Mgonjwa kulipia 'Kumuona Daktari' Hospitali si sahihi

Basi kila sehemu ingekua hivyo tungefika? Mfano ukitaka kusafiri kwenda Morogoro ukiingia tu kwenye abood bus utoe pesa ya kumuona dereva wa basi then ulipie na nauli yako kwa konda
Ni dhuluma ya wazi kabisa , hata ukisahau documents kwenye chumba cha daktari kesho yake ukataka kurudi kuchukua huwezi kuruhusiwa kuingia lazima ulipe hela ya kumuona daktari.
 
Hapo issue siyo kumuona Daktari.

Unacholipia Ni consultation fee.

Yaani kupima vital signs ( pressure, air tract, Breathing rate na kumwelezea Daktari unavyojisikia, halafu akakupa USHAURI na matibabu yake kwa kukuandikia.

Akishakuandikia hiyo 'Kumuona Daktari inaishia hapo"
Inaitwa "consultation fees" na sio kumuona daktari.......
 
Naunga mkono ziondolewe si halali kumuona tu mtu hela.
 
Mgonjwa aliezidiwa kuna 'fast track' au 'emergency' anahudumiwa kwanza malipo yanafuata.

Unachokiwaza leo mamlaka husika wanakifahamu kwa kina, na wanayo picha kubwa kuliko kuangalia upande mmoja tu wa maslahi yako binafsi.
 
Mkuu kumuona mganga wa kienyeji tu unalipia sembuse mtu alie ingia na kusota darasani miaka 6 au zaidi ? Itabidi hata tukiwapigia simu tulipie maana tunawasumbua mno .
Umeandika upumbavu. Ni bora ungeshauri wananchi wachukue bima.
 
Mkuu unataka ukapate ushauri wa kitabibu bure wakati wenzio wanesota darasani.
Mfano unaenda kwa daktari anakufanyia consultation hakafu unaondoka kwenda kununua dawa kwenye maduka ya dawa, hasara itakuwa kwa nani. Kwa wenzetu walioendelea consultation fee inachajiwa kwa muda daktari anaotumia kukuhudumia.
 
Kumuona daktari. Humuangalii kama picha. Ile kumueleza tu shida yako naye akasuggest vipimo au dawa ndicho unacholipia. Kama unaona haina maana kumueleza mtaalamu shida zako jiandikie mwenyewe dawa au vipimo.
 
Madaktari wamefunzwa kutengeneza pesa mahospitalini, na siku zote madaktari hujiona wao ni special sana ukiuliza oh! sijui wamesoma kwa tabu na miaka mingi. Na ubaya watu huwa na mitazamo ya kudhani madaktari wanajua kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…