Kidatu, there you are!. Urais 2015 ni vita!. Watanzania tuna haki na utajiri wa mali asili zetu tulizojaaliwa na Mwenyezi Mungu ambazo hawa manyang'au waliopo wamezitoa sadaka kwa wanaojiita wawekezaji, huku wakikomba kila kitu na kutuacha beggera!. Tanzania sio masikini kihivyo!. Kwa vile Tanzania yenye utajiri na neema ni haki yetu, na haki hiyo hatutaletewa kwenye kisahani cha chai, ni lazima tuipiganie, haki hailetwi, bali inadaiwa na ikibidi inapiganiwa na ndipo inapatikana!.
Wengi wa wanaotamani ukombozi wa kweli, wanautamani wakiamini siku moja ukombozi huo utashushwa toka mbinguni na sisi kutunukiwa kama ile mikate ya mana enzi za Nabii Mussa!. Mimi nasema, haki hiyo lazima itafutwe, idaiwe, ipiganiwe na hata ikibidi damu za watu zimwagike ili ipatikane!.
Kwa wale tunaokubaliana kuwa urais 2015 ni vita, na ili ushinde vita lazima umjue adai yako, kwenye vita hivi vya ukombozi wa pili, adui yetu number moja ni CCM!. Sasa wale wote wanaodhania serikali ya CCM itaotoa utawala kwa wapinzani kama zawadi!, they are wrong!, CCM would wish to consolidate power ili itawale milele!. Kwa vile CCM does exist, mimi ni muumini wa falsafa ya Baba wa Taifa kuwa ukombozi wa kweli wa nchi hii utatokana na upinzani wa kweli ambao utatoka CCM!.
Mimi na wenzangu wachache humu jukwaani, we can see a light on Lowassa, huyu ndie mtu pekee anaweza kuleta ukombozi wa kweli!. Hivyo tunampigania kwa nguvu zetu zote!.
Kitendo cha Lowassa kukubali kubeba zambi za wengine ili CCM iokoke ni uthibitisho wa ushajaa mkubwa alionao ambao mimi naufananisha na Bwana Wetu Yesu Kristu kukubali kubeba dhambi za ulimwengu ili sisi tuokoke!.
Wale mnaosema kwa Lowassa kubeba zambi za wezi, hivyo na yeye ni mwizi!, jee Yesu alivyokubali kubeba zambi za ulimwengu, jee na yeye ni mzambi!. Wajameni tusihukumu tusije tukahukumiwa!.
Naendelea kusisitiza, wale wote mnaoniaminia mimi Pasco wa jf, nawaombeni sana lets bank on Lowassa as the one and only anaweza kuleta mabadiliko ya kweli na tukapata 'ukombozi wa pili'!
Wale wote mnaonibeza na kuamini nimelipwa, nimenunuliwa, najikomba etc, endeleeni kuamini hivyo, kwa kuwasaidia tuu,
kwa wasionijua, tangu enzi za utotoni, pale Msasani kwa Mwalimu ilikuwa ni playing ground yetu!, sekondari nimesoma na mtoto wa kwa Mwalimu, nimesoma darasa moja na mtoto wa Ben, wakati huo mtoto wa Mwinyi akiwa A-Level, Chuo Kikuu nimekutana na mtoto wa JK, hivyo ile access ya one to one na Nyerere (RIP), Mwinyi, Mkapa na JK has/is always there, hivyo kama ni lobbyst ya kujipatia kijipost chochote, basi ningeshalobby zamani na labda saa hizi ningekuwa kivulini!.
Lowassa ni sikio la kufa, sasa nijikombe kwa Lowassa ili nipate nini?. Naombeni mniaminie, kuna type ya watu ambao wao ni masikini na wanaridhika na umasikini wao, hawa wanaitwa "masikini jeuri" na mimi niko kwenye kundi hilo!. Sijalipwa senti tano na yoyote kumpigania Lowassa!.
Namalizia kwa msisitizo, Lowassa ni chaguo la Mungu, lile ambalo kwa binaadamu haliwezekani, kwa Mungu linawezekana!. Subirini mshuhudie "Jiwe Walilolikataa Waashi, Litafanywa Kuwa Jiwe Kuu la Pembeni!".
Pasco
Ni haki yako ya msingi kuwa na maoni yako,lakini sidhani ni sahihi kuwaaminisha wale unaowapa maoni yako upuuzi ambao hata yule aliyelazwa pale Muhimbili kwa matatizo ya akili hawezi kuupokea. Nianze kwa kusema kwamba Edward Lowasa ni jizi lililokubuhu la mali za taifa letu na kamwe usijidangaye na kutaka kuwadanganya WaTZ kwamba huyu Fisadi anatumia sana akili katika kutafuta na kuendeleza biashara zake kwa njia halali.Kamishna wa TRA aliwahi kuzuia uchunguzi wa Kodi za Majengo (Property Tax) anayomiliki huyo Mwizi EL baada ya watumishi wa TRA kufukuzwa na EL wakati huo akiwa PM kumuamuru Kamishna huyo kutothubutu tena kufuatilia mambo hayo.Amepangisha majumba yake lakini hataki kulipa Kodi za Serikali halafu unataka kutuaminisha kwamba huyo ndiye Kiongozi tunayemtaka kwa maendeleo ya Taifa hili,wewe komea hukohuko Monduli na huyo EL wako.
Bwana wetu YESU KRISTO alikuja hapa ulimwenguni kuwapatanisha Wanadamu na Muumba wao MUNGU baada ya Kumuasi,watu walikuwa wakiabudu miungu mingine pamoja na sanamu, wanadamu kwa ujumla wao walikuwa ni watenda dhambi.Untakiwa kujua kwamba MUNGU wetu ni MUNGU mwenye wivu, kamwe hataki kulinganishwa na chochote.
Sasa unapoleta hadithi zako za kipuuzi eti EL alipokubalika kubeba zigo la Richmond alikuwa akifanya sawa na YESU aliyekubali kubeba dhambi za Wanadamu ili wapate kuokoka na kupatanishwa na MUNGU wao, hakika huo ni upuuzi na Ujinga hasa kwa mjivuni kama wewe unayedai Elimu yako ni ya Chuo Kikuu.Yaani unataka kutuambia kwamba zigo la wezi wa Richmond alilobeba EL ilikuwa ni dhamana yake kwa WaTZ wote ambao kwa tasfsiri yako hiyo kwamba wote ni wezi ? Au alibeba ili kuwasaidia wezi wenzake ambao mipango yao ni kupeana madaraka kama pipi siku za usoni,scratch my back I'll scratch yours.Hoooovyoooo.
Hii ni Nchi yenye raia zaidi ya 30 milioni wenye uwezo kamili wa kutuongoza, kwanini EL yeye ana nini so special ambacho WaTZ wanakihitaji ? WaTZ wamesahau nini katika hicho kichwa cha EL hadi wahitaji tena kutumia kichwa chake kutuongoza, kichwa kilichojaa akili ya wizi mtupu.Lowasa ameshiriki wizi mwingi hapa nchini, alimsumbua sana Mwanasheria wa Tanesco MRS.WANDIBA hadi usiku wa manane kwa kumpigia simu ili aweze kutayarisha Documents za mikataba ya hovyo na Ulaji lakini huyo Mama akasimama kidete na Kumkatalia.Alimwogopa kumfukuzisha kazi kwa kuwa kwanza huyo Mama anatoaka kwenye Familia ya Mwalimu Nyerere lakini vilevile Mume wa huyo Mama MR.WANDIBA ndiye Mkuu wa Chuo cha Wanausalama kule Mbweni, nafasi ambayo ni kubwa na amekuwa kwenye System wakati EL bado anavaa Lubega Monduli.
EL anahitaji kushauriwa na wengine (si wewe Pascho) kutafuta shughuli nyingine ya kufanya aachane na sisi wabongo kuhusu uongozi wa nchi yetu, ushenzi aliyokwisha kuifanyia Nchi yetu pendwa TANZANIA ni mkubwa