Mh. Zitto kuna ukweli gani katika ripoti hii?

Mh. Zitto kuna ukweli gani katika ripoti hii?

@niweze

I am commenting on the void of credible leaders, if there is a leader whom the youth of this nation look up to and he lets them down, than which direction are we as a whole humanity heading towards. The problem of corruption is all over the world, its the issue of today. However, in order to move forward in this world, this vice has to be terminated from the roots, not just cut a few branches off. I am more concerned about the young generation, if they have no one with integrity to look up to, then what becomes of us as a whole humanity. What was independence for? What does it say about the world in which we live in now, that to have the latest version of smartphone in your hand makes you more cool than an education? What does this say about morals, values, ethics?

( Chenge did those tricks and we caught them. )

well the above mentioned individual has done alot of tricks & continues to do so. He is roaming free as a Vulture in the streets of Dar. As a protector of the law of this nation, he and his other prominent lawyer friend, together, they have done not a thing to obey the rule of law, instead they have just accumulated wealth to a copious amount that even a million dollars seems like peanuts to the frmer AG. As far as the concept of JUSTICE goes, the guy is rumored to be still involved in denying JUSTICE in a special project which he is still considered to be part off.

As far as corruption in Tanzania goes, its not today's issue, apparently, when a certain case was going on at the local high court, and two individuals were screaming at the top of their lungs how money was being stolen, still their screams fell to deaf years, and today they are both silenced forever. Now, there is a different generation emerging and still facing the same parasite of corruption. I was just saying that it would be a total void if there is not one young leader from the crop of next gen. leaders to atleast have some integrity&character, because in order to move forward the young need to believe in hope. Not false hope.
Hope I made sense.

U will make sense kama utakuwa na ushujaa wa kuondoka huko ulikojificha na kuja nyumbani kuwa huyo CREDIBLE LEADER young people look for>>>>>>>
 
Labda kuna vitu vingine sijavisoma vizuri, nitarudia nipitie vitu vingine. Nguruvi nimekupata sana na wengine vile vile japo wengine kama kawaida hawawezi kuacha kujenga hoja bila kutumia vijembe na innuendos ambazo wanajua kabisa hawana ubavu wala uwezo wa kuzitetea.
 
OmarIlyas,
Mkandara nashindwa kukuelewa: Yaani ulitaka Zitto alazimishe kufutwa kwa mkataba wa Buzwagi? Unaweza kutuambia hilo lingewezaje kufanikiwa?

Zaidi, watanzania ni lazima tukue na kutambua kuwa kuna tofauti kati ya maoni ya mtu na taarifa....Conclusion ya mwanafunzi mtafiti huyu imeegemea zaidi katika maoni yake kuliko taarifa zilizopo na alizopewa. Hauna tofauti na maoni ya wanadiplomasia wa marekani katika cable zao zinazosambazwa na wikileaks....Lakini kama ninyi mmeamua kuwa hizo ndizo njia za kujua ukweli wa kuaminika, then keep swalowing them....
Mkuu wangu siasa sio akili ya darasani bali ni kukubali kutokubaliana na itikadi na sera za mwenzako. Msimamo huu ndio huleta ushindani kati ya vyama na wabunge wetu ni wawakilishi wa fikra hizo ili kuwaletea wananchi maendeleo yao.

Zitto hawezi kufuta mkataba Buzwagi na wala sii msingi wa hoja yangu toka mwanzo kwa sababu hawezi kuibadilisha isipokuwa kama Mbunge wa Chadema na mwakilishi wa wananchi against uwekezaji wa namna hii..Huu ndio msimamo wake na wa chama na hauwezi kubadilika kwa msaada wa mabati ya shule. Shirika kama hili ambalo linainyonya Tanzania na ktk misnigi hiyo ndio kumpa yeye ridhaa ya wananchi ktk kupigania haki yao leo amekuja wakumbatia kwa mtaji mdogo sana wa mabati.. Sasa kama wewe huoni tatizo hapo utakuwa huijui siasa ila unazungmza kwa kutumia logic ya kwamba Mbunge kazi yake ni kuwapeleka wananchi maendeleo na hii ni njia mojawapo regardless.

Na kama ingelikuwa hivyo Republican (Marekani) wangekubali Healthcare ya Obama au kuondoa Tax exemptions kwa matajiri. Huu ndio msimamo wa chama na wabunge wake pamoja na kwamba wote wanajali sana maendeleo ya wananchi wao..Hivyo yeye kuwepo ktk kamati ya madini ya Bomani alitakiwa kuwakilisha na kusimamia sera za Chadema na maadam Buzwagi imeingia ktk mkumbo mikataba mibaya hatakiwi kuunga mkono na kuita swala hili ni win win situation wakati ukweli ni kwamba we are looser!..

Sasa ebu nambie kwa nini swala hili limekuwa zito kulimeza kwa baadhi ya watu?.. ni kwa sababu ya Barrick na sii Zitto ama shirika jingine lolote.. Barrick waliua watu Bulyanhulu, nakujmbuka sana Tundu Lissu alikuwa wakili na alipata matatizo makubwa sana, hawa hawa Barrick wamefanya unyama kila wanapotia mguu na kuua kwao ni jambo la kawaida kabisa wakitumia kuhonga viongozi wa serikali.. Zitto hakutakiwa kukaa nao meza moja hata kidogo unless wao wanasilimishwa (batizwa) na kuikubali haki yetu ya msingi na wajue kwa ufasaha msimamo wa Chadema kama chama.

Mwisho, nimemuuliza Zitto ukweli wa habari hii na yeye kakubali ni ukweli hakusema lolote kama unavyojaribu kupinga hapa kutaka kumwondoa huyu kijana nje ya hoja yake. Na lazima ukubali huyu kijana kaweza kujenga hoja nzito sana na inatupa mashaka zaidi tunapofikiria Zitto mkombozi wetu kanywea kimyaa hali akituambia tumsome yeye ktk tovuti yake. Labda nikwambie tu ya kwamba Sinclair (dalali wenu) huku anasema wazi kabisa ya kwamba hakuna mabadiliko yoyote ya ushuru yanaweza kutokea hivi sasa na amepata uhakika toka kwa viongozi wetu na kodi hizi bado zinatakiwa kupitishwa bungeni na HALITAPITA.. wewe unayajua haya? - No matter what Barrick hawataathirika na sheria yoyote inayoweza kuwekwa..!
 
Kilicho na kinachomponza Zitto ni umaarufu na ufisadi. Mtu anayepiga kelele ili aunganishwe kwenye ulaji ni mbaya sana. Na kwa hili na mengine yaliyojificha Zitto hana tofauti na walafi wengine, pengine tu yeye amekosa channel ya uhakika. Kuna dalili zote kuwa akipata nafasi huyu kijana hawezi kuiachia hata kidogo.

Umaarufu anao na ni wazi kuwa hadi sasa mmeshatambua kuwa juhudi zenu zote mlizozifanya kumuondolea umaarufu huo zinashindikana. U know why? Kwa sababu Zitto ni mtu wa kujifunza kila wakati na hivyo kujiongezea maarifa kila siku tofauti na ninyi na hao mashujaa wenu mnaowachonga kila kukicha....

Baada ya kuanzisha ule mpambano wa madini na kupata umaarufu mkubwa Rais alipo amua kumpa nafasi na yeye kula kupitia ile kamati jamaa hakubisha, aliporudi bungeni kutoa ripoti tone yake ikabadilika kabisa. Akaanza kuonekana kuzungumza zaidi kwa busara kwa kuwa alishakula chake cha juu.

Tatizo akili za watanzania zimekaa kiulaji tu na hivyo kila nafasi mnaiangalia katika muktadha huo. Kama hujui basi mwenzako Zitto alichukulia nafasi adimu kwa yeye kujifunza kuhusu sekta ya madini. Na ndio maana unaona zaidi anaongea kwa busara with facts, figures and solutions na sio ukasuku wa hao mashujaa wenu mnaowachonga kila kukicha mkidhani watamfunika Zitto. Na ndio maana sasa amekuwa zaidi sio tu kama authority katika masuala ya kitaalamu ya sekta ya madini tu bali anaelekea kuwa hivyo hata katika sekta ya mafuta na gesi....

Alipoenda Rais kufungua barabara huko kijijini Kigoma jamaa ndo akawa amekwisha kabisa utafikiri barabara ilikuwa ni favour wakati yeye anatambua hilo ni jukumu la serikali na hata hivyo kwa wale wapiga kula bongo lala ikaonekana kuwa ni juhudi zake binafsi zilizofanya hilo.

Tatizo wengie wenu mnajifanya mnajua kuhusu siasa, utawala na maenmdeleo kumbe hamna kitu. Hivi unadhani miradi ya maendeleo inaenda na kutekelezwa mradi tu ni wajibu wa serikali. Hujiulizi ni vipi serikali hii tuliyonayo miaka karibia hamsini sasa haikutambua wajibu wake wa kupeleka nyenzo na miundombinu ya maendeleao katika mikoa ya Rukwa na Kigoma hadi pale Zitto alipoweza kujenga ushawishi alio nao na Pinda kuwa Waziri Mkuu? Hivi unajua ni mambo mangapi ameyafanya Zitto kuondoa vizingiti vya kila kukicha vyenye kulenga kuzuia ama kuchelewesha miradi hiyo ya maendeleo katika eneo hilo? Hiovi unadhani haya yanafanyika kwa kuwa ni jukumu tu la serikali bila ya juhudi binafsi na nguvu za ushawishi za wabunge ?


Nikielekea upande wa ndani wa chama chetu cha CDM mambo ni yale yale. Ukikuta mtu mnaye kwenye chama kimoja na yeye kila siku anakuwa na mawazo tofauti na chama ujue hilo ni tatizo. Mimi nijuavyo mtu unakubaliana na chama kwa kufuata itikadi na upambavu wake wote. Kama hukubaliani nacho then achana nacho either unahamia kingine au unaanzisha chako ambacho unajua kinakubaliana na malengo yako.

Kumbe ni walewale ..........Hizi siasa za chuki zitawala wenyewe zikawamaliza bila hata hao mnaowaona maadui zenu hawakuathirika nazo.....

Ukirejea siku aliyotamka Bungeni kuwa Spika Makinda anaendesha bunge vizuri sana hiyo ilikuwa ni dharau kwa wenzake kama kina Lema, Lissu, Msigwa na wengineo ambao wamekwaruzana mara kadhaa na Spika huyo. Kwa ufupi ni kusema kuwa wenzake wa CDM ni wahuni bingeni kwa kuwa ndo wanaomkorofiisha Makinda.

Hivi mbunge anayetamka kuwa tufunge milango tupigane ama kusimama bungeni kuongea kama yuko kilingeni kama sio muhuni utamuita nani? Tena wengine ni watumishi wa mungu. angalao Lema na Tundu tunaweza kuwaelewa kuwa ni suala la character ambalo ni wazi malezi yana sehemu yake.....

Sasa lipo wazi kwa nini wabunge wa CDM wanapingana kuhusu posho za vikao. Yeye hataki kuchukua kwa kuwa kuna wengine wanao muwezesha wakati wenzake Bungeni ni sehemu ya kujipatia kipato. Kijana think twice!

Hapa mmeshikwa pabaya na wazalendo wa kweli wataonekana na wajanjawajanja wataonekana.....
 
OmarIlyas,
Mkuu wangu siasa sio akili ya darasani bali ni kukubali kutokubaliana na itikadi na sera za mwenzako. Msimamo huu ndio huleta ushindani kati ya vyama na wabunge wetu ni wawakilishi wa fikra hizo ili kuwaletea wananchi maendeleo yao.

Zitto hawezi kufuta mkataba Buzwagi na wala sii msingi wa hoja yangu toka mwanzo kwa sababu hawezi kuibadilisha isipokuwa kama Mbunge wa Chadema na mwakilishi wa wananchi against uwekezaji wa namna hii..Huu ndio msimamo wake na wa chama na hauwezi kubadilika kwa msaada wa mabati ya shule. Shirika kama hili ambalo linainyonya Tanzania na ktk misnigi hiyo ndio kumpa yeye ridhaa ya wananchi ktk kupigania haki yao leo amekuja wakumbatia kwa mtaji mdogo sana wa mabati.. Sasa kama wewe huoni tatizo hapo utakuwa huijui siasa ila unazungmza kwa kutumia logic ya kwamba Mbunge kazi yake ni kuwapeleka wananchi maendeleo na hii ni njia mojawapo regardless.

Na kama ingelikuwa hivyo Republican (Marekani) wangekubali Healthcare ya Obama au kuondoa Tax exemptions kwa matajiri. Huu ndio msimamo wa chama na wabunge wake pamoja na kwamba wote wanajali sana maendeleo ya wananchi wao..Hivyo yeye kuwepo ktk kamati ya madini ya Bomani alitakiwa kuwakilisha na kusimamia sera za Chadema na maadam Buzwagi imeingia ktk mkumbo mikataba mibaya hatakiwi kuunga mkono na kuita swala hili ni win win situation wakati ukweli ni kwamba we are looser!..

Sasa ebu nambie kwa nini swala hili limekuwa zito kulimeza kwa baadhi ya watu?.. ni kwa sababu ya Barrick na sii Zitto ama shirika jingine lolote.. Barrick waliua watu Bulyanhulu, nakujmbuka sana Tundu Lissu alikuwa wakili na alipata matatizo makubwa sana, hawa hawa Barrick wamefanya unyama kila wanapotia mguu na kuua kwao ni jambo la kawaida kabisa wakitumia kuhonga viongozi wa serikali.. Zitto hakutakiwa kukaa nao meza moja hata kidogo unless wao wanasilimishwa (batizwa) na kuikubali haki yetu ya msingi na wajue kwa ufasaha msimamo wa Chadema kama chama.

Mwisho, nimemuuliza Zitto ukweli wa habari hii na yeye kakubali ni ukweli hakusema lolote kama unavyojaribu kupinga hapa kutaka kumwondoa huyu kijana nje ya hoja yake. Na lazima ukubali huyu kijana kaweza kujenga hoja nzito sana na inatupa mashaka zaidi tunapofikiria Zitto mkombozi wetu kanywea kimyaa hali akituambia tumsome yeye ktk tovuti yake. Labda nikwambie tu ya kwamba Sinclair (dalali wenu) huku anasema wazi kabisa ya kwamba hakuna mabadiliko yoyote ya ushuru yanaweza kutokea hivi sasa na amepata uhakika toka kwa viongozi wetu na kodi hizi bado zinatakiwa kupitishwa bungeni na HALITAPITA.. wewe unayajua haya? - No matter what Barrick hawataathirika na sheria yoyote inayoweza kuwekwa..!

Kaka mfano wako wa REPUBLICANS unajibu mengi kwani kwa mtazamo wangu, washabiki wengi wa CHADEMA wameathirika sana na siasa za Ki-TEA PARTY ambazo msingi wake ni chuki dhidi ya wengine.

Na pia sentensi yako ya mwisho inasema mengi pia...iweje sheria mpya ambayo imeondoa ringfencing na tayari kuna mfano hai wa mgodi wa tulawaka kuathirika na sheria hiyo hivyo kuanza kulipa tofauti na ilivyokuwa mwanzo, bado nasema kuwa Barrick haitaathirika nayo?

Kuhusu kujenga hoja kwa mwandishi wa thesis hii, ni kweli amejenga hoja lakini sio hoja ya kisomi kama ambavyo misingi ya uandishi wa tafiti za kisomi utakavyo. Hoja yake ingekuwa sawa kama angekuwa anaandika makala katika magazeti yetu kamalile la Mwanahalisi....

Kuhusu mtazamo wa win win na kuwa sisi ni losers, well, ni kweli we are losers and we will always be when it come in working with these vultures called multinationals lakini ni wazi Zitto ameweza kutumia nafasi yake aliyoipata kwa taabu na madhara makubwa kisiasa kutufanya tuwe less lossers leo hii 2011 kuliko tulivyokuwa hapo kabla. Sasa kama unadhani angeweza kufanya tuwe winners, tungeshukuru sana kuona mchango wako katika kufikia huko kuliko kuwa mstari wa mbele wa kumuhukumu kwa kutofanya yale ambayo ni wazi asingeweza kufanikisha....
 
Kama nakumbuka mwanzo tu wa thread yako ulianza na kuwa hupendi unafiki ukiwa na maana kuwa tuhuma za huyo mwanafunzi mtafiti ni dalili ama uthibitisho wa unafiki wa Zitto
Hapana Unafiki ni mimi ambaye namshabikia Zitto ili hali ninaweka mashaka na uongozi wake.

Sasa kaka kama angenyamaza kuhusu suala la Dowans huku akijua kuwa wazo lake lingetuokoa katika janga hili tulilo nalo sasa eti kwa kuogopa kuharibiwa jina lake si ndio ungekuwa unafiki wenyewe huo usioutaka? Viongozi wanaopita kuangalia nini mnataka kusikia na kuanza kuimba kama makasuku ndio wametufikisha Tanzania katika majanga mengi tunayoyalalamikia sasa.
Wazo la Zitto lingetuokoa vipi hali leo generator hiyo inawashwa na bado tatizo liko paleplae?.. sikiliza mkuu wangu, JK alikuwa na zaidi ya miaka minne kuleta Umeme wa dharura nchini na kama nakumbuka Rashid alisema tusiponunua generator ya Dowans nchi itaingia kizani. Zitto akichangia kwamba itachukua miezi 16 hadi 18 kuagiza generator mpya na tumekaa na mgao wa kawaida kwa miezi 24 hakuna jipya lililotokea..Kwa ujumla tumekaa miaka mitatu hakuna generator mpya iliyonunuliwa wala kuagizwa. Leo tatizo limezidi ndio mnaikumbuka Dowans!
Kaka lets be honest hapa, hivi kama mlishindwa kuchanga kumtoa mpambanaji wetu wahuko ughaibuni katika matatizo yake ya wakati ule mngeweza kuwachangia watoto wa kigoma kaskazini ili wawe na kitu kinachoitwa shule?
Usimung'unye maneno mkuu wangu Mpambanaji gani?..Kama una maana MM alikuwa haikuwa deal kama mnavyoambiwa ama kusimuliwa na hazikuhitajika fedha kama sikosei. Kwa nini tushindwe kumchangia mbunge wetu Zitto of all people! comeon now - Omar watu wanachangia maiti na harusi watashindwa kuchangia jambo la maana kama hili labda kama itakuwa biashara lakini nina hakika inapofikia harambee mshikaji wala usiombe.
So kwa ushauri wako Zitto ajali zaidi umaarufu wake lakini sio kusimamia yale anayoweza kushawishi na kutekelezeka na pia msaada wa maendeleo kwa wapiga kura wake? Kaka inaelekea tayari una mtazamo wako kuhusu Zitto na sasa umejiunga katika lile kundi la kukaa mkao wa kula wa kupata kitu chochote kile ambacho kitakuwezesha kuhalalisha mtizamo wako kwa watu wengine ili ujisikie vizuri....
Hapana Umaarufu wa Zitto unatokana na kile anachokisimamia na sii sura wala machachari yake. haya ni makosa kmakubwa hutumiwa na baadhi ya watu kwamba Zitto hutafuta Umaarufu kama ingekuwa hivyo angeenda kucheza sinema au kuimba bongoflava! kazi ya siasa ni kazi kubwa sana na inahitaji ujasiri ambao ni yeye na Dr. Slaa pekee wameuonyesha hivyo tunategemea ukomavu wao ktk yale wanayosimamia.
Yawezekana wakati Zitto analipua suala la Buzwagi, kwake yeye ilikuwa ni kujenga mazingira ya kuibua mjadala utakaopleta mabadiliko katika sekta ya madini na wala hakuwa akiwazia umaarufu na hivyo hakuwa tayari kugeuka another demagogue kama ambavyo wengi mngelipenda kumuona anakuwa....
hapana mkuu wangu Zitto hawezi kujijengea mazingira isipokuwa anasimamia haki na hatua za kuifikia haki hiyo huanza Bungeni. Nina imani kabisa kwamba Zitto aliamini na kuelewa kwamba mkataba wa Buzwagi umewekwa kinyume cha sheria tena ya Kitaifa na sii swala la sera ya chama. Na umaarufu wake haukutokana na kusimama kupinga mkataba huo isipokuwa mhanga alokubali kuadhibiwa akisimamia haki hivyo swala la kuwepo mabadiliko ya sekta ya madini umetokana na sacrifice aloichukua na kumpa umaarufu. wananchi sii wajinga kumpa mtu umaarufu kwa sababu nyingine zaidi ya kuwa mtetezi wa mali na haki zao.

Taratibu mkuu wangu unaandika mengi kwa wakati mmoja nashindwa kukufuatilia..
 
Kaka mfano wako wa REPUBLICANS unajibu mengi kwani kwa mtazamo wangu, washabiki wengi wa CHADEMA wameathirika sana na siasa za Ki-TEA PARTY ambazo msingi wake ni chuki dhidi ya wengine.

Na pia sentensi yako ya mwisho inasema mengi pia...iweje sheria mpya ambayo imeondoa ringfencing na tayari kuna mfano hai wa mgodi wa tulawaka kuathirika na sheria hiyo hivyo kuanza kulipa tofauti na ilivyokuwa mwanzo, bado nasema kuwa Barrick haitaathirika nayo?

Kuhusu kujenga hoja kwa mwandishi wa thesis hii, ni kweli amejenga hoja lakini sio hoja ya kisomi kama ambavyo misingi ya uandishi wa tafiti za kisomi utakavyo. Hoja yake ingekuwa sawa kama angekuwa anaandika makala katika magazeti yetu kamalile la Mwanahalisi....

Kuhusu mtazamo wa win win na kuwa sisi ni losers, well, ni kweli we are losers and we will always be when it come in working with these vultures called multinationals lakini ni wazi Zitto ameweza kutumia nafasi yake aliyoipata kwa taabu na madhara makubwa kisiasa kutufanya tuwe less lossers leo hii 2011 kuliko tulivyokuwa hapo kabla. Sasa kama unadhani angeweza kufanya tuwe winners, tungeshukuru sana kuona mchango wako katika kufikia huko kuliko kuwa mstari wa mbele wa kumuhukumu kwa kutofanya yale ambayo ni wazi asingeweza kufanikisha....
- Pasipo na IMANI kuna Uovu, Pasipo na MISINGI kuna Ufedhuli, Pasipo na ITIKADI kuna Ujanjaujanja...Yote haya ni mazalia ya UFISADI..

Hii ndio signature yako na inazungumza mengi kuliko unavyojieleza.

Kama Chadema hawana tofauti na Tea Party ndio maana unashindwa kuwaelewa kwa sababu wewe sii Republican wala Chadema..Matusi ya Tea party yanatokana na uongozi wa Obama mwenyewe ambaye hawasaidii lolote Wamarekani weusi na weupe isipokuwa kuonyesha udhaifu ktk uongozi wake na maswala ya ndani ya Marekani..Huyo huyo Obama anachukiwa na weusi wengi kuliko unavyofikiria wewe kwa hiyo swala sio Obama tena isipokuwa anawapa sababu Tea Party kutudharau sisi wote weusi.. Na pengine chuki ya wana Chadema inatokana na viongozi kama hawa wanaoshindwa kusimamia sera zao bali kutafuta bypartisan ambayo at the end, they will never win..

Zitto hawezi kutufanya tushinde ktk hili la Buzwagi na Barrick isipokuwa Zitto anaweza kutusaidia sana Chadema tushinde uchaguzi ujao na kama tukishinda hayo ya Barrick yatapatiwa ufumbuzi!. Kinachohesabika ni ridhaa ya wananchi kutokana na msimamo wetu imara ktk maswala kama haya..Na mchango wangu mimi ni kama huu kwa Zitto nina hakika unaweza kutupa ushindi baadaye!
 
...... Zitto ameweza kutumia nafasi yake aliyoipata kwa taabu na madhara makubwa kisiasa kutufanya tuwe less lossers leo hii 2011 kuliko tulivyokuwa hapo kabla. Sasa kama unadhani angeweza kufanya tuwe winners, tungeshukuru sana kuona mchango wako katika kufikia huko kuliko kuwa mstari wa mbele wa kumuhukumu kwa kutofanya yale ambayo ni wazi asingeweza kufanikisha....


Kutufanya tuwe less loser haina maana akijisiahu , akikosea au akiteleza tusimshtue. Au unata kausema zitto ni mailaka akisoea twende kweye majumba ya ibada tumuombee?

Inawezekana wako personal haters wa ziito lakini pia watu hapa wamechangia mambo mengi ya msingi sio kwa zitto tu lakini kwa viongozi wote.

- Pasipo na IMANI kuna Uovu, Pasipo na MISINGI kuna Ufedhuli, Pasipo na ITIKADI kuna Ujanjaujanja...Yote haya ni mazalia ya UFISADI..
Hii ndio signature yako na inazungumza mengi kuliko unavyojieleza.
Kama Chadema hawana tofauti na Tea Party ndio maana unashindwa kuwaelewa kwa sababu wewe sii Republican wala Chadema..Matusi ya Tea party yanatokana na uongozi wa Obama mwenyewe ambaye hawasaidii lolote Wamarekani weusi na weupe isipokuwa kuonyesha udhaifu ktk uongozi wake na maswala ya ndani ya Marekani..Huyo huyo Obama anachukiwa na weusi wengi kuliko unavyofikiria wewe kwa hiyo swala sio Obama tena isipokuwa anawapa sababu Tea Party kutudharau sisi wote weusi.. Na pengine chuki ya wana Chadema inatokana na viongozi kama hawa wanaoshindwa kusimamia sera zao bali kutafuta bypartisan ambayo at the end, they will never win..
Zitto hawezi kutufanya tushinde ktk hili la Buzwagi na Barrick isipokuwa Zitto anaweza kutusaidia sana Chadema tushinde uchaguzi ujao na kama tukishinda hayo ya Barrick yatapatiwa ufumbuzi!. Kinachohesabika ni ridhaa ya wananchi kutokana na msimamo wetu imara ktk maswala kama haya..

Umetoa hoja saffi mary ana genralise uwa washabii wa CDM wote Taaizo lao wana chuki binafsi. Je washabkiki wa chama chake tatizo lao nini?

Vipi hawa washabiki wa CDM kama chuki zao zinatokana na zinapata nguvu sababu ya Matatizo yanyosabbishwa na chama anachsabikia yeye.

 
Nimeona nichangie tena maana nadhani wachangiaji wanapotosha makusudi kabisa mjadala huu.

I am not corrupt. I have never been corrupt and I will not.

Mali zote nilizonazo nimeorodhesha katika daftari la mali na madeni. Sina nyumba Dar es Salaam kama baadhi yetu wanavyodai hapa. Ninamiliki magari 2 tu mitumba niliyonunua kutokana na kipato changu.

Sina biashara yoyote hapa nchini. Ninamiliki hisa kampuni moja ya publishing ambazo sijawahi kupata gawio toka ianze kazi.
Nina nyumba ndogo ya vyumba viwili kijijini kwangu Mwandiga.

I have never ever been corrupt and I have no quest for properties. Sina tamaa ya mali.

Ninaomba tujadili hoja hii bila kutukanana wala kuzushiana. Nimejibu hoja hii kama mwulizaji alivyotaka katika post yake ya kwanza kabisa.

Wabunge na Halmashauri za wilaya na miji huomba misaada mbalimbali kwa majimbo yao ili kusaidia maendeleo. Sijawahi kushawishiwa hongo na kampuni ya Barrick sio tu kupewa. Nilikuwa muwazi kabisa katika msaada huu na miye ndio niliyomwambia mtafiti huyu kuhusu suala hili. Sidhani kama makampuni yanazuiwa maeneo ya kutoa misaada. Sijui kiwango gani cha misaada Barrick wametoa kwa wilaya ambazo wao wana endesha migodi.

Nafikiria sio sahihi kwa wanasiasa au mawakala wa wanasiasa kutumia hoja hii kunishughulikia kisiasa kwani sina kosa lolote katika jambo hili.

Sijawahi kuwatetea kwa lolote Barrick. Nimeeleza kuwa nimesimamia mabadiliko ya sheria ya madini na usimamizi wake. Michango yangu Bungeni ipo waziwazi katika blogu yangu www.zittokabwe.com na nimesemea jambo la umuhimu wa kodi.

Sasa kulifanya jambo hili kana kwamba nimekula rushwa ni kunipakazia tu bila sababu. Sina maslahi ya kifedha kabisa na suala hili.


Hon Zitto your defence is based on the wrong premises. We are not saying that you personally benefited from the grant. Hatusemi kuwa you're corrupt. Wala hatuitaji kujua mali au biashara ulizonazo. Najua kuna ambao wamejaribu kukutukana au kukuzushia mambo. Hao siko nao kabisa. However, what most of us are saying is that the act of you, as an MP, submitting the funding proposal, which was accepted, will potentially undermine your independence and impartiality when dealing with issue involving the company you applied for the funds. Hatusemi kuwa this will definitely undermine your independence and impartiality. Tunachojaribu kusema ni kuwa confidence yetu kwako itapungua kwa kiasi kikubwa. Inawezekana kabisa, you honestly submitted the proposal for the sake of the school na hao wanafunzi. Lakini politically ina raise questions because of your position as an MP and your previous stand on the practice of these sort of companies.

Tuchukue kwa mfano Mh Lissu nae atume proposal Barrick kuomba funds za kununua mabati ya kuezekea shule jimboni kwake. Wewe binafsi utaona hii ni sawa kabisa? Unaweza kusema kisheria ni sawa but ethically vipi? Public reaction itakuaje ukinzingatia nae amekuwa mstari wa mbele kupinga practice mbaya ya haya makampuni? Unaweza kusema kabisa kuwa hiyo funding haitabadilisha msimamo wako juu ya hiyo kampuni but do you think the public will have the same confidence on you when you're dealing with issues involving the same company?

Unakumbuka ile kesi ya extradiction ya Pinochet ambapo kwenye jopo la majaji, jaji mmoja alikuwa member wa Amnesty International. Kwa vile Pinochet alitakiwa kuwa extradited ili kujibu makosa ya human rights abuses na Amnesty international ina deal na protection of human rights ilibidi hukumu ya mahakama itenguliwe kwa sababu yule judge angeweza kuwa bias kumwe-extradict Pinochet japokuwa hata hivyo hakuwa biased kwenye hukumu yake. Sasa vipi leo tukitaka kuichunguza hiyo kampuni na ukateuliwa kwenye kamati ya kuichunguza, unaweza ukatuhakikishia vipi utakuwa independent, impartial and unbiased? Still kwenye maamuzi yako unaweza ukawa independent, impartial and unbiased na kuamua in favour of the company. Lakini upande wa pili si wataweza ku argue kwamba hawaamini ulikuwa independent, impartial and unbiased kwenye maamuzi yako because the company you decided in their favour granted some funding in your constituent following a proposal you personally submitted?

Unafikiri kama mwalimu mkuu wa hiyo shule angeandaa na ku submit hiyo proposal angepewa hizo fedha? Kama proposal ilikuwa imeandikwa na kutumwa na local government ya jimboni kwako, then hapo kusingekuwa tatizo. Lakini kama wewe, kwa kupitia nafasi na ofisi yako ya ubunge, uliandika na ku submit hiyo proposal then, sio tuu hii inaweza ku-undermine your independence na kupoteza confidence ya watu hasa unapodeal na issue zinazohusu hiyo kampuni, bali pia you may have stepped out of your shoes as an MP. The very act of submitting the proposal yourself as an MP is questionable. Inside your constituent, as an MP, you are expected to carry out the normal duties of meeting and talking to constituents regularly. However, submitting proposals to companies for developments projects is like stepping in the shoes of the local government and other bodies responsible for those tasks.

The problem we have in our country is that MPs are not provided with a job description or role specification. Individual MPs have complete autonomy on how to discharge their role and are held accountable for their decisions by voters at the ballot box. There is no prescribed list of responsibilities only conventions, customs and the desire to be re-elected. Kama tungekuwa na job description za MPs, you would not have done what you did.

We all know effective constituency work entails casework (getting information and lodging demands on behalf of people), policy work (seeking ways to benefit constituencies through existing or proposed national programs and legislation), voicing out views or concerns of constituents regarding national policy issues (this involves listening and explaining and expressing informed positions, although MPs are not obliged to agree with morally or ethically unsound views), and attending social events (particularly important in rural constituencies as a key means of maintaining close personal ties with their constituents).

However, as the Policy Forum have said, the reality of conducting constituency work in developing countries such as Tanzania poses many challenges. Generally, MPs operate with limited resources and in a political climate where the executive is dominant and potentially restrains MPs' legislative efforts to assist the needs of constituents. Moreover, constituents usually expect to receive direct assistance from their MPs given the ‘patron-client' nature of politics common in our country that encourages the expectation of direct forms of help. Expectations of direct forms of help ndio inawafanya wale wabunge ambao hawana uwezo kuomba fedha kwenye makampuni binafsi ili ku fulfill promises walizozitoa wakati wa kampeni. Kuna uwezekano hata wapiga kura kuingiwa na fikra kuwa ili kupata direct assistance inabidi kumchagua mbunge mwenye fedha zake au connections za kupata fedha.

In this context, the Policy Forum says constituency work predominantly involves MPs being inundated with individual claims for assistance leaving little time to engage in constructive member-constituent relations or other parliamentary activities. Leo ume submit proposal ya kuomba fedha za kununua mabati ya kuezekea shule. Kesho utatuma proposal kwenye kampuni nyingine kuomba fedha za kununua vitanda hospitali. Kesho kutwa utatuma proposal kwa kampuni nyingine tena kuomba fedha za kujenga stendi ya mabasi. Sasa hapa utakuwa mbunge au an executive arm of the local government? Hili sio tatizo la Zitto tuu. This is a problem in our country as far as the role of MPs in their constituencies is concerned.
 
Hongereni sana kwa mjadala mzito. Hivi ndivyo inavyopaswa. Lazima tuwajibishe viongozi wetu kwa matendo yao. Ukishakuwa kiongozi wa umma ujue wewe sasa ni mali ya umma na kila tendo lako litachokonolewa.

Watanzania tumezingirwa mno na rushwa kiasi kwamba tumekuwa kama mtu aliyeumwa nyoka. Tumeshajeruhiwa na kila kitu kinachofanana na nyoka tunadhani ni nyoka na inabidi tukimbie au tuanze kuupiga huo unyasi, baadaye tukigundua kwamba kumbe ni unyasi tu tunaanza kujicheka!!

Kwa kuwa msingi wa mtoa hoja ni kwamba kitendo walichofanya Barrick ni kitendo cha ama rushwa, hongo au kifisadi. Inabidi sasa turudi kwenye mstari na tutoe tena maana ya maneno haya ya 'rushwa', 'hongo' na 'ufisadi' maana ni maneno yanayochanganya.

Kwa mujibu wa Kamusi za Kiingereza na Kiswahili, maneno haya mawili yana maana zifuatazo:

i) Rushwa/corruption: tendo au matendo mabaya, yasiyo ya kiuaminifu na yanayokwenda kinyume cha sheria, hasa yanapofanywa na watu waliokabidhiwa madaraka (illegal, bad or dishonest behaviour, especially by people in positions of power-CD)

ii) Hongo/bribery: fedha au zawadi unayempatia mtu fulani ili afanye jambo fulani kwa ajili yako, mara nyingi jambo ambalo halina uaminifu au la kimaadili. (Money or a present that you give to someone so that they will do something for you, usually something dishonest.

iii) Ufisadi/grand corruption: Fisadi ni mtu anayefanya matendo ya rushwa, mtu ambaye hana aibu katika matumizi ya mali/raslimali ya/za umma (a fisadi is person acting corrupt, someone who has no shame, no conscience in regards of..management of public resources.

Sasa twende kwenye hoja ya Mhe Zito.

i) Je, kitendo cha Barrick kusaidia kujenga shule katika jimbo la Zitto ni rushwa. Bila shaka, kwa mujibu wa tafsiri hapo juu ni hapana, kwani hakuna sheria yeyote iliyovunjwa wala hakuna sehemu katika maandishi haya inayotuambia kwamba Zito aliwafuata hao Barrick kuwaomba wamsaidia kujenga shule ili wamafanyie kitu fulani.

ii) Je, kitendo cha Barrick ilikuwa ni kitendo cha hongo? Jibu hapa ni ndio na hapana. Ndio, kwa sababu pengine Barrick waliamini kwamba kwa kufanya vile wangeweza kumnyamazisha Zito katika kuwabana kuhusu ubeberu wao kupitia kampuni zao za madini hapa nchini. Hapana kwa sababu mbili:
  • sio jambo lisilo la kawaida kwa kampuni hizi za kibepari kutoa misaada ya kijamii kama sehemu ya jitihada zao za kukubalika katika jamii ili waendelee kunyonya vizuri bila kelele. Walichokifanya Barrick ni sehemu ya utamaduni wa makampuni ya kibepari (Corporate capitalist culture)
  • inawezekana kabisa Barrick walifanya vile kama sehemu ya jitihada zao katika kumnyamazisha Zito. Lakini je, walifanikiwa? Kwa maoni yangu sijaona ushahidi wowote kwamba Zito amenyamazishwa kwa Barrick kujenga shule katika Jimbo lake. Sana sana nimeona akiendelea kuibeba bango kampuni hii, na majuzijuzi ameishambulia kampuni hii kwamba hailipi kodi, madai ambayo ni mazito!
iiii) Je ni kitendo cha kifisadi kwa Zito kukubali msaada wa shule kutoka Barrick? Kwa tafsiri tulioitoa hapo juu, jibu lake ni kwa sauti kubwa HAPANA!

Hitimisho la kimantiki: Barrick walitumia ujanja wa kawaida wa kisaikolojia kwa kujaribu kumnyong'onesha Zito ili aachane na kelele zake za kuwabana kwa kumfanya ajisikie vibaya kuwashambulia watu waliomsaidia. Hii ni sehemu ya technique za persuasive psychology ambazo hutumiwa sana na makampuni ya kibepari. Ni wazi kwamba Barrick waliona kwamba kumhonga Zito moja kwa moja isingewezekana, bali kwa kufanya jambo la kijamii kule kwake. Inawezekana Zito kukataa msaada wa Barrick lingekuwa jambo zuri kinadharia na kisayansi, lakini lingekuwa jambo la ajabu na hatari kisiasa na kijamii. Bahati mbaya au nzuri, Zitto sio mwanasayansi/mwanadharia, Zito ni mwanasiasa na mwana jamii!! Muhimu hapa ni matendo ya Zito baada ya msaada wa Barrick huko Kigoma. Akiacha kusimamia misingi yake kuhusu raslimali za madini hapa nchini Barrick watakuwa wamefanikiwa katika jitihada zao za kisaikolojia.

Hivyo basi, kwa maoni yangu, hakuna kitu alichofanya Zito katika hili kinachoashiria kwamba ame-compromise principle yeyote ya kimaadili na kiwajibikaji, ambayo amekuwa akiisimamia.
 
Bwana Kitila

Suala letu kuu jee nani ali initiate msaada huo?

Kama ni Zitto ndiye aliyeomba (na inaonekana ni hivyo na wala mwenyewe hajakanusha) ni kwa nini alifanya hivyo?

Bila ya shaka utakuja na maelezo ya kuwa hajavunja kanuni wala sheria za msingi kwa vile Tanzania inaruhusu kuomba msaada kutoka kwa yoyote, lakini morally ni haki kwa Msimamizi wa sheria kumuomba anaemsimamia sheria yake msaada?

Ni sawa kwa polisi akiwa amekukamata huna leseni, akakuomba umpatie msaada wa fedha za chakula kwa watoto wake nyumbani?

Ni haki kwa mwalimu mwenye karatasi yako ya majibu ya mtihani, akakuomba umsaidie kusomesha watoto wake nyumbani?

Ni haki kwa TRA kuomba sadaka kwa watoto yatima, wakiwa kwenye duka ambalo limekeuka sheria?


Kwangu inaonekana zaidi kama ni blackmail kuliko ufisadi, rushwa wala hongo
 
Hon Zitto your defence is based on the wrong premises. We are not saying that you personally benefited from the grant. Hatusemi kuwa you're corrupt. Wala hatuitaji kujua mali au biashara ulizonazo. Najua kuna ambao wamejaribu kukutukana au kukuzushia mambo. Hao siko nao kabisa. However, what most of us are saying is that the act of you, as an MP, submitting the funding proposal, which was accepted, will potentially undermine your independence and impartiality when dealing with issue involving the company you applied for the funds. Hatusemi kuwa this will definitely undermine your independence and impartiality. Tunachojaribu kusema ni kuwa confidence yetu kwako itapungua kwa kiasi kikubwa. Inawezekana kabisa, you honestly submitted the proposal for the sake of the school na hao wanafunzi. Lakini politically ina raise questions because of your position as an MP and your previous stand on the practice of these sort of companies
Thank you EMT, may you allow me to ice your cake a little bit.

Hon Zitto, majority is not implicating you with any dubious business iota. Ironically they ask for clarification for good reasons. You shouldn't take their opinions as offensive rather than a challenge to work together as citizen to secure the future of our nation.

Zitto, you're still nascent in political sphere albeit you have achieved a lot. We all know that you've an ambition for more political role in the future.
The road ahead is rough and the onus to smooth it lies upon you. When controversy like this arises you need to clarify once and for all.
It's easier for the political opportunists to capitalize the saga for your downfall.

When the time comes, the opponents will draw an analogy with issues like barric, school, corruptions and your ambition.
The good example is on the 'Daily news online today' whereas the Wiki Leaks information implicates president JK in dubious deal with Kilimanjaro Kempsiki as per US ambassador comments.

Although the Ikulu has refuted the allegation, still the news has grossly undermined the credibility, integrity and public confidence on our president.
You need to confute the 'researcher' and not raise self defense. This is an opportunity to seize; otherwise it is a dormant volcanic eruption
 
U will make sense kama utakuwa na ushujaa wa kuondoka huko ulikojificha na kuja nyumbani kuwa huyo CREDIBLE LEADER young people look for>>>>>>>

The fight agains the corrupt and corruption is more importantly a moral fight. Corruption is evil, its pure greed, & greed has no bottom. If every MP is that weak to be lured into the corruption trap, then what will happen to the future of the country? If the youth have no one with integrity, character, moral values to look up to, whats the future then? Everymen for himself. Complete greed? I recall a quote from MLK, "the moral arc of the universe is long but it bends at the elbow of justice". It is the duty of this generation to guide the next gen. to the right path, not take them on the wrong moral path. People have died fighting, exposing corruption in this country, the past generation did it the way they knew best, through print media, radio etc.
 
Kama nitakuwa nimeielewa habari ya 'The Guardina' point number 3 kama nilivyoiweka, barric waliombwa na Zitto '
Anachotakiwa kujibu ni mambo yafuatayo:

1. Reseacher amesema Zitto ali benefit, je anakubali au anakanusha(benefit haina maana pesa tu hata kisiasa)

2. Kama ABG ilitaka win win situation (iliyotajwa mara 2) je win win ilikuwa kati ya taifa na ABG au ABG na Zitto kupitia jimbo lake!

3. Je ni Kweli ali submitt proposal ? na hiyo inamweka katika nafasi gani tukijua kuwa ni Barric waliosababisha atimuliwe bungeni.
kwanini baadhi ya watu wasiamini kuwa ukali wake juu ya Buzwagi ulikuwa ni kujenga mazingira ya quid pro quo.

4.Kwa kuomba msaada ABG, je hiyo haija compromise integrity, moral, sobriety,impartiality na public confidence yake.

5. Je Zitto haoni kuwa kuna conflict of interest akiwa mbunge 'thorn' kwa ABG, mjumbe wa kamati ya Bomani ,ambaye pia ni beneficiary wa ABG kisiasa jimboni kwake.

6. Je Zitto alitumia kigezo gani kuomba msaada barric akielewa kuwa kulikuwa na public interest ambayo ina compromise and undermine public confidence yake. Kwanini asifikirie mashirika mengine. Nasema hivi kwasababu Barric hawakwenda bali yeye aliwaomba.

7.
Je ushirikiano wa Zitto na kampuni hii inayotajwa kwa mabaya duniani (kama alivyoainisha MM) haiwezi kuzua maswali

Duh Mkuu mbona umepiga chini ya mkanda!! Hayo ndiyo maswali ya kujiuliza juu ya hili sakata. Na majibu yake yako wazi kabisa. Hapa ndg. Zitto hakuitendea haki jamii ya kitanzania. Kwa kifupi tunasema amezunguka mbuyu!!
 
Kwa hiyo huo msaada wa Barrick ulikuja vipi kwenye jimbo la Zitto? Nadhani hapa ndio kuna maswali ya wisdom, ethics n.k Je ni kwa kiasi gani msaada wa Barrick ulikuja jimbo kwa sababu waliombwa na Zitto? Nimerudi kusoma hiyo hoja na nimekutana na maneno haya ambayo nilidhani ndivyo nilivyoyasoma awali:

Kigoma North government submitted a proposal and Barrick funded it because Kigoma North's education system is lagging behind national standards. Kabwe had complained about the same issue in parliament for years, with no effect.

Hili ni tatizo ambalo tulikutana nalo kwenye barua ya Jairo ambapo mtu mmoja alisema "mawasiliano" wakati neno "mawasiliano" halipo kwenye barua yenyewe lakini watu wakawa wanazungumzia "fedha za mawasiliano" badala ya "mawasilisho". Sasa hapa tunaambiwa kuwa "Kigoma North Government".. sijui kwanza ni kitu gani!

Kwa hiyo kabla hatujaenda moja kwa moja kusema ni Zitto aliinitiate huu mradi kwa kupeleka proposal Barrick tukubaliane kwanza wanapozungumzia Kigoma North government ni kitu gani au kina nani hasa. Sasa tukishaonesha kuwa Zitto kuwa ni mmoja au kiongozi mkuuw a hiyo Kigoma North kwani kwa kadiri ninavyojua Kigoma ina wilaya nne Kasulu, Kibondo, Kigoma Mjini na Kigoma vijijini na hivyo Kigoma North haiwezi kuwa ni utawala wa serikali kuu bali wa Jimbo kwani tunajua kuwa lipo Jimbo la Kigoma Kaskazini.

Sasa kama ni kweli ni Jimbo la Kigoma Kaskazini lililoenda kupeleka proposal kwa Barrick kwa ajili ya tatizo hilo la Elimu basi maswali ya msingi yatahitaji kujibiwa; maswali ambayo tayari yameshaoneshwa hapa. Lakini katika kutafuta majibu ya maswali hayo twende taratibu kwa kuangalia facts tu na tuzifuate zinakotupeleka.
 
Mkuu MMM nadhani ni vyema kweli kujua hii Kigoma North Government ni nini. Kigoma kaskazini ni jimbo tu la uchaguzi na liko chini ya wilaya ya kigoma chini ya mkuu wa wilaya ya kigoma (Kigoma mjini na vijijini zipo chini ya mkuu mmoja wa wilaya).

Kwa mantiki hiyo Kigoma kaskazini haina halmashauri. Ukienda mbali utakuta kwamba hakuna kitu kinaitwa serikali ya kigoma kaskazini. Hapo kigoma kaskazini kutakuwa na Ofisi ya Mbunge ambayo huenda ndio imetumika kama serikali. Bado Zitto anaingia hapa.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Sikutaka kuchangia lolote kwenye huu mjadala. Ukweli usiopingika ni kuwa kama Zitto alipeleka maombi ya kichangiwa mabati Barrick, atakuwa ameigharimu political reputation yake kwa kiasi kikubwa. Bahati mbaya sana hata ukisoma utetezi wake na wa watetezi wake ni rahisi kujua kuwa kuna tatizo kubwa kwa Zitto mwenyewe kwa upande mmoja na Zitto na Chama chake kwa upande wa pili. Utetezi wa Zitto haukidhi haja. Haujajibu swali la NI KWELI ALIPELEKA PROPORSAL?
Lakini watu kama Omariyasi (mimi namtambua kama mtu wa karibu sana sana na Zitto) maelezo anayoyatoa yanaashiria mambo si shwari ndani ya Chadema. Huwezi kukiita Chama ambacho unaemshabikia ni kiongozi wake kuwa ni Tea Party alafu ukaacha tuamini kuko salama. Lakini kitendo cha kuwaita Lissu na Lema ni wahuni ambapo uhuni wao unaweza kutokana na malezi kumenifadhaisha sana. Katika vita hii ambayo Chadema wanayo sasa dhidi ya CCM hizi lugha ni house keepeng languages, hazitoki hadharani
 

"Kigoma North government submitted a proposal and Barrick funded it because Kigoma North's education system is lagging behind national standards. Kabwe had complained about the same issue in Parliament for years, with no effect." Reads part of the research seen by The Guardian on Sunday.

sidhani kama Zitto ndiye aliyeandaa hiyo proposal na kuituma Mkuu, kama tukisoma hapo juu kwa mapana....

Mkuu ndio maana nilisema kwenye post yangu ya awali kabisa kuna sentensi zinajicontradict zenyewe. On one hand inasena: "This move, according to the ABG's Public Relations Manager Teweli Teweli, was a result of a proposal submitted to the company by Kigoma North MP."

On the other hand inasema: "Kigoma North government submitted a proposal and Barrick funded it because Kigoma North's education system is lagging behind national standards. Kabwe had complained about the same issue in Parliament for years, with no effect." Reads part of the research seen by The Guardian on Sunday.

So which is which? The only person to give the correct answer is Hon Zitto. Hata hivyo kama alivyosema Mwanakijiji huwa kuna manispaa ya Kigoma North? Kigoma Mjini, Kigoma Vijijini, Kibondo na Kasulu ndio manispaa za kigoma. Hii "Kigoma North government" ndio ipi?
 
Mkuu MMM nadhani ni vyema kweli kujua hii Kigoma North Government ni nini. Kigoma kaskazini ni jimbo tu la uchaguzi na liko chini ya wilaya ya kigoma chini ya mkuu wa wilaya ya kigoma (Kigoma mjini na vijijini zipo chini ya mkuu mmoja wa wilaya). Kwa mantiki hiyo Kigoma kaskazini haina halmashauri. Ukienda mbali utakuta kwamba hakuna kitu kinaitwa serikali ya kigoma kaskazini. Hapo kigoma kaskazini kutakuwa na Ofisi ya Mbunge ambayo huenda ndio imetumika kama serikali. Bado Zitto anaingia hapa.

Hakuna cha Kigoma North Government, huo ni mkakati wa kumnyamazisha Mbunge wa Kigoma Kaskazini ili waendelee kuvuna mabilioni ya Dollar na kutuachia sisi peremende za thamani ya Dollar Elfu kumi au laki moja huku wakibeba mabilioni ya Dollar kupeleka Canada na USA. Ni bora kutokuwa na migodi hata mmoja katika nchi kama Tanzania.

Frankly speaking, we are better without them. We will never avoid resource curse engulfing every resource-rich developing country like Tanzania. We need a solid checks and balance mechanism on how we run our affairs as a nation. Everyone is doomed to spoilt for his/her personal interest.
 
Mkuu ndio maana nilisema kwenye post yangu ya awali kabisa kuna sentensi zinajicontradict zenyewe. On one hand inasena: "This move, according to the ABG's Public Relations Manager Teweli Teweli, was a result of a proposal submitted to the company by Kigoma North MP."

On the other hand inasema: "Kigoma North government submitted a proposal and Barrick funded it because Kigoma North's education system is lagging behind national standards. Kabwe had complained about the same issue in Parliament for years, with no effect." Reads part of the research seen by The Guardian on Sunday.

So which is which? The only person to give the correct answer is Hon Zitto. Hata hivyo kama alivyosema Mwanakijiji huwa kuna manispaa ya Kigoma North? Kigoma Mjini, Kigoma Vijijini, Kibondo na Kasulu ndio manispaa za kigoma. Hii "Kigoma North government" ndio ipi?

Hapa inabidi Mheshimiwa Zitto na Teweli Teweli watupatie ufafanuzi, maana kuna contradiction.... tukienda kwa ku guess nafikiri tunaweza kuchukua the wrong direction
 
Back
Top Bottom