Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

imani yangu kuhusu ENL inazidi kushuka kwa kasi, alikua poa sana lakini tangu ajeruhiwe amekuwa mpole na mnyenyekevu ili kutafuta upenyo wa kulipiza kisasi. sijui akishika hatamu itakuaje.
Possibly makeke yake ulikuwa unayaona kwakuwa alikuwa kwenye power,,kwasasa yuko pembeni kidogo hivyo si rahisi kuonyesha...lakini kiukweli huyu mzee pamoja na mapungufu yake ni AMSHA AMSHA ile mbaya akiwa na Authority.
 
.................. tunamtaka alitue hilo zigo amkabidhi mwenyewe, na yeye ndie ateuliwe kuwa mgombea wa CCM tumpigie debe, aingie Ikulu!.

Mkuu hapo kwenye red. Zigo ni zito mno ER alishaanza kulitua kidogo kidogo! kama vile kumtolea macho mkuu wa kaya kwenye vikao....
 

juzi kwenye habari za channel ten Lowasa ameoneshwa anatoa Mchango wa shiling milion 65
 
Mfano mzuri wa wizi wa EL ni ile proposal ya kutengeneza mvua ili bwawa la Mtera lijae. Hivi sisi ni matajiri kiasi gani kuweza kutengeneza mvua ambayo waarabu wanaohitaji maji wameshindwa kutengeneza?

Kama yule waziri mkuu wa wakati huo hakupinduliwa yangekuwa yale yale ya Richmond, tungesikia kampuni iliyowaleta hawa jamaa ina mahusiano na EL.

MUNGU ATUEPUSHE NA IBILISI HUYU KUTUTAWALA, NI MROHO MNO WA MADARA NA MALI.
 

mkuu huwa nakuheshimu sana lakini linapokuja swala la EL upeo wako huwa unapotea kabisa na kuongea vitu vya ajabu kabisa ambavyo havifanani na ww

Naomba kujua bei yako namimi nizisakae pesa ili unitungie mapambio ya kunisifu na kunipa sifa za kijinga ambazo sistahili.
 
kweli sikuwahi ona mtu akiogelea kuvuka kivukoni lakini kwa magufuli jamaa kaogelea na akavuka vzuri,nkagundua kumbe wabongo tunadeka tu
 
ipo kazi! sioni hizo fedha zilikopatikana kama sehemu kubwa ya maisha yake ni mtumishi seriKalini ...... agh nimekumbuka hivi dowans hawajalipwa? kama wamelipwa sio ajabu sana mapesa yote hayo kutawanywa. kingine kama kweli ni msafi na mpo mawakili mnaotetea uadilifu wa E.L humu JF. tuambieni ile nyumba ulipo ubalozi wa South Afrika pesa za kujengea nyumba ile kapata wapi?
 

sema usemavyo kwa akili yako hakuna mtu au kiongozi yeyote angethubutu au hata kujaribu kufanya aloyafanya lowasa kama ulivyotaja hapo juu labda wewe ungeweza tu.acha ujinga el mchapakazi sio kichwa cha tende cha mzee wa visasi.ngoja mwalim atakapofufuka ataenda moja kwa moja msola kuhoji kwanini alimuua
 
pasco una mahaba na lowassa,lowassa alishindwa kumwambia nyerere alivyopata mali zake!na huoni kumiliki hayo makampuni akiwa kiongozi mwandamizi serikalini kuna conflict of interest au undue influence?
maandamano, Kwanza, tumwache Nyerere aopumzike kwa amani!, kama Nyerere angelifufuka na kuwahukumu aliowaachia nchi, Mwinyi angetupwa gerezani kwa sera ya ruksa na kuliua Azimio la Arusha na kuleta lile la Zanzibar!. Mkapa angefanywa kuni kwa kufanya biashara mahali patakatifu!, JK angetupwa motoni kwa kuigeuza Ikulu ni pango la walanguzi!. Lowassa ana dhambi gani?, msiitaje Richmond, hilo ni zigo la watu na wenye zigo lao wapo!.
 

Mkuu Adobe;
Unahitajika kujibu kwa hoja sio kwa hisia na hasira,najua unampenda Lowassa.Unatakiwa uonyeshe ni kitu gani kigumu ambacho wengine wangeshindwa? ugumu ulikua wapi? Kubaki tu na kusema ati EL mchapakazi bila kuonyesha "anything special" from him hakutatufikisha tunapotaka kwenda.Mimi naona EL ni mtu mwenye rekodi mbaya iliyopita na mnachofanya sasa ni kuhangaika kumsafisha. A good leader must be shining on the majority eyes basing on his/her perfomance,hakuna haja ya kuhangaika kusema sana.


Hamjanijibu maswali yangu wapambe wa Lowassa
 

Pasco

Wewe usitudanganya hapa,Kwa namna yoyote ile huwezi kumtenganisha Lowassa na Richmond hasa kwa nafasi aliyokuwa nayo ya mtendaji mkuu wa serikali.Mtapiga tick tack zote lakini ana case ya kujibu katika richmond.Kama halimhusu kwa nini awajibike kwa kitu kisichomhusu,basi kama aliwajibika kwa kisichomhusu hilo nalo ni kosa ambalo linamwondolea credit pia.

Pasco,huwezi kusema ati tujitenge kuongelea Richmond tunapomwongelea Lowasa,Coz Lowassa ni Richmond na Richmond ni Lowassa,we dont care men behind the scenes.
 
Kiukwelu utjiri alionao lowasa ni mkubwa sana. Hapa wengi watahoji upatikanaji wa huo utajiri. Mimi kwa mtazamo wangu namuona kama lowasa ndiye mtu tunaomuhitaji kwa wakati huu, kwa kuwa ni mtu mwenye mikakati na mipango thabiti ya kututoa hapa alipotuweka mpendwa wetu jk. Achilia mbali na skendo za ufisadi, kwa kweli huyu jamaa tunamihitaji sn kuliko tunavyomsema kwa ufisadi. Mimi naamini lowasa anaweza kufanya makubwa sana kwa nchi hii. Tumpe nafasi kama akipata atufanyie maendeleo.
 
 


10% ya mashangingi ya wabunge.
 
Unajua ktk hili sakata la richmond, lowasa alifanya kosa sana kubeba mzigo ambao si wake. Hapa alikuwa anapaswa kutumia falsafa ya kila mtu atabeba msalaba wake. Binafsi namlaumu sana lowasa kwa hilo. Ona sasa tunamuhitaji atutoe hapa lakini ndo anakutana na vikwazo ambavyo vinamchafulia. Hapa yapaswa huyu jamaa tumsamehe ili tumtumie atuvushe hapa tulipo. Lowasa usivunjike moyo kwa kuwa wewe unaweza ukawa mtu sahihi wa kututoa hapa tulipo.
 

Dhambi ya Lowassa hii hapa:

Salaam kwa Mh. Edward Lowassa na wenzake
 

Sio yako tu, ni mengi sana hayajibiki.
Ukiona mtu anatumia matusi na kashfa ujue......
 


:A S embarassed::shock:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…