Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

imani yangu kuhusu ENL inazidi kushuka kwa kasi, alikua poa sana lakini tangu ajeruhiwe amekuwa mpole na mnyenyekevu ili kutafuta upenyo wa kulipiza kisasi. sijui akishika hatamu itakuaje.
Possibly makeke yake ulikuwa unayaona kwakuwa alikuwa kwenye power,,kwasasa yuko pembeni kidogo hivyo si rahisi kuonyesha...lakini kiukweli huyu mzee pamoja na mapungufu yake ni AMSHA AMSHA ile mbaya akiwa na Authority.
 
.................. tunamtaka alitue hilo zigo amkabidhi mwenyewe, na yeye ndie ateuliwe kuwa mgombea wa CCM tumpigie debe, aingie Ikulu!.

Mkuu hapo kwenye red. Zigo ni zito mno ER alishaanza kulitua kidogo kidogo! kama vile kumtolea macho mkuu wa kaya kwenye vikao....
 
Najiuliza na kukosa majibu Mh.Lowasa si mfanyabiashara,zaidi ya kuwa mbunge,nimejionea siku za hivi karibuni katika vyombo vya habari akichangia mambo mengi hasa katika miradi ya maendeleo  nakatika taasisi binafsi na zamakanisa.Huyu mweshimiwa pesa anazitoa wapi?je alikwisha tangaza mali zake hadharani?na kipato chake kiko vipi?Alipokuwa waziri katika awamu ya tatu kwa nini akufanya hivyo?na alipokuwa waziri mkuu kwa nini alishidwa kufanya hivyo?Na kwa nini safari zake na hotuba zake zinapewa umuhimu mkubwa katika vyombo vyetu vya habari?

juzi kwenye habari za channel ten Lowasa ameoneshwa anatoa Mchango wa shiling milion 65
 
Mfano mzuri wa wizi wa EL ni ile proposal ya kutengeneza mvua ili bwawa la Mtera lijae. Hivi sisi ni matajiri kiasi gani kuweza kutengeneza mvua ambayo waarabu wanaohitaji maji wameshindwa kutengeneza?

Kama yule waziri mkuu wa wakati huo hakupinduliwa yangekuwa yale yale ya Richmond, tungesikia kampuni iliyowaleta hawa jamaa ina mahusiano na EL.

MUNGU ATUEPUSHE NA IBILISI HUYU KUTUTAWALA, NI MROHO MNO WA MADARA NA MALI.
 
Jamii01, fuatilia thread za Lowassa humu utaziona mpaka mali zake zimeorodheshwa!. Lowassa ni tajiri wa ukweli aliyepata mali zake zote kihalali na ndio maana amezisajili zote kwa jina lake na la mkewe Rejina!.

Ila hakuna ubishi CCM imegubikwa na ufisadi hali inayopelekea kila yeyete mwenye chochote kitu kuonekana fisadi.

Lowassa ni miongoni mwa wanaitwa mafisadi wakuu kufuatia kukubali kulibeba lile zigo kubwa la Richmond ili kumnusuru best wake na chama chake na aibu ya mwaka, hivyo yeye kuchafuka kwa kukubali kujitwisha msalaba wa ukombozi na salama ya CCM!.

Anachokifanya huko makanisani na kwenye michango mbalimbali ni kuonyesha uwezo wake kwenye kitu kinachoitwa mass mobilization kwa ajili ya kujiletea maendeleo, kitu ambacho JK ameshindwa kabisa!.

Hilo la kuandikwa magazetini, na kwenye vyombo vya habari, ni kufuatia EL kuwa na mvuto wa ajabu uliotoka kwa Mungu. Kila asemalo linamantik kwa hali ilivyo sasa!. Lowassa ni photo genic!, akipigwa picha anapendezea!, akiongea anavutia kumsikiliza!, na kikubwa zaidi yeye sio mtu wa maneno maneno na vitendo sifuri kama JK, yeye ni mtu wa maneno mafupi na vitendo virefu.

Wakuu wengi waliopo wakisikia JK atatembelea mahali, huandaa taarifa safi, mkuu akifika, akishasomewa taarifa, hupiga makofi na kuendelea na ziara!. Enzi za Lowassa akishasomewa taarifa huipokea na kuelekea physically kuyaangalia hayo yaliyozungumziwa!. Hivyo watu wakisikia JK anakuja, hukaa miguu juu, ila wakisikia ni Lowassa!, kijasho huwa kinawatoka maana jamaa hakubali kabisa longo longo yoyote!.

Ni kufuatia utendaji huu ndio maana mimi na wenzangu wachache humu jukwaani, tumeamua kujitolea kumsafisha Lowassa na ule uchafu wa Richmond, tunamtaka alitue hilo zigo amkabidhi mwenyewe, na yeye ndie ateuliwe kuwa mgombea wa CCM tumpigie debe, aingie Ikulu!.

mkuu huwa nakuheshimu sana lakini linapokuja swala la EL upeo wako huwa unapotea kabisa na kuongea vitu vya ajabu kabisa ambavyo havifanani na ww

Naomba kujua bei yako namimi nizisakae pesa ili unitungie mapambio ya kunisifu na kunipa sifa za kijinga ambazo sistahili.
 
Kama Lowassa ni msafi

1.Kwa nini alifukuzwa ukurugenzi wa AICC kwa kujilimbikizia mali ?,alifukuzwa na Juliasi Nyerere.

2.Kwa nini alijiuzulu kwa sakata la Richmond ambalo nyie mnadai hakuhusika,na kwa nini ameendelea kuficha ukweli hadi sasa kama ni mtu anayetakia mema taifa hili? mbaya zaidi kwa unafiki wake alidai anajiuzulu kwa sababu watu wanautaka uwaziri mkuu wake.

3.Atakuwaje mkombozi wa pili na wakati amekuwapo kwenye serikali kwa miaka mingi sana na hatujaona "something so special" from him?.Afadhali hata magufuli tunaona impact kila sehemu anayoenda.

4.Ni maamuzi magumu gani ambayo mnasema Lowassa ameyafanya? Usitaje kujiuzulu kwa sababu hayo pia ni maamuzi magumu kama ya jambazi anayeenda kuvunja nyumba ya mtu.Amejiuzulu ili kuendelea kulindana na aidha wezi wenzake au wazembe wenzake

Until unijibu maswali haya kiufasaha,ntahamia rasmi kwenye kambi ya Lowassa.
kweli sikuwahi ona mtu akiogelea kuvuka kivukoni lakini kwa magufuli jamaa kaogelea na akavuka vzuri,nkagundua kumbe wabongo tunadeka tu
 
ipo kazi! sioni hizo fedha zilikopatikana kama sehemu kubwa ya maisha yake ni mtumishi seriKalini ...... agh nimekumbuka hivi dowans hawajalipwa? kama wamelipwa sio ajabu sana mapesa yote hayo kutawanywa. kingine kama kweli ni msafi na mpo mawakili mnaotetea uadilifu wa E.L humu JF. tuambieni ile nyumba ulipo ubalozi wa South Afrika pesa za kujengea nyumba ile kapata wapi?
 
Mfuga Ng'ombe;

1.Nashukuru kwa kuniweka sawa katika ishu ya kufukuzwa AICC,niombe radhi kwa kumbukumbu zangu kutokuwa sahihi.On top of that kwa nini alishindwa kuelezea utajiri wake ameutoa wapi alipoulizwa na nyerere 1995?

2.Maamuzi uliyoyataja hapo sioni kama yanastahili kuitwa magumu kwa sababu zifuatazo;

a)Ni masuala ambayo kwa waziri yeyote ambae angekua kwenye post hiyo angeyafanya,tunaweza kusema that was expected of any person in that post.So nothing special.

b)City Water ni moja kati ya kashfa nyingine nyingi zilizokuwepo serikalini hasa wakati alipokuwa waziri mkuu,Hivyo city water tu ambayo pia ni matokeo ya uzembe wa serikali hiyohiyo haiwezi kuwa ni credit ya maana kwake.

c)Msimamo wa maji ya ziwa victoria sio wa Lowassa kama unavyotaka kumbinafsishia,ulikua ni msimamo wa serikali na ni baraza la mawaziri,alitumika kusema.

3.List of Shame ya CDM sio comprehensive list ya mafisadi wote,namaanisha sio mafisadi wote wako katika hiyo list of shame,ila kila aliye katika list of shame ni fisadi.

4.Kama point yenu ninyi wapiga kampeni wa Lowassa ni uchapakazi,basi yeye sio mchapakazi ukimfananisha na Magufuli.Tunaona impact za magufuli kila anapoenda.

5.Amekaa wizara ya maji mda mrefu,je ni asilimia ngapi ya watanzania wanapata maji safi na salama kwa sasa katika reasonable price?

6.Haujanijibu kuhusu kashfa yake ya Richmond.

Asante,nawasilisha

sema usemavyo kwa akili yako hakuna mtu au kiongozi yeyote angethubutu au hata kujaribu kufanya aloyafanya lowasa kama ulivyotaja hapo juu labda wewe ungeweza tu.acha ujinga el mchapakazi sio kichwa cha tende cha mzee wa visasi.ngoja mwalim atakapofufuka ataenda moja kwa moja msola kuhoji kwanini alimuua
 
pasco una mahaba na lowassa,lowassa alishindwa kumwambia nyerere alivyopata mali zake!na huoni kumiliki hayo makampuni akiwa kiongozi mwandamizi serikalini kuna conflict of interest au undue influence?
maandamano, Kwanza, tumwache Nyerere aopumzike kwa amani!, kama Nyerere angelifufuka na kuwahukumu aliowaachia nchi, Mwinyi angetupwa gerezani kwa sera ya ruksa na kuliua Azimio la Arusha na kuleta lile la Zanzibar!. Mkapa angefanywa kuni kwa kufanya biashara mahali patakatifu!, JK angetupwa motoni kwa kuigeuza Ikulu ni pango la walanguzi!. Lowassa ana dhambi gani?, msiitaje Richmond, hilo ni zigo la watu na wenye zigo lao wapo!.
 
sema usemavyo kwa akili yako hakuna mtu au kiongozi yeyote angethubutu au hata kujaribu kufanya aloyafanya lowasa kama ulivyotaja hapo juu labda wewe ungeweza tu.acha ujinga el mchapakazi sio kichwa cha tende cha mzee wa visasi.ngoja mwalim atakapofufuka ataenda moja kwa moja msola kuhoji kwanini alimuua

Mkuu Adobe;
Unahitajika kujibu kwa hoja sio kwa hisia na hasira,najua unampenda Lowassa.Unatakiwa uonyeshe ni kitu gani kigumu ambacho wengine wangeshindwa? ugumu ulikua wapi? Kubaki tu na kusema ati EL mchapakazi bila kuonyesha "anything special" from him hakutatufikisha tunapotaka kwenda.Mimi naona EL ni mtu mwenye rekodi mbaya iliyopita na mnachofanya sasa ni kuhangaika kumsafisha. A good leader must be shining on the majority eyes basing on his/her perfomance,hakuna haja ya kuhangaika kusema sana.

Hamjanijibu maswali yangu wapambe wa Lowassa
 
maandamano, Kwanza, tumwache Nyerere aopumzike kwa amani!, kama Nyerere angelifufuka na kuwahukumu aliowaachia nchi, Mwinyi angetupwa gerezani kwa sera ya ruksa na kuliua Azimio la Arusha na kuleta lile la Zanzibar!. Mkapa angefanywa kuni kwa kufanya biashara mahali patakatifu!, JK angetupwa motoni kwa kuigeuza Ikulu ni pango la walanguzi!. Lowassa ana dhambi gani?, msiitaje Richmond, hilo ni zigo la watu na wenye zigo lao wapo!.

Pasco

Wewe usitudanganya hapa,Kwa namna yoyote ile huwezi kumtenganisha Lowassa na Richmond hasa kwa nafasi aliyokuwa nayo ya mtendaji mkuu wa serikali.Mtapiga tick tack zote lakini ana case ya kujibu katika richmond.Kama halimhusu kwa nini awajibike kwa kitu kisichomhusu,basi kama aliwajibika kwa kisichomhusu hilo nalo ni kosa ambalo linamwondolea credit pia.

Pasco,huwezi kusema ati tujitenge kuongelea Richmond tunapomwongelea Lowasa,Coz Lowassa ni Richmond na Richmond ni Lowassa,we dont care men behind the scenes.
 
Kiukwelu utjiri alionao lowasa ni mkubwa sana. Hapa wengi watahoji upatikanaji wa huo utajiri. Mimi kwa mtazamo wangu namuona kama lowasa ndiye mtu tunaomuhitaji kwa wakati huu, kwa kuwa ni mtu mwenye mikakati na mipango thabiti ya kututoa hapa alipotuweka mpendwa wetu jk. Achilia mbali na skendo za ufisadi, kwa kweli huyu jamaa tunamihitaji sn kuliko tunavyomsema kwa ufisadi. Mimi naamini lowasa anaweza kufanya makubwa sana kwa nchi hii. Tumpe nafasi kama akipata atufanyie maendeleo.
 
Pasco,

EL ni mwizi wa mali za umma, na hiyo ndo source ya mtaji wa utajiri anaokuza kila siku ya iendayo kwa Mungu. Nina mashaka na ulipaji wake kodi huko TRA, kwani pale kwenye makampuni yake ya hapa Dar wakaguzi wa TRA wanagwaya kuyakagua.

EL hawezi kuonyesha chanzo halali alikopata mtaji wa biashara zake, ila atatumia njia ya ku influence watakao hoji jambo hili kwa kuwahonga kidogo. Ndo maana hata katika ripoti ya Mwakyembe kwenda kwa IGP kuhusu njama za kutaka kuuliwa yeye, Mengi na Dr. Slaa alitajwa mtoto wa Lowasa alivyokuwa anawapelekea nyama na chakula ma hit - men. Mwakyembe na Dr. Slaa wamemlipua mara nyingi EL kwamba ni fisadi, anajua wana evidence ya hili ndo maana anataka waondoke duniani.
Kwa kujua udhaifu wa law enforcers, EL anawa control kwa remote, ile report IGP hakuishughulikia zaidi ya kumshauri EL aachane na mpango anaotaka kufanya.
Narudia tena: neno rahisi la kufafanua utajiri wa EL ni kwamba ni kutokana na wizi wa mali za umma.
[/QU
UNAYOSEMA KWELI LAKINI UKICHANGIA KANISA UMEUNGAMA NA MALI HARAMU ZINAKUWA HALALI MFUMO KRISTO
 
ipo kazi! sioni hizo fedha zilikopatikana kama sehemu kubwa ya maisha yake ni mtumishi seriKalini ...... agh nimekumbuka hivi dowans hawajalipwa? kama wamelipwa sio ajabu sana mapesa yote hayo kutawanywa. kingine kama kweli ni msafi na mpo mawakili mnaotetea uadilifu wa E.L humu JF. tuambieni ile nyumba ulipo ubalozi wa South Afrika pesa za kujengea nyumba ile kapata wapi?

10% ya mashangingi ya wabunge.
 
Unajua ktk hili sakata la richmond, lowasa alifanya kosa sana kubeba mzigo ambao si wake. Hapa alikuwa anapaswa kutumia falsafa ya kila mtu atabeba msalaba wake. Binafsi namlaumu sana lowasa kwa hilo. Ona sasa tunamuhitaji atutoe hapa lakini ndo anakutana na vikwazo ambavyo vinamchafulia. Hapa yapaswa huyu jamaa tumsamehe ili tumtumie atuvushe hapa tulipo. Lowasa usivunjike moyo kwa kuwa wewe unaweza ukawa mtu sahihi wa kututoa hapa tulipo.
 
maandamano, Kwanza, tumwache Nyerere aopumzike kwa amani!, kama Nyerere angelifufuka na kuwahukumu aliowaachia nchi, Mwinyi angetupwa gerezani kwa sera ya ruksa na kuliua Azimio la Arusha na kuleta lile la Zanzibar!. Mkapa angefanywa kuni kwa kufanya biashara mahali patakatifu!, JK angetupwa motoni kwa kuigeuza Ikulu ni pango la walanguzi!. Lowassa ana dhambi gani?, msiitaje Richmond, hilo ni zigo la watu na wenye zigo lao wapo!.

Dhambi ya Lowassa hii hapa:

Salaam kwa Mh. Edward Lowassa na wenzake
 
Mkuu Adobe;
Unahitajika kujibu kwa hoja sio kwa hisia na hasira,najua unampenda Lowassa.Unatakiwa uonyeshe ni kitu gani kigumu ambacho wengine wangeshindwa? ugumu ulikua wapi? Kubaki tu na kusema ati EL mchapakazi bila kuonyesha "anything special" from him hakutatufikisha tunapotaka kwenda.Mimi naona EL ni mtu mwenye rekodi mbaya iliyopita na mnachofanya sasa ni kuhangaika kumsafisha. A good leader must be shining on the majority eyes basing on his/her perfomance,hakuna haja ya kuhangaika kusema sana.

Hamjanijibu maswali yangu wapambe wa Lowassa

Sio yako tu, ni mengi sana hayajibiki.
Ukiona mtu anatumia matusi na kashfa ujue......
 
Unajua ktk hili sakata la richmond, lowasa alifanya kosa sana kubeba mzigo ambao si wake. Hapa alikuwa anapaswa kutumia falsafa ya kila mtu atabeba msalaba wake. Binafsi namlaumu sana lowasa kwa hilo. Ona sasa tunamuhitaji atutoe hapa lakini ndo anakutana na vikwazo ambavyo vinamchafulia. Hapa yapaswa huyu jamaa tumsamehe ili tumtumie atuvushe hapa tulipo. Lowasa usivunjike moyo kwa kuwa wewe unaweza ukawa mtu sahihi wa kututoa hapa tulipo.

:A S embarassed::shock:
 
Back
Top Bottom