Mh. Rais, kwani mkopo wa madaktari ni wa bure hawalipi?

Inanikumbusha story ya mzaire mmoja alimpeleka mtoto wa dada yake ya London.

Kufika huko dogo akaanza kujichanganya na watoto wengine wa kizaire waliozaliwa kule na kuanza tabia za ajabu ajabu.

Uncle akamuweka chini wewe nimekupeleka huko usome, ufanye kazi usaidie familia yako hao jamaa achana nao wazazi wako ulaya.

Dogo akajibu umekuwa unanipangia sana namna ya kuishi tangia unifikishe huko, kama vipi nikulipe hela yako.

Mjomba wake akamwambia mimi sina shida na hela yako, kama nilichofanya rahisi wewe si una wadogo zako vuta mmoja tu London, halafu akifika umchoree mchongo kama nilivyokufanyia apate papers za kuishi utakuwa umenilipa. Dogo ilibidi aombe msamaha.

Ndio watu kama nyie mnaona kazi iliyofanywa na serikali ni rahisi sana, kisa hao watu sasa hivi wanauwezo wa kulipa madeni yao.

Ebu kila daktari asomeshe mmoja tu kwa hela yake tuone wangapi wana jeuri hiyo, walipe na mishahara yao ya internship, halafu ndio waende kuongea na serikali.
 
Mwenye shibe,na wanaoshibishwa na wenye shibe kamwe hawawezi kumkumbuka mwenye njaa .hivyo hata waimba mapambio kwa kuwa wanaouhakika washibe wanaona sawa kwa wenye njaa wapambane na hali zao kivyao.
 
Mhe.Rais dkt. John Magufuli amezungumzia DAKTARI BINGWA, ambaye lazima atakuwa amepata ufadhili maalum kusomeshwa ubingwa na ndio maana wanakuwa wamejaza mkataba maalum kutumikia serikali; ila baada saa za kazi ruksa sekta binafsi na hasa vijiwe vyao walivyofungua kila kona katika miji mikubwa🤣🤣

​
 
1. Magufuli usiwapangie cha kufanya, Walisoma kwa mkopo ni pesa ya taxpayers sio yako, baba wala mama yako.

2. Jifunze kufuata sheria za nchi, Hizi sheria peleka kwa mke na watoto wako.

3. it was a shame election, you are not a legitimate President, just a Gang Leader!
 
Wanalipa favor yao ni kupewa 100% tena kipindi cha nyuma siku hiz wengine mpk wanakosa inategemea umesoma shule gani
Ndiyo maana nikasema labda imebadilika. Mi niliona wanapewa bila kulipa miaka kama kumi imepita.
 
Mkuu leo nilikaa na kanda mmoja wa chama cha kijani mpumbvu sana! Yeye hajui lolote kuhusu mtumishi wa umma ana ropoka tu. Raisi huyu hajawaongezea mishahara watumishi miaka yte mitano leo anabwabwaja ati dr kakimbia
 
Damu ya Saanane itakufuata kila step shwain?
 
Mkuu Tumaini, si bure pengine labda kauli hii imetolewa kwa makusudi ili kuwatoa watu katika mjadala unaondelea hivi sasa nchini juu ya wimbi jipya la maambukizi na vifo vitokanavyo na COVID 19. Hii hasa inatokana na mara baada ya madhehebu makubwa mawili ya Kikristo kutoa neno.
 
Kuna makabila siyo ya kuyapa kabisa nchi kuongoza/ kutawala! kutokana tu na hulka zao za ubabe, udikteta, ubinafsi, ujuaji, ukabila, ukaidi, uonevu, ukatili, na ubaguzi.
 
Jiwe anaona hii nchi kama ni yake vile! Mungu tutetee na hili janga..
 
Kuna kitu najiuliza hivi , daktari akitumikia sekta binafsi ikiyopo Humu Humu tanzania ni kosa kwani ?
Au akienda sekta binafsi anakua halipi pesa Ya mkopo anayodaiwa ?
Maana bado anaendelea kutumikia watanzania šema tu ni kwa njia nyingine,
Hapa mzee baba , kasahau kua yeye aliacha ualim kisha akaenda kwenye siasa , kihalisia ilikua anafuata maslahi binafsi hakuridhika na sehemu aliyopo .

Ukwel lažima usemwe ,
Au našema uongo ndugu žangu
 

Huyo mzee Kikwete ataaongea nini wakati na yeye alikuwa mchafu, na huyo mwenye kiburi cha madaraka ni kwakuwa anajua waliomtangulia sio wasafi.
 
Aliyetoa hiyo kauli akapimwe mkojo lazima utakuwa mchafu sana!
 
Nina siku sijakusoma. Balaa limerudi. Hata na huyo Jmc06 anayekushukuru ni sampuliyo. Nilishasema wewe ni kilaza kama jina lako lilivyo( kithembe tu). Mfano/ kisa ni fundisho zuri. Umetumia isivyo. Ukilaza haujaacha mtu salama!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…