Elections 2010 Mh. Kikwete anaumwa nini na Ulinzi wa Sheikh Yahya

Leo nimesikia kwenye Magazeti kwamba Sheikh Yahya anadai kwamba Kuanguka Mara kwa Mara kwa Mh JK ni kutokana na Nguvu za Giza, sasa ameamua kumuongezea mheshimiwa Rais Nguvu zaidi "Zisizoonekana"

Swali langu Je JK na CCM ndiyo wameomba huo Ulinzi, Je wao wanasemaje kuhusu huo Ulinzi wa Nguvu za Giza, je Hii haina maana kwamba JK haamini Madaktari?

Too bad!
Namsikitikia sana rafiki yangu na class-mate wangu Dr. Mfisi ambaye ndio anamtibu huyu JK!
Sijui analichukuliaje suala hili, maana ni dharau ya moja kwa moja kwa fani ya tiba!... huh!
 
Kwa maana hiyo ni kuwa ulinzi aliopewa hautoshi. Mkuu wa usalama wa Taifa hafanyi kazi yake siyo hivyo amwachie ofisi Sheikh Yahya!!

.....JK anaamini zaidi ulinzi anaopewa na waganga wake kuliko wa usalama....

lakini always ole wake anayemtumainia mwanadamu .....
 
Nina rafiki yangu mmoja ni mtu wa Bagamoyo.
Yeye anaamini sana ulinzi wa dizaini hiyo kuliko hata madaktari.
Nadhani kuna kitu common kwa watu wa Bagamoyo.
 
kuna mwana psychologia mmoja aliwahi kuniambia kadri unavyoongelea ugonjwa wa mtu mbele yake ndivyo mgojwa huyo anavyozidi kuzidiwa. Kwa hiyo shekhe yahya kuongelea hali ya kikwete public amezidi kumtonesha na kumsononesha zaidi. Nafikiri hata yeye kikwete na viongozi wa ccm wenye akili timamu ukiacha makamba hawatafurahia kitendo hiki, ni punguani tu atakayeshabikia hili.

makamba na riziwani.........
 
Leo nilikuwa nasikiliza radio maria asubuhi kipindi cha magazeti shekh yahaya alisema kikwete haumwi na amemweka ulinzi wa ziada ambao hauonekani jaman nchi inaongoza na mungu kwel ah Tanzania
 
....... Alisema kutokana na matukio hayo, atatoa ulinzi usionekana kwa macho, kumkinga Rais Kikwete, ili mtu yeyote asijaribu kumfanyia mchezo wowote kama ilivyotokea Jangwani.
“Mtu yeyote asijaribu kumfanyia mchezo wowote kama ule wa Jangwani kwa sabababu litakalomkuta atajua mwenyewe,” alionya.
Sheikh Yahya alisema katika taarifa hiyo ya ukurasa mmoja kuwa amefikia hatua hiyo kutokana na uchungu alionao kwa nchi na kwa Rais Kikwete anayempenda.
CHANZO: NIPASHE

Niatia kinyaa na aibu kubwa sana kwa Taifa.
Huyu Jamaa (Kikwete Hafai kabisa), atawekaje mambo ya kishirikina kwenye kuongoza Taifa?
Sheikh Yahaya haweze kusema tu, kunaonyesha kuwa na mawasilianao na hata Kikwete kwenda kwenye RAMLI ndio mana mtu na akili zake anasema Kikwete alianguka sababu za kishirikina.
JE NDUGU WATANZANIA TUKO TAYARI KUONGOZWA NA VIONGOZI KAMA HAWA?
 
God's Second Commandment forbids the worship of the true God by images or similitude, God has declared such worship to be sin:
.

"Thou shalt not make unto thee any graven image, or any likeness of anything that is in heaven above, or that is in the earth beneath, or that is in the water under the earth: thou shalt not bow down thyself to them, nor serve them. "
 
....... Alisema kutokana na matukio hayo, atatoa ulinzi usionekana kwa macho, kumkinga Rais Kikwete, ili mtu yeyote asijaribu kumfanyia mchezo wowote kama ilivyotokea Jangwani.
“Mtu yeyote asijaribu kumfanyia mchezo wowote kama ule wa Jangwani kwa sabababu litakalomkuta atajua mwenyewe,” alionya.
Sheikh Yahya alisema katika taarifa hiyo ya ukurasa mmoja kuwa amefikia hatua hiyo kutokana na uchungu alionao kwa nchi na kwa Rais Kikwete anayempenda.
CHANZO: NIPASHE

MWONGO SANA HUYU KIGAGURA!
ALIKUWA WAPI SIKU mKULU anabwagwa chiNI hadi anajifanya kustuka saa hizi?
Kwanza usikute ni yeye mwenyewe alisababisha ili atafutwe kutoa tiba, na kuongeza zindiko!...huh!
 
10th September 10
Sheikh Yahya aingiza ushirikina uchaguzi Mkuu

Mwandishi Wetu

Mnajimu mashuhuri wa Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein, amezua jambo kwa kuelekeza harakati za uchaguzi katika mambo ya kishirikina huku akitangaza kuwa utatawaliwa na mambo ya giza.
Mtabiri huyo alikwenda mbali zaidi kwa kutangaza kwamba atatoa ulinzi usioonekana kwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete.
Sheikh Yahya alisema hayo jana kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo NIPASHE ilipata nakala yake.
Sheikh Yahya alisema kupatwa kwa jua kulikotokea Juni mwaka huu, kuliashiria mambo mengi kutokea na kuhusisha viongozi wa kisiasa na kidini hapa nchini.
Pia, alisema kupatwa huko kwa jua kuliashiria kwamba watu wengi watatumia uchawi na majini kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Kwa mujibu wa Sheikh Yahya, matukio mengine yanayotokana na kupatwa kwa jua ni kuchezeana.
Katika uzushi huo wa kishirikiana, Sheikh Yahya alioanisha “kuchezeana” na tukio lililompata Rais Kikwete wakati akihutubia mkutano wa kampeni Agosti 21, mwaka huu katika Viwanja vya Jangwani.
Sheikh Yahya alidai kuwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu, utatawaliwa na vitendo vya kishirikina vitakavyofanywa na wanasiasa ili kupata ushindi.
Alitabiri kuwa viongozi wa dini watatoa kauli mbaya kuhusiana na wagombea wa dini fulani au kususiana katika shughuli mbalimbali.
Alitoa mfano wa tukio kama hilo, hatua ya viongozi wa dini ya Kikristu kukataa kuhudhuria futari waliyoandaliwa na Rais Kikwete.
“Hizi zote ni ishara mbaya zinazoletwa na kupatwa huko kwa jua pamoja na hayo, tunatakiwa tujihadhari sana na mambo haya kwa sababu Rais Kikwete ni Rais wa Tanzania na anahudhuria shughuli zozote za kidini...” alisema.
Alisema kutokana na matukio hayo, atatoa ulinzi usionekana kwa macho, kumkinga Rais Kikwete, ili mtu yeyote asijaribu kumfanyia mchezo wowote kama ilivyotokea Jangwani.
“Mtu yeyote asijaribu kumfanyia mchezo wowote kama ule wa Jangwani kwa sabababu litakalomkuta atajua mwenyewe,” alionya.
Sheikh Yahya alisema katika taarifa hiyo ya ukurasa mmoja kuwa amefikia hatua hiyo kutokana na uchungu alionao kwa nchi na kwa Rais Kikwete anayempenda.

NIPASHE

Sheikh Yahya aingiza ushirikina uchaguzi Mkuu
MY TAKE:
Huyu mwanga alisema atakayempinga Kikwete atakufa sasa cha ajabu jamaa anakatakata fyuzi yaani mawasiliano sasa huu ulinzi usioonekana ndo mambo ya kumfanya msukule! asije kummaliza kabisa ohooooooo........
 
Kweli Tanzania imekosa mwelekeo. Tusubiri tamko la CCM kuhusiana na kauli ya mkurugenzi wa unajimu wa Ikulu
 
Tutamsikia Salva akisema tuheshimu maoni ya huyo shehe Yahaya. Kazi kweli kweli nchi hii.
 
Kitendo cha Yahya kusema kwamba ataongeza ulinzi wa Jk, kinanipa mshangao kwamba hili taifa linaongozwa na waganga wa kienyeji nyuma ya pazia. Kumbe ndio maana mambo hayaendi.
 
Unategemea niño Kama nchi inakuwa na rais anayependa kuaamni uchawi obvious lazima afanye mambo kwa maelekezo ya waganga wa kienyeji
 
Leo nimesikia kwenye Magazeti kwamba Sheikh Yahya anadai kwamba Kuanguka Mara kwa Mara kwa Mh JK ni kutokana na Nguvu za Giza, sasa ameamua kumuongezea mheshimiwa Rais Nguvu zaidi "Zisizoonekana"

Swali langu Je JK na CCM ndiyo wameomba huo Ulinzi, Je wao wanasemaje kuhusu huo Ulinzi wa Nguvu za Giza, je Hii haina maana kwamba JK haamini Madaktari?
nafikiri anaamini madaktari wake, sema hapo ameaply maagizo ya imani kidini kujiunga na nguvu za kijini na kipepo ili viweze kumsaidia, shekhe yahya analijua hilo, ilimu ahera ndiyo inafanya kazi
 
Ukiangalia misafara yote ya Kikwete ndani na nje ya nchi huwa kuna walozi!
 
Too bad!
Namsikitikia sana rafiki yangu na class-mate wangu Dr. Mfisi ambaye ndio anamtibu huyu JK!
Sijui analichukuliaje suala hili, maana ni dharau ya moja kwa moja kwa fani ya tiba!... huh!

Magonjwa mengine hayana tiba wala kinga jamani!
 
Kuna mstari umeandikwa kwenye biblia ila nimesahau uko wapi ila maneno yako yanasema kitu kama hiki:

".......Kama nyumba/Mji haulindwi na Bwana, walindao wanafanya kazi bure."

Heri basi walau angelianza kuwa mcha Mungu wa kweli. Haya majini hayamfikishi popote.

Utatafuta wachawi wee kumbe wachawi unao hapohapo wamekuzunguka akina Rostam, Lowassa, And all Mafisadi.
 
Duh! Ila tumefikia mahali pabaya kama taifa: kutegemea ushirikina katika kuongoza nchi. Huyu mzee inafaa akemewe. Vinginevo kama kweli mheshimiwa anamwamini basi amejiweka bapaya sana: kwani si ajabu kila atakachoamuru kama sharti la zindiko lake litakubaliwa. Na hii hi hatari. Je, kwa mfano akisema anahitaji ngozi ya mtu au kiungo chochote ili atimize shughuli yake ya "ulinzi"/zindiko, atakataliwa?? Kujiweka chini ya waganga wa kienyeji ni kuhatarisha usalama wa raia na nchi kwa ujumla. Huyu mzee akemewe kwa ukali.
 
Sheikh Yahya aingiza ushirikina uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi wetu

10th September 2010

Sheikh%20Yahya%20Hussein,%284%29.jpg

Back
Top Bottom