata pesa ya kumuona daktari hana, pengine ikapelekea akasusa hata baadae maradhi yakamzidi na akafariki kwa kuchelewa kupata matibabu!

Nimewaza sana na kujiuliza kuna uhalali gani wa malipo haya? Si hospitali ya serikali si private, yaani hata daktari hajasema chochote anaku chaji pesa ambayo imeshapangwa wewe na yeyote yule atakayeingia chumba hicho atoe kwanza kabla ya gharama zingine za matibabu.

Tuombe serikali iondoe gharama hizi kutupunguzia mzigo wa maisha angalau tuwe tunalipia vipimo na dawa tu.
Mkuu unataka ukapate ushauri wa kitabibu bure wakati wenzio wanesota darasani.
Mfano unaenda kwa daktari anakufanyia consultation hakafu unaondoka kwenda kununua dawa kwenye maduka ya dawa, hasara itakuwa kwa nani. Kwa wenzetu walioendelea consultation fee inachajiwa kwa muda daktari anaotumia kukuhudumia.
 
Kumuona daktari. Humuangalii kama picha. Ile kumueleza tu shida yako naye akasuggest vipimo au dawa ndicho unacholipia. Kama unaona haina maana kumueleza mtaalamu shida zako jiandikie mwenyewe dawa au vipimo.
 
Madaktari wamefunzwa kutengeneza pesa mahospitalini, na siku zote madaktari hujiona wao ni special sana ukiuliza oh! sijui wamesoma kwa tabu na miaka mingi. Na ubaya watu huwa na mitazamo ya kudhani madaktari wanajua kila kitu.
 
Back
Top Bottom