Nakuk bin laaden
Member
- Aug 29, 2013
- 37
- 3
siasa kama za akina Mwigulu Nchemba zinahitajika sana hapa tanzania
kwa hiyo huko marekani na uk amekwend kutengeneza chama au kuomba msaada..na kwa bahati mbaya atapata msaada wowote
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
siasa kama za akina Mwigulu Nchemba zinahitajika sana hapa tanzania
siasa kama za akina Mwigulu Nchemba zinahitajika sana hapa tanzania
MWIGULU NCHEMBA APASUA ANGA KIMATAIFA,SASA KUTIKISA MAREKANI NA UINGEREZA ZAIDI YA MWEZI MMOJA ---KUIMARISHA CCM KIMATAIFA,KUZUNGUMZA NA WATANZANIA KWENYE MATAIFA HAYO MAKUBWA DUNIANI.
CHADEMA WAWEWESEKA,YEYE AAHIDI KUKAZA KAMBA MWANZO MWISHO NDANI NA NJE YA NCHI.Ni kweli,ni uhakika,ni dalili za wazi kuwa Mh.Mwigulu Nchemba sasa hakamatiki,ni moto wa kuotea mbali katika siasa za nchi hii.Akabidhiwa beji ya kuimarisha chama kimataifa.Camera yetu imenasa habari za uhakika kuwa ,Mbunge wa Iramba Mgharibi na Naibu katibu Mkuu wa CCM-TANZANIA BARA Mh.Mwigulu Nchemba anaanza rasmi ziara yake ya kikazi,ziara ya kujenga na kuimarisha chama cha mapinduzi kimataifa,Ziara ya kuzungumza na vyama rafiki wa CCM ndani ya Marekani na Uingereza, ziara ya kuzungumza na watanzania kule kule waliko MAREKANI NA UINGEREZA.
![]()
Mwigulu Nchemba anategema kuanza ziara yake siku ya kesho katika majimbo mbali mbali ndani ya Marekani na baadae kuelekea Uingereza katika miji ya West London,Birmigham,Reading Na Manchester kwa kazi maalum zifuatazo.
1.Mbunge huyo mwiba mkali kwa CHADEMA anategemea kuzunguka zaidi ya Mwezi Mzima Marekani na uingereza kufungua matawi mbalimbali na kuzungumza na wanachama wa CCM Katika Mataifa hayo makubwa mawili Duniani.
2.Pia Mh.Mwigulu Nchemba anategema kwenda kukutana na viongozi wa juu wa vyama vikubwa na vikongwe vya mataifa hayo mawili,Vyama rafiki vya CCM ndani ya Marekani na Uingereza.Hii ni fusa ambayo itatumika kujenga uimara wa CCM kidiplomasia hasa kwenye siasa za kimataifa.
3.Mbunge huyo anategemea kushiriki mkutano wa UN unaotegemea kufanyika mwishoni mwa Mwezi huu ndani ya WASHINGTON D.C (Hapa anategemea kupata uzoefu wa kukaa na kujadili mambo na mataifa makubwa duniani na viongozi wenye beji za heshima mbalimbali katika ulimwengu huu).
4.Pia Mh.Mwigulu Nchemba anategemea kuzungumza na watanzania karibia wote wanaoishi ndani ya nchi hizo mbili.Katika mambo muhimu anayokwenda kuzungumza ni pamoja na Katiba mpya,Maendeleo ya kiuchumi ndani ya Taifa letu,ajira,Amani na mwenendo wa siasa ndani na nje ya Tanzania.Pia anakwenda kujadiliana na watanzania maisha yao nje ya nchi na changamoto wanazokutana nazo.Kubwa zaidi anakwenda kuzungumza uimara wa CCM na uhakika wa kuendelea kuongoza nchi na namna watakavyobwaga upinzani kwenye uchaguzi ujao kwa sababu Upinzani Watanzania haujitambui,hawana malengo,ni vyama vyenye ubinafsi na ufamilia ndani yake hivyo havifai kupewa nchi.
KUWEWESEKA KWA CHADEMA,Paparazi wetu amenasa tetesi kuwa Viongozi wa juu wa CHADEMA wamesikia Taarifa za Mwigulu Nchemba kutua Marekani na Uingereza,jambo hilo linaonekana kuwapa wakati mgumu sana viongozi wa CHADEMA na kupelekea kufanya vikao vya ghafla vya hapa na pale na kufikia maamuzi ya kumwmbia Dr.slaa naye afunge ziara kwenda marekani siku tatu akajaribu kujibu mapigo ya Mh.Mwigulu Nchemba.
Kuweweseka huku kwa CHADEMA si mara ya kwanza,kila mmoja anakumbuka kuwa Mh.Mwigulu Nchemba aliporejea kutoka china baada ya kukutana na viongozi wa juu wa kikomunisti wa nchi ile,CHADEMA waliloa jasho,wamekuwa wakilia kila siku kuwa Mwigulu anawadhoofisha kisiasa na wamekuwa wakisema alikwenda china kwa lengo maalumu la kujifunza siasa za kisayansi.JE MWIGULU NCHEMBA AKIREJEA KUTOKA MAREKANI NA UINGEREZA CHADEMA MTAPONA KWELI???Mziki wa China tu imewafanya chadema wachuje kiasi kwamba inaonekana sio chama cha upinzani tena.Hii yote ni kazi ya mikono ya Mh.Mwigulu NChemba kuhakikisha upinzani hawafui dafu mbele ya CCM na kweli imewezekana.Je ikirejea kutoka ziara ya Marekani tutegemee nini kama sio kifo cha chadema ama kusambaratika kabisa???Duru za habari zainaonesha wazi kuwa Mh.Mwigulu Nchemba ndiye kijana anayeandaliwa na watu wakubwa wanchi hii kuchukua nafasi ya Urais,Rejea kauli ya JK kuwa nchi hii hatamuachi mtu Mzee.BASI kaaa ukijua kuwa Mh.Mwigulu Nchemba anaandaliwa kiti cha kugombea Urais,na vijana wa CCM wanasubiria kwa hamu sana kuona Mbunge huyo anatajwa kuwa ndiye atapeperusha bendera ya CCM kwenye kiti cha Urais.![]()
Hii ya Urais inaonekana kuwa mwiba sana Kwa CHADEMA kutokana na namna wanavyomuogopa Mbunge huyu,iwapo yeye ni mbunge tu amewashinda kisiasa kiasi hiki,Je akiwa Rais wanchi tutegemee kuiona chadema tena??Tusubiri macho yetu tu kuona chadema na vyama vya upinzani vikitafuta njia mbalimbali za kukimbilia.
Nilipojaribu kumtafuta Mh.Mwigulu Nchemba kuhusiana na ziara hii kama ni kwelu au la!!akaniambia Ni kweli naeleka kikazi zaidi huko Marekani na Uingereza,napeperusha bendera ya nchi yangu na chama changu kimataifa,Nakwenda kukutana na viongozi mbalimbali wa vyama rafiki na CCM,nakwenda kuzungumza na Watanzania wenzangu,nakwenda kuimarisha chama na kufungua matawi ya CCM huko nje ya nchi,Nimezaliwa kwaajili ya kulitumikia Taifa langu na chama change CCM,Na furaha yangu ni kuona wale ninaopambana nao kwenye siasa wanakasirika kila siku kwani ni ishara ya wazi kuwa nawapiga kisawasawa na nitaendelea kufanya hivyo bila kukata tamaa. alidokeza.
MY TAKE ::Mh.Mwigulu Nchemba anaziwezea sana siasa za nchi hii,na swaga zake za kijamaa Chegua Vara,Fidel Castro n.k atafika mbali sana.Na kwa Taifa hili lenye vyama vibovu vya upinzani tunahitaji mtu wa aina ya Mh.Mwigulu Nchemba.Huyu mbunge hana cha kulaza damu,yeye ni kazi kazi,ni MORINGE SOKOINE MWINGINE NDANI YA TAIFA LETU.![]()
ASANTE.
VIVA Mwengulu, Viva Sii Sii Eeeeem, Ukirudi uwasaidie CDM kwenda kujisajili upya. Ama kweli si lazima uokote makopo ndipo tukupeleke Mirembe. Ukiwaza kwa kupiga kelele tunaweza pia kukupeleka huko. Kama unapiga yowe kuwa unaenda kuiba na unapitia Police Central lazima wakukamate.
Si, Nape kasema CDM walipewa mchango wa mshiko kuja kuharibu mchakato wa katiba na nchi hizo hizo anakoenda Mchemba jamani au nilisikia vibaya?
Mwingulu, sema unataka kutakatisha fedha flani flani ulizoleta China juzi kati hapa. Ukianza kuzimwaga useme ulipewa Marekani na UK. Sawa mkuu tumekusikia, tumeona matangazo yako kuwa unasafiri kwa wakubwa huko kuomba msaada wa kuibomoa na kuiteketeza kabisa CDM. Sisi CDM hatutishwi na fedha haramu ambazo ni lazima zikatakatishwe kwa safari ya USA na UK.
Ati kiboko ya CDM, naona huyo ndiye aliyeandaliwa na Mungu kuimaliza kabisa CCM. Just mark ma words. Mlianza kushambulia kuwa CDM wamepewa fedha nyingi sana huko ugaibuni ili nyie mpate huu mlango wa kutakatishia hizo fedha haramu lakini tunalijua hilo. Akirudi na neti za mbu za matundu makubwa sawa. Huo ndio msaada mnaoweza kupewa huko. Lakini akirudi na uwezo mkubwa kifedha, twajua hiyo ni Janja tuuu.
Mataifa hayo wameshajua moto wa CDM. Haufunikikiiiiiii. 2015 inavyozidi kukaribia mtaweweseka saana tu.
Duuuuu,bado tupo katika nyakati za giza,inawezekana kweli kwa CCM?Jamaa hana hata sifa moja ya kuwa rais,Ni mfumo wetu mbovu ndio unaomlinda tu,vinginevyo......ndio maana anaongoa mambo makubwa na kutuhumu watu lakini jeshi la polisi wanogopa ata kumuoji tu?Alisema anao ushahidi wa mlipuko wa bomu katika mkutano wa chadema Arusha,lakini mpaka leo polisi awaja......na hakuna kinachoendelea.MUNGU ibariki TANZANIA
Juliana Shonza naona waendelea kutetea mkate wako wa kila siku.... Hapo cha ajabu kipi?? Kwenda US na UK?? Mfyuuuuu...... Halafu kuna mtu Mzima jana anaponda Dr Slaa kwenda Marekani william j. Malecela..... Kwa Mwigulu Nchemba kwenda Marekani na UK hili nalo utaliponda?? Au kwa vile ni CCM sawa??viva CCM,VIVA MWIGULU NCHEMBA
Wenye schedule ya hii ziara please weka hapa JF. Mh Mwigulu tunakusubiri Washington DC, Jiandae sana, maana tunajiandaa watu wenye uchungu na Tanganyika tuje na maswali mengi na magumu. Muungano wa serikali tatu, kuhusu mauaji au ushirika wako katika Ugaidi na Kauli yako uliyoitoa kuhusu Membe na Lowasa. Remember, kila kitu kitakuwa kwa Kiingereza na will be recorded ili tuweke katika Youtube. We' re going to push all your buttons and No body will help you there. If you put your hands on anybody, you'll be arrested. Take this as friendly advice