Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

I dont believe so, EL is strong , yes, lakini sidhani kama proffesional journalist hawezi kum-face na kumuuliza

unakumbuka alivyoita waandishi wa habari nyumbani kwake?? kuna waandishi walimuuliza kuhusu issue ya Richmond!!imagine kwa miaka zaidi ya mitatu waandishi waliandika mengi sana kuhusu ufisadi wa huyu mtu! lakini siku walipokutana naye walimuuliza kuwa 'kama wanayoyaandika ni kweli'

hauhitaji kujua mind set za magazeti yetu, waandishi wetu ...ni umbea na kuuza magazeti basi! na sisi tunanunua tukifurahia fulani kuitwa fisadi! sometime we even call these journalists ni heroes...eti haogopi!

kama EL fisadi nakala hii haimsaidii mtanzania wa kawaida, why they are not pressing government to press charge against these criminals? au kuwa mzalendo wa kweli nchi hii ni 'kubweka tu' na katu si kupigana wezi wapelekwe jela

asilolijua huyu mwandishi ni kuwa watu wa aina ya Lowassa wakialikwa huwa wanasambaza kadi kwa rafiki zake,wanachanga na baadae kwenda mahali husika ambako anawasilisha michango. si siri kuwa yeye ni tajiri na ambao wanao katika familia yake hata kabla ya kuwa kiongozi! wengine tusiojua mambo tunafahamu hivi kwa kufanya upelelezi mdogo tu.

muda umefika wa kubadili teknic zetu za kupambana na mafisadi...

magazeti yanauza tu hawako real
Mkuu Waberoya, you have a point and I agree with you to large extend. Kusema ukweli waandishi wengi hawajui watakula vipi bila kuwa na bahasha kutoka kwa politicians, kuna mambo mengi yanahitaji kuzungumziwa au kuandikwa ili kumsaidia mwananchi wa wakawaida, lakini hayaandikwi.
Pengine fani hii basi imekuwa ni kimbilio la wanaopenda kupiga dili za mjini wanavyoita wenyewe. Its too sad we know what the right thing to do, yet we can't do anything to rectify the situation. EL anamakosa yake, lakini hayuko/hakuwa peke yake na ndiyo maana ana nguvu ya kusonga mbele wakati huu bila pingamizi kuuubwa ndani ya chama chake. Utakubaliana namimi kuwa, EL kawashika pabaya CCM wakati huu kuliko kipindi cha nyuma. Na pengine kundi pekee lilikuwa linaleta upinzani mkubwa kwa EL ni hili la akina Dr Mwakyembe & Mzee Six. Anyway, tuendelee kusubiri upepo ndani ya chama tawala hadi uchaguzi utakapofanyika hapo baadae mwaka huu.
 
Milion 152 kwa siku, zidisha kwa miaka miwili. i.e 152,000,000x730=110,960,000,000. Hii ni miaka miwili tu ya Richmond. Michango yooooote, alowai kutoa haijafika hata bilion moja. Hata kama hamna marafiki, ana uwezo wa kuchanga mihela hadi october 2015.
Lakini swali la kujiuliza, kwa nini hiyo misaada wasichangie kwenye huduma za jamii kama hospitali au shule? Hili jambo Watanzania tunatakiwa tulitazame kwa mapana zaidi! Haiwezekani ikiwa ukarimu, kuna jambo hapa!
 
kinacho nichanganya toka mwanzo ni huyu jamaa kuitwa waziri mkuu mstaafu, kivipi? wanaficha nini? huyu jamaa ni mtu hatari sana, na ccm wanampa kichwa vilivyo.
 
Huyu ni journalist, anatakiwa amfuate EL na kumuuliza ana kwa ana kulikoni? anaweza akajuakila kitu deeply....hatuna waandishi wa habari wa namna hii Tanzania....wote wamebaki kuandika nakala na kubadili misamiati na kuandika kwa style tofauti.....these kind of b/shit journalism imeiua Tanzania na kudumaza bongo za wengi.

marupurupu ya serikali na fedha za richmond ndio zina mpa nguvu hivi?

yaani EL ni tajiri sana kiasi kwake mmillioni 60 kuipoteza haiumi??

kua asichokijua mwandishi kuhusu hizi changizo na hajataka kuelewa

aaargh! naenda chuo cha uandishi wa habari

Waberoya huna sababu ya kumshambulia huyu mwandishi eti kwavile hakumuuliza Lowassa hao marafiki wanaomchangia hizo fedha ni wakina nani? Lowassa anapokuwa huko kwenye harambee hufuatana na wapambe wachache ambao hawawezi kuchangisha kiasi hicho cha fedha; mara nyingi hufuatana na mbunge wa Kigoma Serukamba, ambae maisha yake yote humtegemea Lowassa kwa kuishi; pia wanakuwepo wafanya biashsra wadogo wadogo wachache anaowakusanya toka Arusha; hawa wote hawaelekei kuwa wana pesa kiasi hicho cha kumchangia !! Ni wazi kuna watu ambao hawaonekani ambao wanachanga pesa za kumuwezesha Lowassa kuchangia haya mamilioni ya pesa na lazima hizi ni pesa chafu ama sivyo wafadhili wake wasingejificha na yeye asingewaficha pia!! Ndio maana mwandishi anauliza hawa wanaomfadhili Lowassa mapesa yote haya ni Rostam na nani wengine; mdogo wa Rostama alikamatwa huko Tanga na madawa ya kulevya yenye thamani ya mabillion ya shillingi je hizi ndio fedha zinazomfadhili Lowassa? Huo utajili wa kifamilia aliokuwa nao Lowassa unaujua wewe peke yako, kwani mwalimu alipomsema juu ya utajili wa upesi upesi aliojilimbikizia wakati huo hakuwa na familia? Huyu bwana kama Chenge wamechuma hizo fedha kwa kuwa watumishi wa serikali hakuna ng'ombe wala nguruwe waliouzwa kupata utajiri huo!!
 
Jiulize Lowasa atakapokua Raisi wa hii nchi atazirudishaje hizo hela? Tafakari sana ewe Mtanzania!
 
I dont believe so, EL is strong , yes, lakini sidhani kama proffesional journalist hawezi kum-face na kumuuliza

unakumbuka alivyoita waandishi wa habari nyumbani kwake?? kuna waandishi walimuuliza kuhusu issue ya Richmond!!imagine kwa miaka zaidi ya mitatu waandishi waliandika mengi sana kuhusu ufisadi wa huyu mtu! lakini siku walipokutana naye walimuuliza kuwa 'kama wanayoyaandika ni kweli'

hauhitaji kujua mind set za magazeti yetu, waandishi wetu ...ni umbea na kuuza magazeti basi! na sisi tunanunua tukifurahia fulani kuitwa fisadi! sometime we even call these journalists ni heroes...eti haogopi!

kama EL fisadi nakala hii haimsaidii mtanzania wa kawaida, why they are not pressing government to press charge against these criminals? au kuwa mzalendo wa kweli nchi hii ni 'kubweka tu' na katu si kupigana wezi wapelekwe jela

asilolijua huyu mwandishi ni kuwa watu wa aina ya Lowassa wakialikwa huwa wanasambaza kadi kwa rafiki zake,wanachanga na baadae kwenda mahali husika ambako anawasilisha michango. si siri kuwa yeye ni tajiri na ambao wanao katika familia yake hata kabla ya kuwa kiongozi! wengine tusiojua mambo tunafahamu hivi kwa kufanya upelelezi mdogo tu.

muda umefika wa kubadili teknic zetu za kupambana na mafisadi...

magazeti yanauza tu hawako real

Nakubaliana na wewe. Huyu ni mmoja wa waandishi makanjanja wanapandikiza fikra za kufikirika ndani ya vichwa vya watanzania.... haya yalitakiwa yaandikwe endapo tu EL atachukua fomu ya kugombea 2015 na si sasa!
 
Lowassa aliiba sana kipindi kile Serikali inaingia tenda ya kuagiza magari ya Toyota Kwa Ajili ya matumizi ya serikali.Yeye ndiye aliyesimamia ile tender na hivyo ten percent jamaa kapiga.Infact jamaa ni mwizi nafasi zote za utumishi wa umma alizokua anapata anazitumia vilivyo kwa kuiba.Ila the good thing with him ni mwizi mwenye akili.Kuna wezi wengine wanaiba,kwa mfano ananunua mahekari ya ardhi na kuyaacha idle.Huyu bwana hawezi kuiacha hiyo ardhi idle,analima.Ila kwa kifupi EL ni mwizi kama wezi wengine wote CCM.
 
Wazazi acheni mpunga uliwe KKKT ndo wanaongoza kulamba,kwa Kadinali Pengo ndo haooo wanaingia jamvini Ifakara,mashehe nafikiri waanze kunawa mbele ya Pesa hata Kritu alisalitiwa hatuwashangai makasisi; mwacheni amwage mchele halafu habari ya uraisi wataisikia kwenye bomba; CCM wakimleta mtu mzima Edo,itabidi Dr Slaa atangaze baraza la mawaziri kabla ya Kampeni na ndo itakuwa kiama chao; ila mpunga tule tu haina kokoro;
 
No free lunch in this world, [Wazungu]. Ukitaka kula sharti uliwe kidogo, [JK]. Sasa kaa ukijua, ipo siku moja zitarudi tena nyingi zaidi.
 
Huyu ni journalist, anatakiwa amfuate EL na kumuuliza ana kwa ana kulikoni? anaweza akajuakila kitu deeply....hatuna waandishi wa habari wa namna hii Tanzania....wote wamebaki kuandika nakala na kubadili misamiati na kuandika kwa style tofauti.....these kind of b/shit journalism imeiua Tanzania na kudumaza bongo za wengi.

marupurupu ya serikali na fedha za richmond ndio zina mpa nguvu hivi?

yaani EL ni tajiri sana kiasi kwake mmillioni 60 kuipoteza haiumi??

kua asichokijua mwandishi kuhusu hizi changizo na hajataka kuelewa

aaargh! naenda chuo cha uandishi wa habari

Yeye kama mwandishi anaweza kuwa anajua lakini anachokonoa ili jamii iamke na kumjua mhusika ni mtu wa aina gani na pia sio kila mtu anakuwa tayari kurelease financial statements ama reports zake kwa public wewe unafanya hivyo bank accounts zako marafiki zako wanajua zina kiasi gani?sometimes hata mke wako kama unae pengine unamficha.Hebu rejea ile tamtthilia iliyoisha kabla haijaanza ya viongozi kutaja mali zao ndio utajipa majawapo ya hoja zako.
 
Hivi alishatamka kwamba anautaka urais au ni tetesi tu?

mbona unakurupuka kiasi hicho mzee,nani kazungumzia habari ya urais?umeona neno urais au rais kwenye comment yangu uliyoniquote au umeona nimesema kuna mtu katangaza nia ya kugombea urais?muwe mnasema kwanza comment ya nusu mstari na unaona uvivu kuisoma yote.
 
Nakubaliana na wewe. Huyu ni mmoja wa waandishi makanjanja wanapandikiza fikra za kufikirika ndani ya vichwa vya watanzania.... haya yalitakiwa yaandikwe endapo tu EL atachukua fomu ya kugombea 2015 na si sasa!

wewe kenge inaonekana moja kwa moja ni mtetezi maalum wa lowassa maana unajibu kila coment inayomhusu jamaa,nimekutazama sana,uzuri watetezi wa lowasa kila siku ni wale wale mnahama toka thread moja hadi nyingine,ndio hatupati tabu siku hizi na umaarufu wa bandia wa lowasa humu ndani,maana hamuongezeki ni walewale tu mko kama 6 hivi lakini ni mahodari wa kuwemo humu muda mwingi,kiufupi lowassa hafai hafai hata kwa huo ubunge alionao ndio maana jamaa kamgonga..sio urais kwa kuwa kwenye urais yeye wala hafikiriwi tena bali huo ubunge alionao tunataka auachie akaendeleze biashara zake huko
 
ni obvious ni fedha itokanayo na rushwa,maana ukimhoji aliipataje kuanzia mwanzo hatakuwa na majibu,huyu bwana hajafanya a days job zaidi ya siasa.
 
Waberoya huna sababu ya kumshambulia huyu mwandishi eti kwavile hakumuuliza Lowassa hao marafiki wanaomchangia hizo fedha ni wakina nani? Lowassa anapokuwa huko kwenye harambee hufuatana na wapambe wachache ambao hawawezi kuchangisha kiasi hicho cha fedha; mara nyingi hufuatana na mbunge wa Kigoma Serukamba, ambae maisha yake yote humtegemea Lowassa kwa kuishi; pia wanakuwepo wafanya biashsra wadogo wadogo wachache anaowakusanya toka Arusha; hawa wote hawaelekei kuwa wana pesa kiasi hicho cha kumchangia !! Ni wazi kuna watu ambao hawaonekani ambao wanachanga pesa za kumuwezesha Lowassa kuchangia haya mamilioni ya pesa na lazima hizi ni pesa chafu ama sivyo wafadhili wake wasingejificha na yeye asingewaficha pia!! Ndio maana mwandishi anauliza hawa wanaomfadhili Lowassa mapesa yote haya ni Rostam na nani wengine; mdogo wa Rostama alikamatwa huko Tanga na madawa ya kulevya yenye thamani ya mabillion ya shillingi je hizi ndio fedha zinazomfadhili Lowassa? Huo utajili wa kifamilia aliokuwa nao Lowassa unaujua wewe peke yako, kwani mwalimu alipomsema juu ya utajili wa upesi upesi aliojilimbikizia wakati huo hakuwa na familia? Huyu bwana kama Chenge wamechuma hizo fedha kwa kuwa watumishi wa serikali hakuna ng'ombe wala nguruwe waliouzwa kupata utajiri huo!!

Mkuu tatizo lako na mwandishi ni kuona ni fedha chafu, haujui akina nani wanaochanga fedha na yet unasema ni fedha chafu.Hivi ukiwa na fedha safi lazima ujitangaze?? mkuu unapata wapi hii theory

Pili kusema fedha chafu zinapokelewa na nani?aliyeziona chafu ni wewe na mimi, je makanisani na misikitini wanaziona chafu?? au wale ni watoto hawafikirii wala kuona, ila nyie mna akili?

je fedha hii chafu kanisani inakuwa fedha safi? si chafu? kwa nini usi-mobilize waumini wasiingie kwenye makanisa na mashule ya kiislamu yaliyojengwa na fedha hizi chafu? can you?

ukishindwa hiyo task unarudi kulekule kuwa watu wako tofauti na mwandishi inabidi alijue hili

mwisho ili kubadili strategy nimeuliza mtu mchafu anaandikiwa nakala? kwa nini waandishi wetu hawabadili technic?? tangu lini tumesikia haya, umeishawahi kuona nakala inamsema vibaya DPP, CAG, waziriwa sheria na chief justice kuwa hawawezi kuwapeleka hawa wezi kortini?? hivi ukiimba fedha zile chafu ndio zinarudi, si inawezekana katika mzunguko ule na wewe umezipata kwa nini tunajisiwe na fedha chafu , na huku tunatumia fedha chafu?

tukubali tumeshindwa na sasa tumebaki kubweka tu!
 
Waberoya, makala nyingi zimeaandika juu ya DPP na uhusiano wake na watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi na ndio maana kesi zao hazipelekwi mahakamani; pia makala nyingi zimeandikwa juu ya Rostam Azizi na jinsi alivyohusishwa na wizi wa EPA na ingawa ushahidi upo wa kujitosheleza wa kuweza kumpeleka mahakamani [ikiwemo confession ya Manji kuhusu Kagoda] lakini serikali haioni umuhimu wa kufanya hivyo. Pesa za Lowassa ni chafu kwasababu kama nilivyoeleza kuwa Rostam Azizi ni mfadhili na mshirika wake mkubwa ambae anahusishwa na pesa chafu!!
 
Mkuu tatizo lako na mwandishi ni kuona ni fedha chafu, haujui akina nani wanaochanga fedha na yet unasema ni fedha chafu.Hivi ukiwa na fedha safi lazima ujitangaze?? mkuu unapata wapi hii theory

Pili kusema fedha chafu zinapokelewa na nani?aliyeziona chafu ni wewe na mimi, je makanisani na misikitini wanaziona chafu?? au wale ni watoto hawafikirii wala kuona, ila nyie mna akili?

je fedha hii chafu kanisani inakuwa fedha safi? si chafu? kwa nini usi-mobilize waumini wasiingie kwenye makanisa na mashule ya kiislamu yaliyojengwa na fedha hizi chafu? can you?

ukishindwa hiyo task unarudi kulekule kuwa watu wako tofauti na mwandishi inabidi alijue hili

mwisho ili kubadili strategy nimeuliza mtu mchafu anaandikiwa nakala? kwa nini waandishi wetu hawabadili technic?? tangu lini tumesikia haya, umeishawahi kuona nakala inamsema vibaya DPP, CAG, waziriwa sheria na chief justice kuwa hawawezi kuwapeleka hawa wezi kortini?? hivi ukiimba fedha zile chafu ndio zinarudi, si inawezekana katika mzunguko ule na wewe umezipata kwa nini tunajisiwe na fedha chafu , na huku tunatumia fedha chafu?

tukubali tumeshindwa na sasa tumebaki kubweka tu!

Ni makala mheshimiwa sio nakala.Tumeshindwa katika nini hasa labda umeshindwa wewe na genge lako,leo watu hawako tena kamati kuu...na pia watatakiwa kuchagua kati nec ama ubunge huo ushindi wa kupita pita makanisa ni ushindi hafifu sana
 
heshima kwa wanajukwaa.Nimekuwa napata taarifa kumuhusu Lowasa, leo kasaidia mil 70 Mbeya,kesho Mil 100 KKKT Mwanza nk.
Mh Lowasa ni mbunge kama wabunge wengine na hata kama atasema anatumia pension ya uwaziri mkuu haitatosha nishawishi kuamini anapotoa pesa hizo..kwa mahesabu ya harakaharaka huyu mzee anafikisha mil 500 na zaidi kwa mwaka huu pekee kwa misaada tu. kwa mimi mTanganyika wa kawaida hizi pesa ni nyingi sana..
Mheshimiwa ninaomba unijuze wapata wapi hizo senti na mimi nkajichotee.
 
Lowasa kaweka hela kwenye ma tank kama ya kuhifadhia maji
Ma-Sim tanks!!

Swali gani unauliza hilo?? Umeshawagi kumuona lowasa akiwa anatoa cheque?? Yeye na maburungutu ya pesa tu!!! Anachota kwenye sim tank!!!

Yule masai kiboko ya nape na ccm wote!!
 
heshima kwa wanajukwaa.Nimekuwa napata taarifa kumuhusu Lowasa, leo kasaidia mil 70 Mbeya,kesho Mil 100 KKKT Mwanza nk.
Mh Lowasa ni mbunge kama wabunge wengine na hata kama atasema anatumia pension ya uwaziri mkuu haitatosha nishawishi kuamini anapotoa pesa hizo..kwa mahesabu ya harakaharaka huyu mzee anafikisha mil 500 na zaidi kwa mwaka huu pekee kwa misaada tu. kwa mimi mTanganyika wa kawaida hizi pesa ni nyingi sana..
Mheshimiwa ninaomba unijuze wapata wapi hizo senti na mimi nkajichotee.

Ile njemba hatari bana mie nafikiri baadhi ya pesa ilizaliwa nazo
 
Back
Top Bottom