Elections 2010 Mh. Kikwete anaumwa nini na Ulinzi wa Sheikh Yahya

Elections 2010 Mh. Kikwete anaumwa nini na Ulinzi wa Sheikh Yahya

(Perhaps you) and me know very well kuwa ushirikina haufanyi kazi...Huyo shehe mwenyewe analijua hilo am sure.
This is another deliberately timed move (ikitanguliwa na ile ya maisha binafsi ya Dr Slaa kupitia media houses za govt) ya JK & co kui-divert electorate (na hata Slaa & co wenyewe) kutoka kwenye issues.
Dr Slaa awe careful not be drawn into such cheap stuff - nimekuwa saddened kidogo kwamba ame-react against comments za kichawi za sheke Yahaya.
Namshauri kazi hii awaachie akina Marando & co, wakati yeye akiendelea kuchanja mbuga kuhubiri issues.
 
nasikitika mpaka sasa JK amkaa kimya, hii inaonyesha anakubaliana na ofa aliyopewa na mnajimu
 
mie nikuuluzeni mungu gani anaekuwa na mzinzi?

unajua biblia imakataza sana uzinzi

na inamini familia na jamii bora ni ile watu waliooana na sio kukamatana wakazaa(kama alivyofanya Dr slaa kwa mwanamke wa kwanza), kuchochea kuvunjika ndoa za wengine kwa kuwaibia wake/waume zao

na tunapotafuta rais moja ya kazi yake ni kujenga jamii yenye maadili, ambayo hii ndio itakuwa na uelewa na uwezo wa kujenga uchumi ulio imara

itawezekanaje taifa linaloongozwa na mzinzi na aliefeli maadili kutufikisha hapo?

Hahahahaaaaaaa, duh kweli jamaa mzinzi, HEBU ANZA BASI KUMRUSHIA JIWE kwani weye ni msafi sana!
 
He bothers you for sure, but he spoke a point! A nation 'd not be governed by metaphysics and Superstition! I am sure this current president is doing a lot of Horoscope before doing anything, that is why our country is here now! Uswahiliiiiiiiiiiii!!!!!!!

Ndo maana alizimia jukwaani, Mwajua Michael Jackson alifariki kwa sababu ya kuzidisha DOZI za madawa mchanganyiko, sasa huyo mtanzania mwenzetu akiongeza tena DOZI ya shekh Yahya tunaweza kumpoteza kwani "concentration" itaaongezeka!!
 
Nimshukuru Ndg Njiwa kwa kunukua sehemu mbalimbali ndani ya Quoran ambazo zimejibu swali la mtoa mada na kudhihirisha JK sio mwislamu safi, nimeipenda hii nukuu, nyingine zipo katika posting ya Njiwa:
"...black magic in Islam, is totally prohibited and must be kept away at all time. A person is not in any condition is permitted to use the black magic to help overcome his/her nessesities. In Islam, a person is a mushrik or a polytheistic if he is engaged in Black magic. The Prophet (peace and blessings be upon him) said, "Whoever blows on knots practices magic, and whoever practices magic is a mushrik (polytheist)."
 
Sheikh%20Yahya%20Hussein,(6).jpg

Mnajimu Sheikh Yahya Hussein.

Serikali imesema haihusiki na hoja ya ulinzi usioonekana kwa Rais Jakaya Kikwete, kama ilivyotangazwa juzi na Mnajimu Sheikh Yahaya Hussein.
Juzi Sheikh Yahya alitoa taarifa ambayo pamoja na mambo mengine, aliahidi kumpatia Rais Kikwete ulinzi usioonekana.
Kwa mujibu wa Sheikh Yahya, ulinzi huo utawezesha kumkinga Rais Kikwete dhidi ya wabaya wake hasa wanaotumia majini na kuchezeana.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, alipoulizwa kuhusu kauli ya Sheikh Yahaya, aling'aka na kusema serikali haihusiki.
"Hatuhusiki na ulinzi wa aina hiyo, siyo mimi niliyetoa taarifa hiyo...sikukuu njema na kwa heri,"alisema kwa ufupi na kukata simu.
NIPASHE iliwasiliana na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi, ambaye alikataa kuzungumzia hoja hiyo.
Dk Mwinyi alisema wizara yake haihusiki na masuala ya ulinzi wa Rais, hivyo hawezi kutoa maoni yake.
"Mwandishi tunaulizana maswali ya aina gani bwana, wizara yangu inahusika na ulinzi wa mipaka bwana, hilo la Rais watafute wahusika," alisema.
Aidha NIPASHE ilipowasiliana na mwanasiasa wa mkongwe, Samuel Malecela, kujua maoni yake juu ya taarifa ya Sheikh Yahya, alipokea simu, lakini baada ya mwandishi kujitambulisha alikata.
Jitihada za kumpigia simu kwa mara nyingine zilishindikana kutokana na simu yake ya kiganjani kuita pasipo kupokewa.
Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na Mwenyekiti wa kampeni za Rais Kikwete, Abdulrahman Kinana, hawakupatikana kuzungumzia kuanguka kwa Rais Kikwete wakati akihutubia Jangwani Agosti 21, mwaka huu, kwamba ilisabaishwa na uchawi na majini.
Hoja hiyo ni miongoni mwa mambo yaliyotajwa katika taarifa ya Sheikh Yahya juzi na kukaririwa kwenye vyombo vya habari jana.
Pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (utawala bora) hakupatikana kutoa maoni yake kuhusu ulinzi wa Rais Kikwete usiionekana.
Sheikh Yahya alihusisha kupatwa kwa jua kulikotokea Juni mwaka huu, kama kiashiria muhimu cha harakati za uchaguzi kutawaliwa na mambo ya nguvu za giza yakiwahusisha viongozi wa kisiasa na kidini.

Source: NIPASHE.
 
Shehe Yahya Hussein halindi Serikali, na amekua akimlinda JK Kikwete tangu siku nyingi tu, anasema atamuongezea nguvu.
hajasema atailinda serikali, hayo ni makubaliano ya Shehe Yahya na Kikwete, wanakutana wapi na vipi wanajuana.ila lililowazi ni kua JK amepokea huduma hiyo, ni yeye mwenyewe wakukanusha, kukubali na kumkana mtu huyo.
lakini wana urafiki wa karibu hawa, nasikia JK aliwahi hata kumpeleka mganga wake hospitali nje ya nchi kwa ukaribu wao.
 
mimi naamini anataka umaarufu tu. lkn hana uwezo wa kumlinda mtu.

anaishi kwa uganga, anamiliki mali nyingi kwa uganga, kwa wakazi wa magomeni watakupa ushuhuda.
huyu mtu shehe Yahya hatibu watu mafukara, hatoi tiba kwa masikini, anatibu matajiri, wanasiasa, anaagua watu wanataka bahati, nyota za mafanikio, na hirizi yake kuubwa ni mapete pete fulani hivi.
anamaanisha, na anarudia kusema haya kwa style nyingine baada ya kipindi kirefu. Ikulu inahusishwa na ushirikina, aibu sana.
 
Shehe Yahya Hussein halindi Serikali, na amekua akimlinda JK Kikwete tangu siku nyingi tu, anasema atamuongezea nguvu.
hajasema atailinda serikali, hayo ni makubaliano ya Shehe Yahya na Kikwete, wanakutana wapi na vipi wanajuana.ila lililowazi ni kua JK amepokea huduma hiyo, ni yeye mwenyewe wakukanusha, kukubali na kumkana mtu huyo.
lakini wana urafiki wa karibu hawa, nasikia JK aliwahi hata kumpeleka mganga wake hospitali nje ya nchi kwa ukaribu wao.
Hapo kwenye bluu unakosea..

Kama ni mambo personal kwanini Kigagura huyo ameyaweka sasa kuwa ya jamii nzima ya Watanzania?...kwanini asibaki kwenye agreement ya kwanza ya usiri, maana nadhani walipatania sirini tusikopajua!...Kutangaza hadharani tayari kunalifanya Taifa listuke!...

Mbinu za kishetani huwa hazina muda mrefu, na hazijitoshelezi!...utafanya hiki, utakuta bado kina mapungufu!..mwishowe ishu imemwagika hadharani...

Mimi nasema ..Ni AIBU tupu!
 
huyu mzee wa majini Yahya Hussein , kajisahau, kajikuta karopoka, sasa maji yamemwagika , siri iko nje.
hakika ni aibu sana.
 
Basi itakuwa ni TLP kama CHADEMA haihusiki kumchafua JK kutumia waganga wa kienyeji

Mbona unatoa hoja zilizojaa hisia? Haya tuambie ni kwa namna gani TLP au CHADEMA inahusika! JK mwenyewe hajakanusha suala hilo wewe umekimbilia kumtetea!
 
Mbona unatoa hoja zilizojaa hisia? Haya tuambie ni kwa namna gani TLP au CHADEMA inahusika! JK mwenyewe hajakanusha suala hilo wewe umekimbilia kumtetea!

Sijamtetea ila nimetumia logic ya kawaida tu, kama mume akidai haki zake kwa kuibiwa na kudhalilishwa kwa kuibiwa mkewe ni mbinu ya CCM kumchafua Slaa basi inawezekana pia Mchawi kujihusisha na JK ni mbinu ya CHADEMA kumchafua JK.
 
Kama nilivyosema ni hisia! Kwa bahati mbaya mfano wako sio logical kama unavyodai! Kwa upande wa wanayedai mchumba wa Dkt Slaa alionekana naye na wanadai kwamba alimtambulisha kwamba ni mchumba wake, kisha mume wa zamani amepeleka kesi Mahakama Kuu! Kwa upande wa Sheikh Yahya amedai kwamba atatoa "ulinzi usioonekana" kwa JK! Ulinzi huo hajaenda kuutafuta kwenye Ofisi za CHADEMA au TLP, pia hajataja CHADEMA/TLP popote!
Kauli za Sheikh Yahya pia hazijaanza leo. Kuna wakati alidai kwamba atakayepambana na JK kwenye uchaguzi atakufa! Sasa kwa kauli hiyo nako utadai ametumiwa na CHADEMA/TLP?
 
Kwa nini una wa undermine CHADEMA kiasi hicho? unadhani ni CCM peke yao ndio wana uwezo wa ku play dirty?
 
Back
Top Bottom