10th September 10
Sheikh Yahya aingiza ushirikina uchaguzi Mkuu
Mwandishi Wetu
Mnajimu mashuhuri wa Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein, amezua jambo kwa kuelekeza harakati za uchaguzi katika mambo ya kishirikina huku akitangaza kuwa utatawaliwa na mambo ya giza.
Mtabiri huyo alikwenda mbali zaidi kwa kutangaza kwamba atatoa ulinzi usioonekana kwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.
Sheikh Yahya alisema hayo jana kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo NIPASHE ilipata nakala yake.
Sheikh Yahya alisema kupatwa kwa jua kulikotokea Juni mwaka huu, kuliashiria mambo mengi kutokea na kuhusisha viongozi wa kisiasa na kidini hapa nchini.
Pia, alisema kupatwa huko kwa jua kuliashiria kwamba watu wengi watatumia uchawi na majini kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Kwa mujibu wa Sheikh Yahya, matukio mengine yanayotokana na kupatwa kwa jua ni kuchezeana.
Katika uzushi huo wa kishirikiana, Sheikh Yahya alioanisha kuchezeana na tukio lililompata Rais Kikwete wakati akihutubia mkutano wa kampeni Agosti 21, mwaka huu katika Viwanja vya Jangwani.
Sheikh Yahya alidai kuwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu, utatawaliwa na vitendo vya kishirikina vitakavyofanywa na wanasiasa ili kupata ushindi.
Alitabiri kuwa viongozi wa dini watatoa kauli mbaya kuhusiana na wagombea wa dini fulani au kususiana katika shughuli mbalimbali.
Alitoa mfano wa tukio kama hilo, hatua ya viongozi wa dini ya Kikristu kukataa kuhudhuria futari waliyoandaliwa na Rais Kikwete.
Hizi zote ni ishara mbaya zinazoletwa na kupatwa huko kwa jua pamoja na hayo, tunatakiwa tujihadhari sana na mambo haya kwa sababu Rais Kikwete ni Rais wa Tanzania na anahudhuria shughuli zozote za kidini... alisema.
Alisema kutokana na matukio hayo, atatoa ulinzi usionekana kwa macho, kumkinga Rais Kikwete, ili mtu yeyote asijaribu kumfanyia mchezo wowote kama ilivyotokea Jangwani.
Mtu yeyote asijaribu kumfanyia mchezo wowote kama ule wa Jangwani kwa sabababu litakalomkuta atajua mwenyewe, alionya.
Sheikh Yahya alisema katika taarifa hiyo ya ukurasa mmoja kuwa amefikia hatua hiyo kutokana na uchungu alionao kwa nchi na kwa Rais Kikwete anayempenda.
NIPASHE
Sheikh Yahya aingiza ushirikina uchaguzi Mkuu
MY TAKE:
Huyu mwanga alisema atakayempinga Kikwete atakufa sasa cha ajabu jamaa anakatakata fyuzi yaani mawasiliano sasa huu ulinzi usioonekana ndo mambo ya kumfanya msukule! asije kummaliza kabisa ohooooooo........