Mh.Waziri Aweso Mfute Kazi Meneja Wa MWAUWASA.

Mh.Waziri Aweso Mfute Kazi Meneja Wa MWAUWASA.

Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2020
Posts
5,616
Reaction score
14,106
Mwanza.
Naandika jambo hili nikiwa na hasira sana,juu ya kero ya maji katika jiji la Mwanza.Sote tunafahamu Jiji hili lina chanzo cha uhakika cha maji (Ziwa Viktoria) Sasa huu ukosefu wa maji kwenye baadhi ya maeneo unasababishwa na nini ?

Si Machweo si Mawio,naona watoto wakiume nawa kike maeneo ya Sweya na Luchelele (kwa uchache) wamebeba ndoo za maji vichwani mwao,ambayo wameyachota kwenye Ziwa,haya maji sio safi na Salama kwa matumizi.

Mbaya zaidi ni kwamba maeneo haya yako karibu kabisa na mradi mkubwa wa maji wa Butimba.kama maeneo ya karibu na mradi hayapati maji ya uhakika mradi huu una faida gani ?

Na kwa maeneo ya mbali na mradi huu hali ikoje ?

Nakuomba Mh.Aweso,mfute kazi haraka sana Meneja wa MWAUWASA.
 
Back
Top Bottom