Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Mh. Edward N. Lowassa anapata wapi nguvu ya pesa?

Dr. Pombe Magufuli is a better choice than EL.

Kweli nyani haoni masaburi yake !!! Unajua nyumba za serikali zilikua zinauzwa na nani? Unajua aliuzia nyumba hizo wanachama wa familia yake ambao siyo hata watumishi wa serikali? Kuna nyumba za serikali ziliuzwa Oysterbay kwa $ 20,000.00 leo vigogo wanaziuza kwa $ 2 mill?
Kuna maswali mendi sana kwenye suala la kuuzwa nyumba za serikali. Mtu anaweza kusema iliamuliwa na baraza la mawaziri na yeye alikua mtekelezaji, mimi nitauliza kwa nini hakujiuzulu kupinga wizi huu? Kwa nini atleast hazikuuzwa at a fair market value? Kwa nini watu wasiostahili kuuziwa nyumba hizi waliuziwa? Kwa nini mawaziri mpaka leo wanakaa hotelini wakati serikali ilikuwa ina nyumba za wao kuishi?
Kashfa ya kuuza nyumba za serikali imeitia hasara kubwa serikali kuliko ufisadi wote unaodhaniwa wa Lowassa !! Think about it.
Mshikaji wako hafai. Ana jazba sana.Hashirikishi ubongo latika maamuzi yake. Hana tofauti na Pinda aliyehukumu wauaji wa maalbino moja kwa moja kwamba wauawe, mahakama zipo kwa ajili gani? Inabidi wauawe kwa amri ya mahakama siyo kwa amri ya Mheshimiwa. Dr. wako anaongoza kwa hisia zaidi, anafaa zaidi kuwa academician than a political leader.
 
Hapana, hapana, hapana, Hukunielewa. I agree with most of the stuff you have wriiten, ndio vity ambavyo watanzania wanahitaji kwa leo hii. A strong leader with a vision. lakini bado nakataa kwa herufi kubwa choice yako.

Akitokea mtu mwingine mwenye verified and proven track record of these qualities, other than Lowassa nitakuunga mkono Okada. Lakini kwa sasa hivi sijaona mwingine bado.
EL siyo muoga, ana ushawishi, ana maamuzi, hana urasimu na mbunifu. Vitu ambavyo hata wewe unakubali kwamba ni sifa za kiongozi tunayemhitaji.
 
Hapop kwenye red. Huu ubunifu umepitiliza. Ubunifu wa Richmond.
Ndugu yangu, mwenye hilo jina la avator yako akijua unatemtetea... he will turn in his grave!
Why do not you consider changing your name?
Mobutu could be better than Nkwame Nkuruma....
 
Nimefurahi kuona kwamba una kumbu kumbu za events. Unafahamu alichokuwa anafanya mshikaji wako EL wakati anatembelea Mikoani/Wilayani/halmashauri? Behind the scenes??? Unajua ni kwa nini walikuwa wanamwogopa (ukiacha swala la yeye kuhakikisha kila anachoambiwa?????????))) Behind the scenes???? si unajua alivyoisuka TAMISEMI kwa ajili ya haya unayomsaidia kupigania hapa?

Alikua anafuatulia maendeleo na ahadi za serikali kwa wananchi wake. Serikali inatakiwa kuogopa wananchi, na siyo kinyume chake.
Watumishi walikua wanamuogopa kwa sababu wao walikua wamezoea kufanya kazi kwa mazoea yeye alikua anawakumbusha wajibu wao kila alipoenda.
 
Hapop kwenye red. Huu ubunifu umepitiliza. Ubunifu wa Richmond.
Ndugu yangu, mwenye hilo jina la avator yako akijua unatemtetea... he will turn in his grave!
Why do not you consider changing your name?
Mobutu could be better than Nkwame Nkuruma....

Kwa nini mnapozungumzia issue ya Richmond hamumtaji JK?
Nkrumah is my role model kwa jinsi alivyokua na original ideas and started projects from scratch, Akasombo dam, The port and aluminium smelter plant at Tema, just to name a few. Viongozi wa sasa wa Africa hawana hizi qualities. Wachache wana similar qualities Kagame ni mmoja wao, EL akipata nafasi ni mmoja wao.
 
Alikua anafuatulia maendeleo na ahadi za serikali kwa wananchi wake. Serikali inatakiwa kuogopa wananchi, na siyo kinyume chake.
Watumishi walikua wanamuogopa kwa sababu wao walikua wamezoea kufanya kazi kwa mazoea yeye alikua anawakumbusha wajibu wao kila alipoenda.

Hapana. You have missed a point kuhusu mshikaji wako. Sio mzuri kama unavyodhani. waulize watu wa TAMISEMI hili mwanalijua vizuri sana.
Unajua ni nani alimsukia ajali aliyekuwa Municipal director wa Kinondoni na ikawezekana kumhamisha kuwa RAS Singida? Unajua kisa ni nini? unajua hili lilifanikishwa na kina nani, hadi Mkuu ya Kaya bila kujua????
 
Kwa nini mnapozungumzia issue ya Richmond hamumtaji JK?
Nkrumah is my role model kwa jinsi alivyokua na original ideas and started projects from scratch, Akasombo dam, The port and aluminium smelter plant at Tema, just to name a few. Viongozi wa sasa wa Africa hawana hizi qualities. Wachache wana similar qualities Kagame ni mmoja wao, EL akipata nafasi ni mmoja wao.

Kagame na EL ni kama Uislam na ukisto!
 
Akitokea mtu mwingine mwenye verified and proven track record of these qualities, other than Lowassa nitakuunga mkono Okada. Lakini kwa sasa hivi sijaona mwingine bado.
EL siyo muoga, ana ushawishi, ana maamuzi, hana urasimu na mbunifu. Vitu ambavyo hata wewe unakubali kwamba ni sifa za kiongozi tunayemhitaji.

Haya unayoyasema ni kweli kabisa. Shida, kale katabia ka ufisadi! kwa hilo, mimi na wewe tutatofautiana hadi siku ya mwisho.
 
Kwa nini mnapozungumzia issue ya Richmond hamumtaji JK?
Nkrumah is my role model kwa jinsi alivyokua na original ideas and started projects from scratch, Akasombo dam, The port and aluminium smelter plant at Tema, just to name a few. Viongozi wa sasa wa Africa hawana hizi qualities. Wachache wana similar qualities Kagame ni mmoja wao, EL akipata nafasi ni mmoja wao.

KWani tukimtaja JK ndio itabadilisha nini? hapa tunaongelea EL na sio JK mkuu!
 
Ni kweli kwamba ENL ni mtu tajiri sana,ana hela nyingi ambazo sasa anazitumia kuanza maandalizi ya kuwa rais.Ninavyo muona huyu bwana kwa harakati zake hizi anazoendelea nazo inaelekea atkuja kuwa the next president wa nchi hii.Lakini mkae mkijua kwamba huyu bwana ana kila dalili za kuwa dikteta.Ingawa kwa sasa ma diktator Afrika wanaenda wanapungua Tanzania iko likely kukumbwa na janga hili kwa mara ya kwanza,Eh Mungu tuepushe na janga hili!
 
Najiuliza na kukosa majibu Mh.Lowasa si mfanyabiashara,zaidi ya kuwa mbunge,nimejionea siku za hivi karibuni katika vyombo vya habari akichangia mambo mengi hasa katika miradi ya maendeleo na katika taasisi binafsi na zamakanisa.Huyu mweshimiwa pesa anazitoa wapi?

Je alikwisha tangaza mali zake hadharani? na kipato chake kiko vipi?Alipokuwa waziri katika awamu ya tatu kwa nini akufanya hivyo?na alipokuwa waziri mkuu kwa nini alishidwa kufanya hivyo? Na kwa nini safari zake na hotuba zake zinapewa umuhimu mkubwa katika vyombo vyetu vya habari?

ROSTAM ABDULRASUL AZIZ ndo mwenyekiti wa kamati ya ushindi!! Si mnamjua kwenye siasa huyu jamaa kama Fergy kule Old traford,mlijifanya kushangilia alipojivua gamba sasa ndo mtajua kuwa mlivalisha kondom wakat mshapigwa bao kavukavu!!Rostam ni silent killer jiulizen mbona olesendeka,kilango,lembeli hamuwasikii?
 
Hapana. You have missed a point kuhusu mshikaji wako. Sio mzuri kama unavyodhani. waulize watu wa TAMISEMI hili mwanalijua vizuri sana.
Unajua ni nani alimsukia ajali aliyekuwa Municipal director wa Kinondoni na ikawezekana kumhamisha kuwa RAS Singida? Unajua kisa ni nini? unajua hili lilifanikishwa na kina nani, hadi Mkuu ya Kaya bila kujua????

Vigumu sana kulumbana na wewe . Majibu unayo wewe maswali unaniuliza mimi.
Anyways, nina uhakika alifanya yote hayo ili kuongeza ufanisi.
 
Najiuliza na kukosa majibu Mh.Lowasa si mfanyabiashara,zaidi ya kuwa mbunge,nimejionea siku za hivi karibuni katika vyombo vya habari akichangia mambo mengi hasa katika miradi ya maendeleo na katika taasisi binafsi na zamakanisa.Huyu mweshimiwa pesa anazitoa wapi?

Je alikwisha tangaza mali zake hadharani? na kipato chake kiko vipi?Alipokuwa waziri katika awamu ya tatu kwa nini akufanya hivyo?na alipokuwa waziri mkuu kwa nini alishidwa kufanya hivyo? Na kwa nini safari zake na hotuba zake zinapewa umuhimu mkubwa katika vyombo vyetu vya habari?

Kazi ya nabii Joshua hiyo.
alikuwa analipwa mil 152 kila siku kwa kodi za walala hoi.
hivyo bado anazo.
amehonga magazeti yote mpaka Mwanahalisi.
amehonga wana-harakati wote mpaka CHADEMA NA CUF.
amehonga vijana wanafanya kazi kwenye mitandao, nahofia hata wewe unaweza ukawa hapa ulipo unapima upepo tu, ukamjulishe.
KUMBUKA Lowasa ni rais wenu nyie sio Rais wa 2015 hpa Tanzania au Tanganyika yetu baada ya Katiba Mpya.
FISADI HUYO, HATUDANGANYIKI.
 
Na Nkwazi Mhango

Dira ya Mtanzania

Hakuna shaka kuwa Edward Lowassa waziri mkuu aliyetimka madarakani kutokana na kuingiza kampuni feki ya Richmond iliyoishia kuleta maafa kwa taifa, ni mtu ambaye amegeuka kuwa mkarimu hata kupita kiasi.

Hivi karibuni akiwa Kigoma akichangia shule ya Sekondari ya FPCT Bigabiro, Kigoma, alitoa mchango wa shilingi 60, 500,000 cash ukiwa ni mchango wake na marafiki zake ambao hawatajwi kwa majina. Huu si mchango mnono wa kwanza wa Lowassa hasa baada ya kuondoka madarakani. Wengi wanajiuliza: Kama ana uchungu na taifa hili kiasi cha kulitakia maendeleo na mengine mema, mbona alitumia nafasi yake kujinufaisha kwa kuingiza kampuni feki iliyoliingiza taifa kwenye zahama? Mwaka 2006 alichanga jumla ya shilingi shilingi 60, 000,000 kati ya sh 88,340,000 kwa ajili ya shule ya sekondari ya michezo ya Kigamboni. Hapa bado hatujaorodhesha michango mingine ya kuanzia shilingi 10,000,000 kwenda juu ambazo Lowassa ameishachangia kwa vituo vya yatima, kuzindua album, makanisa na mingine mingi.

Je hii pesa inayochangwa imepatikana kihalali au ni matunda ya tuhuma zake za Richmond na nyingine za zamani za marehemu baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere aliyedai mwaka 1995 kuwa Lowassa amejilimbikizia utajiri mwingi ambao hautokani na kipato halali-asioweza kuutolea maelezo ulivyopatikana. Na kweli, tangu mwalimu alirushe kimondo hicho, si Lowassa wala familia yake walikuwa tayari kuelezea walivyochuma huo utajiri!

Baada ya Lowassa kulazimishwa kuutema uwaziri mkuu, alijikuta akikabiliwa na pigo jingine takatifu. Pigo hili ni pale chama chake Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipomtuhumu kuwa gamba au mtuhumiwa mkuu wa ufisadi kiasi cha kumtaka aachie hata nyadhifa chache alizokuwa amebakia nazo. Lowassa hakukubali kutupwa nje ya uringo wa siasa hasa ikichukuliwa kuwa anatajwa tajwa kutaka eti kumrithi rais Jakaya Kikwete hapo 2015 jambo ambalo wanaojua alivyochafuka sana wanaona ni kama tusi na kejeli kwa taasisi ya urais na wananchi wa Tanzania kwa ujumla.

Ili kufanikisha azma yake hii, Lowassa, bila kujali kuwa watu wana akili za kuhoji na kuchambua, amekuwa akimwaga pesa kwa njia ya michango ili kujiweka karibu na wapiga kura akiwaaminisha kuwa anaweza kuwafaa wakati nafasi ya kufanya hivyo aliishaipoteza kwa kuitumia vibaya na kuliacha taifa kwenye zahama ya kiza na kulanguliwa umeme.

Je haya mamilioni anayotoa Lowassa yanatokana na malipo ya marupurupu ya ustaafu anayopewa kinyume cha sheria? Maana, Lowassa hakuwahi kustaafu zaidi ya kulazimishwa kuachia ngazi. Wengi wanashangaa ni kwanini Lowassa anaendelea kutanua bila kufikishwa mahakamani. Pia wengi wanashangaa jinsi CCM inavyomgwaya kiasi cha kumtishiatishia bila kumchukulia hatua. Kuko wapi kutekeleza dhana ya kujivua gamba ambako kumekuwa kukiahirishwa baada ya Lowassa kutishia kumwaga mtama? Je Lowassa kwa kukikamata mateka chama chake na serikali yake anaweza vile vile kuwakamata mateka watanzania akaishia kuwa rais wao hata kama ataingia kwenye vitabu vya historia kuwa anaweza kuwa rais mwenye kuchafuka kuliko waliowahi kumtangulia? Je watanzania ni wa hovyo kiasi hiki?

Je wanapopokea mamilioni yake wanategemea kumpa kura wakati ukifika au kuyatumia kama ushahidi kutaka aeleze aliko na alivyoyapata huku pia wakimlazimisha atoe maelezo kuhusu shutuma zake?

Wengi pia wangetaka kuwajua hao marafiki wa Lowassa wenye uchungu na taifa letu kiasi cha kumwaga mamilioni kama wameyapata kihalali au ni watu wa kuaminika au kutisha shaka. Lazima kujiridhisha isijekuwa wananchi na michango ya maendeleo vinatumika kusafishia pesa chafu itokayo kwa magenge ya watu wachafu. Hata hivyo, kwa wanaokumbuka adha alizowasababishia Lowassa kwa kubariki na kuingiza kampuni ya Richmond na hatimaye Dowans, hata awape nini hawawezi kumsamehe. Kwa wanaokumbuka ni mabilioni mangapi ya shilingi yaliteketezwa na mradi huu ambao waziri wa zamani wa Nishati na Madini Ibrahim Msabaha aliwahi kusema ni waziri mkuu yaani Lowassa na mhindi wake yaani Rostam Aziz, hawezi kupumbazwa na misaada ya mamilioni wakati wao walichuma mabilioni ukiachia mbali kuendelea kuchuma ya ustaafu wakati Lowassa hakustaafu.

Kama michango yote ambayo Lowassa ameishaitoa ingefanyiwa mahesabu, ni pesa nyingi kuliko hata mishahara yake yote ya utumishi wake serikalini. Kwa mfano mifano miwili hapo juu ya michango ya Lowassa ya shilingi 120,000,000 ni zaidi ya mshahara wa mbunge wa mwaka mzima. Hapa hajala wala kulisha familia yake kuvaa na kufanya mambo mengine. Kama Lowassa akifanyiwa ukaguzi wa kimahasibu tangu aanze kazi na marupurupu yake yote vikalinganishwa na misaada aliyowahi kutoa na mali anazomiliki itagundulika kuwa maneno ya baba wa taifa yalikuwa ya kweli. Na hivyo, yasipuuzwe wala kusahauliwa hasa wakati huu ambapo nchi inahitaji uongozi adilifu na mpya.

Tumalizie kwa kumtaka Lowassa awataje hao marafiki zake na jinsi walivyopata hayo mamilioni. Lazima tujue kama wanafanya biashara au kazi halali, wakilipa kodi na kama ni watumishi wa umma akiwamo naye na Lowassa, je wametaja mali zao kama wanavyotakiwa na sheria?

Kujua ukweli kuhusu jinsi wanavyopata pesa hii wanayotoa kwa jina jema la kusaidia jamii ni jambo jema. Lazima kila kitu kieleweke ili kuepuka jamii kugeuzwa kama fisi kulishwa nyama yake nayo ikaifakamia kwa uchoyo. Ni wakati muafaka kuangalia nani anatoa kuliko kuangalia nini kimetolewa. Hapa tuepuke cha baniani mbaya kiatu chake dawa.
 
Huyu ni journalist, anatakiwa amfuate EL na kumuuliza ana kwa ana kulikoni? anaweza akajuakila kitu deeply....hatuna waandishi wa habari wa namna hii Tanzania....wote wamebaki kuandika nakala na kubadili misamiati na kuandika kwa style tofauti.....these kind of b/shit journalism imeiua Tanzania na kudumaza bongo za wengi.

marupurupu ya serikali na fedha za richmond ndio zina mpa nguvu hivi?

yaani EL ni tajiri sana kiasi kwake mmillioni 60 kuipoteza haiumi??

kua asichokijua mwandishi kuhusu hizi changizo na hajataka kuelewa

aaargh! naenda chuo cha uandishi wa habari
 
Mkuu Waberoya, pengine ndiyo mwanzo wa mambo mengi yatakayofuata baada ya hii makala. Wote tunajua EL anavyotisha kiasi cha mtu yeyote akimwendea vibaya matokeo yake anaweza kuacha kufanya anachofanya.
 
I dont believe so, EL is strong , yes, lakini sidhani kama proffesional journalist hawezi kum-face na kumuuliza

unakumbuka alivyoita waandishi wa habari nyumbani kwake?? kuna waandishi walimuuliza kuhusu issue ya Richmond!!imagine kwa miaka zaidi ya mitatu waandishi waliandika mengi sana kuhusu ufisadi wa huyu mtu! lakini siku walipokutana naye walimuuliza kuwa 'kama wanayoyaandika ni kweli'

hauhitaji kujua mind set za magazeti yetu, waandishi wetu ...ni umbea na kuuza magazeti basi! na sisi tunanunua tukifurahia fulani kuitwa fisadi! sometime we even call these journalists ni heroes...eti haogopi!

kama EL fisadi nakala hii haimsaidii mtanzania wa kawaida, why they are not pressing government to press charge against these criminals? au kuwa mzalendo wa kweli nchi hii ni 'kubweka tu' na katu si kupigana wezi wapelekwe jela

asilolijua huyu mwandishi ni kuwa watu wa aina ya Lowassa wakialikwa huwa wanasambaza kadi kwa rafiki zake,wanachanga na baadae kwenda mahali husika ambako anawasilisha michango. si siri kuwa yeye ni tajiri na ambao wanao katika familia yake hata kabla ya kuwa kiongozi! wengine tusiojua mambo tunafahamu hivi kwa kufanya upelelezi mdogo tu.

muda umefika wa kubadili teknic zetu za kupambana na mafisadi...

magazeti yanauza tu hawako real
 
I wish he is not paving the way for 2015 presidency!
 
Back
Top Bottom