Mh, Rais ikikupenda ndugu Robert Heriel Mtibeli , mtazame anakufaa katika kazi zako

Mh, Rais ikikupenda ndugu Robert Heriel Mtibeli , mtazame anakufaa katika kazi zako

Watibeli ni watu wenye misimamo, sidhani kama "atafaa" japo yupo vizuri.
 
Kama mama amekufikia kuna sababu gani ya kuja kuweka bango huku jukwaani ?
 
Watu wa vetting waangalie muda ana opost mada zake, mara nyingi ni usiku akiwa amelewa. Angepata hata kazi ya ulinzi wa geti, ila pombe sasa, msafara wa president ukiingia unamkuta kalala au kile kirungu kapeleka nyumbani akakipikie kama kuni. Hata kama mnataka akafie jela, lakini sio kwa staili hii
 
Wana-Ccm wenzangu ndugu Robert Heriel Mtibeli , mfikirieni kumteua .

Kijana huyu anatufaa katika Serikali , Elimu yake ni Shahada .

Umri 30s

Atatufaa katika kutuandikia hotuba , n.k

Asante

Hii inaweza kuhesabiwa kama;
1. Uchokozi na uchokonozi
2. Heshima ikiwa mwandishi ameandika kwa dhamiri ya kweli.
3. Kupima upepo kujua Mtibeli anakubalika kiasi gani na kujua wenye roho za chuki dhidi yake. Ingawaje sio wote watashindwa kujizuia kuonyesha hisia na Maoni hayo ya Chuki dhidi ya mtajwa.

4. Kuonyesha mitazamo ya wanaJF dhidi ya Mtajwa, wanamchukuliaje bila kujali wanampenda au hawampendi.

Mtoa Mada, nakushukuru kwa kuniwaza na kunipa heshima ya kipekee kwa kuniona nina uwezo wa kiwango ambacho ninaweza Kufikiriwa na mtu mwenye cheo cha Urais. Huu kwangu ni heshima ingawaje unaweza kuchukuliwa kwa namna hasi.

Kwa ambao wameonyesha hisia zao za kuniponda na kuhisi ninajipigia Promo. Nawapongeza pia kwa maoni yao na uhuru wao kama ulivyofanya mtoa Mada.
Sisi Watibeli tunatambua Uhuru wa maoni na kuchagua. Hatutaki kupendwa na kila mtu kwani hakuna huo ulazima na hakuna tija ya kupendwa na kila mtu.

Pili, Watibeli hatufanyi mambo ili kutafuta Favour ya mtu yeyote ikiwemo Rais au mtu yeyote. So wale wenye mitazamo ya aina hiyo wasituhusishe na tabia na tamaduni zao. Tunafanya yale tunayojisikia kufanya bila kujali yoyote nasisitiza bila kujali yoyote atachukuliaje na atapenda au hatapenda. Kumaanisha hatuhitaji kubwa impress au kutaka validation kwa watu wengine kwani hiyo haituhusu.

Tatu, sisi hatuwezi kujitangaza wala kujipa Promo kwa sababu sisi wenyewe tunamajina makubwa na uwezo unaotosha na majina yetu yapo kwa Wakuu na watu wenye nafasi. So hatuhitaji huruma wala kufikiriwa fikiriwa. Muda kwetu ndio Muamuzi na kwa wasiojua tayari tunatumikia nchi kwa namna nyingi tuu.

Mwisho, Nafurahi kuona mtu akichukua muda wake kuandika kile anachotamani katika Maisha yangu kitokee. Hii ni muujiza na baraka kubwa sana kwangu. Tena kutamka hadharani ni jambo kubwa sana kwangu. Ni heshima. Fikiria mtu ana ndugu, jamaa na marafiki hajapendekeza waonwe na Rais anakuwaza wewe, hiyo kama sio heshima ni kitu gani. Mimi nashukuru sana Mkuu.

Ubarikiwe.
 
Kumbe mkishajifanya washauri wa maisha ya watu humu ndani ,hata nyie hamna kazi za kufanya mpaka mpate uteuzi😂😂.

Rudi Kwenu Kilimanjaro ukalime ,Dar pagumu endelea kuandika stori zako ipo siku utachoka.
 
Ili mradi familia yako ikae hadi msalani kwa vile vyoo vya kukaa
Huku familia zetu zikifanya mazoezi hadi msalani kwa kuinuka gogo likidondoka na kushuka anapolisukuma kwakuwa choo kimejaa
 

😀😀
Mkuu katika Maisha yako kuna mambo huwezi kuyazuia yanayohusu watu;
1. Huwezi kuzuia watu kufikiri
2. Huwezi kuzuia watu kusema kulingana na mitazamo, maoni na uelewa wao.

Kwa sisi watibeli kujua hilo hatujishughulishi na kile mtu/watu wanachowaza juu yetu, au wanachosema juu yetu. Na hiyo sio sisi tuu bali ni kanuni za kisaikolojia na kisosholojia.

Mtu kaamua kutoa maoni yake vile anavyohisi na kuniona kama mtu mwenye uwezo wa kuteuliwa na Rais. Siwezi kumpinga kwa uwezo wake na mawazo yake.
Halikadhalika siwezi kumpinga mtu mwingine atakayeona sifai kwa sababu ya maoni na uwezo wake vile anavyonitafsiri.

Huo ni utibeli.
Kusimamia Haki, kwamba kila mtu anahaki ya kutoa maoni kulingana na uelewa na uwezo wake.
Ukweli, kukubali ukweli kuwa watu hawafanani Uelewa, mtizamo na uwezo.
Upendo, kuishi kwa kuvumiliana na kupendana kwa kujua kubwa kila mtu ni muhimu bila kujali nafasi, uwezo na alivyo.
Akili, kuishi kwa kutatua matatizo yanayotuzunguka ili kufanya maisha yawe bora.
 
Back
Top Bottom