Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,746
- 5,772
Tumekusikia mara kwa mara ukilalamika juu ya wasimamizi wa sheria za nchi kunyanyasa raia wa kawaida.
Leo hii tar 25 Feb 2021 unalalama juu ya watumishi wa TRA kubambikia wanachi kodi na kuleta kilio kikubwa. Hili ni tatizo kubwa sana, wewe kama mkuu wa nchi hukupaswa kuwalilia wanaobambikizwa kodi. Una mamlaka na vyombo vyote vya kukupatia taarifa za ukweli, turitarajia kusikia neno la ukweli hii leo.
Hivi rais wetu jinsi unavyofuatilia mambo, hujui kuwa bado jeshi la polisi halifai? Hujui kuwa wanaoua hawafikishwi mahakamani na wasioua wanaozea rumande?
Mh rais watanzania wanataka mabadiliko makubwa juu ya upatikanaji wa haki za msingi hapa Tanzania. Kwa ujumla masuala ya watu kubambikiwa kodi ni sehemu tu ya tatizo sugu.
Mh Rais, kama kweli wewe ni mpenda haki na hutaki dhuluma, unda tume huru juu ya uvunjivu wa haki za binadamu, miezi miwili ni mingi utapata jibu.
Polisi, ofisi ya DPP zote zimeoza. Watanzania wanaonewa na kuteseka. Hivyo TRA kubambikia watu kodi kubwa ili wapate rushwa ni kama mzaha tu.