Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 72,020
- 129,293
Tumekusikia mara kwa mara ukilalamika juu ya wasimamizi wa sheria za nchi kunyanyasa raia wa kawaida.
Leo hii tar 25 Feb 2021 unalalama juu ya watumishi wa TRA kubambikia wanachi kodi na kuleta kilio kikubwa. Hili ni tatizo kubwa sana, wewe kama mkuu wa nchi hukupaswa kuwalilia wanaobambikizwa kodi. Una mamlaka na vyombo vyote vya kukupatia taarifa za ukweli, turitarajia kusikia neno la ukweli hii leo.
Hivi rais wetu jinsi unavyofuatilia mambo, hujui kuwa bado jeshi la polisi halifai? Hujui kuwa wanaoua hawafikishwi mahakamani na wasioua wanaozea rumande?
Mh rais watanzania wanataka mabadiliko makubwa juu ya upatikanaji wa haki za msingi hapa Tanzania. Kwa ujumla masuala ya watu kubambikiwa kodi ni sehemu tu ya tatizo sugu.
Mh rais kama kweli wewe ni mpenda haki na hutaki dhuluma, unda tume huru juu ya uvunjivu wa haki za binadamu, miezi miwili ni mingi utapata jibu.
Polisi,ofisi ya Dpp zote zimeoza. Watanzania wanaonewa na kuteseka. Hivyo TRA kubambikia watu kodi kubwa ili wapate rushwa ni kama mzaha tu.
Unajifanya unaleta mada kisha unampamba kuwa ni mpenda haki na mfuata sheria! Hakuna mwizi yoyote wa kura ambaye ni muadilifu. Na hilo suala la TRA kubambikia watu kodi na kunyanyasa wafanyabiashara ni maagizo yake. Hapo alikuwa anafurahisha genge la wenye uelewa mdogo, ili kuwahadaa kuwa hujui nini kinaendelea.
Ukitaka kujua hafuati hiyo katiba na wala sio mtendaji haki, kawatangaza meya na naibu meya leo kwa nafasi ambazo hupatikana kwa kura za wajumbe. Amejisahau kutokana na yale maagizo aliyotoa ya kunajisi uchaguzi mkuu, sasa hivi anayafanya hayo hadharani maana amejua anaoongoza taifa lenye wanasheria wategemea tumbo, na wananchi makondoo. Huyo jamaa ni mlevi wadaraka kama walivyo walevi wengine wa madaraka.