Mh. Zitto kuna ukweli gani katika ripoti hii?

Mh. Zitto kuna ukweli gani katika ripoti hii?

Kabwe kabwela, hana utetezi kwa hili.
Huyu nae mweupe machoni lakini si msafi kabisa...ukimfutilia vyema kwa zama hizi amekuwa akimsifia sana JK na Chama chake kistahili..kwa wale waliopata kumwona siku ya Uzinduzi wa Barabara Kigoma - Manyovu na Kavila Mimba..wanaweza kujua huyu Kijana yupoje kwa undani..ni mNafiki mkubwa!

Campanero, mimi sishangai kwa huyo Juma Mwapachu kuingia kwenye hizo bodi za Barrick na Exim kwani kwa wale wanaomjua hizo ndio zake "social climber' yaani wale marehemu Chachage[RIP] aliwaita Makuwadi wa capitalism!! Nakumbuka hilo jina la Dambisa Moyo ni yule binti wa Zambia aliyeandika kitabu cha DEAD AID au mwingine wa hapa bongo?

Ndiyo huyo Dambisa wa Zambia, cheki anavyoifagilia Barrick hapa: One-on-one with Dambisa Moyo, Barrick Gold's newest Board member

kaka yuor love for zitto is blinding you,..you seem to defend him even where he(zitto)has admitted failure..we all admire his courage lakini tunapohisi anakosea lazima tumweleze ukweli only to make him a better leader,..pamoja na upungufu wake uzalendo wa zitto ni wajuu ukilinganisha wanaccm wote except nyerere..
whatever it is msaada kutoka barrick to our law makers una aina flani ya conflict of interest
Wanajamvi, mimi najaribu kujiuliza maswali, criteria zilizotumiwa naBarrick kupeleka msaada Kigoma. Je ni kwa vile maeneo wanakochimba madini wamepata msaada wa kutosha na sasa hawahitaji tena? Je ni kwa vile waliko barrik wananchi wanazoshule, barabara nzuri hudma za afya na mengine? Sidhani kama ni suala la CSR (corporate social responsibility) kama anavyotaka tuamini mheshimiwa zitto. Kimsingi inawezekana walimhonga bila yeye kujua kama hiyo ni hongo

Honestly. Nimesoma hiyo habari yote hapo juu sikuona pabovu. Nilidhani Zitto alipata faida binafsi kuoka Barrick kumbe ni msaada, tena wa mabati ya shule ya sekondari. Hivi Watanzania wanajua hawa jamaa wanatuibia kiasi gani? Sembuse huo msaada kidogo? Na msaada unapelekwa kwenye halmashauri ya Wilaya, si kwa ofisi ya mbunge.

Zitto kaza buti mwanangu....Maana mti wenye matunda ndio utupiwao mawe!
Ability may get you to the top, but it takes character to keep you there.

Na wewe una matatizo kumtwe. Hivi unamlaumu hizo fedha alitumia yeye na familia yake au walipewa watanzania kama ambavyo akina Mengi na Bahrasa waanapeleka misaaada kwa watu mbalimbali ndani na nje ya nchi? Poleni sana.

Gats tatizo sio kutumia au kutokumia. Hapa tatizo ni transparency na ku - compromise kila anachofanya. Tuache mapenzi ya vyama au watu waliopo kwenye vyama kosa ni kosa liwe limefanywa na CCM au CDM. basil Mramba wakati alipokuwa waziri wa fedha alipeleka miradi mingi sana kwake huko Rombo na kusahau watanzania waliopo mahala kwingine. Je, tumwite hero kwa kuwa kafanya hivyo? No ways, he was wrong and he will remain to be wrong. Huo ni mfano mmoja tu. Suala la uwajibikaji ni pamoja kuwa makini katika kila jambo mtu makini afanyalo. Zitto was and is still wrong on what he did because that has no difference with most CCM cadres do, PERIOD

mbona hajafunga huo mdomo na bado anawaongelea? na unavyoonekana ungekua na huo ushahidi usingeweza kuvumilia mpaka dakika hii ungeshatafuta umaarufu siku nyiiingi... vipi walimpiga picha wakimkabidhi hizo kilo 5 au walimsainisha, ushahidi gani unauongelea? unaonekana una wivu tu wewe, tena wivu ambao haujaenda vidato

Mbona tunajua sana suala hilo. wanapiga kelele bungeni baada ya vikao wanapiga simu kuomba msamaha na kusema hiyo ilikuwa danganya toto. kwa mtazamo wako watanzania tutabaki masikini daima

Wanajamvi, mimi najaribu kujiuliza maswali, criteria zilizotumiwa naBarrick kupeleka msaada Kigoma. Je ni kwa vile maeneo wanakochimba madini wamepata msaada wa kutosha na sasa hawahitaji tena? Je ni kwa vile waliko barrik wananchi wanazoshule, barabara nzuri hudma za afya na mengine? Sidhani kama ni suala la CSR (corporate social responsibility) kama anavyotaka tuamini mheshimiwa zitto. Kimsingi inawezekana walimhonga bila yeye kujua kama hiyo ni hongo

Mkuu hiyo ni hongo 100%. kama barrick wangepeleka msaada huo Mtwara wakati Zitto anawakomalia ingekuwa kitu kingine kabisa. Now, why Kigoma kwa mtu anaowashupalia? He is just another thief like those who are in CCM

Mimi simu amini Zitto hata siku moja kwasababu nimnafki kupitiliza .
1. Alipokuja i
Iringa kwenye maandamano alisema ana muheshimu sana Mboye kwani yeye ndiye aliye mjenga kisiasa na kama kuna matatizo wanayamaliza ndani ya vikao lakini ni yuleyule aliye wapinga wabunge wenzie na kukimbilia TBC.
2.Alikuwa mkari sana kwenye Issue ya CEO wa Mwananchi lakini kumbe ilkuwa kwa kwaajiri ya ilo gazeti kumuungezea reputations na baada ya siku nne gazeti liliandika kuwa Zitto pekee ndie aliye kataa posho.!!
3. Amekataa posho wakati bunge lilopita alizikwapua zote. Km kweli si mnafki arudishe na Vxi km Mboye.
4. Anapenda sina pia ni corrupt person.

Mbona tunajua sana suala hilo. wanapiga kelele bungeni baada ya vikao wanapiga simu kuomba msamaha na kusema hiyo ilikuwa danganya toto. kwa mtazamo wako watanzania tutabaki masikini daima

Jamani tusipende kupotosha watu kwa ushabiki, mimi nafikiri kwa mtazamo wako waTZ ndio tutabaki maskini daima. Wewe kama mtu anapigania haki za wananchi kwa uchungu wote halafu unadiriki kusema akitoka anapiga simu kuomba msamaha, ili anufaike na nini? Na wewe unakua wapi anapozipiga hizo simu mpaka ukayajua haya!? Mnataka wabunge wote wawe kama wa CCM kazi kusema tu ndioooooo bungeni na kulala? Msiogope challenges

Mbona tunajua sana suala hilo. wanapiga kelele bungeni baada ya vikao wanapiga simu kuomba msamaha na kusema hiyo ilikuwa danganya toto. kwa mtazamo wako watanzania tutabaki masikini daima

Jamani tusipende kupotosha watu kwa ushabiki, hizi ndio zile siasa za maji taka. Mimi nafikiri kwa mtazamo wako waTZ ndio tutabaki maskini daima. Wewe kama mtu anapigania haki za wananchi kwa uchungu wote halafu unadiriki kusema akitoka anapiga simu kuomba msamaha, ili anufaike na nini? Na wewe unakua wapi anapozipiga hizo simu mpaka ukayajua haya!? Mnataka wabunge wote wawe kama wa CCM kazi kusema tu ndioooooo bungeni na kulala? Msiogope challenges

Mimi simu amini Zitto hata siku moja kwasababu nimnafki kupitiliza .

1. Alipokuja i

Iringa kwenye maandamano alisema ana muheshimu sana Mboye kwani yeye ndiye aliye mjenga kisiasa na kama kuna matatizo wanayamaliza ndani ya vikao lakini ni yuleyule aliye wapinga wabunge wenzie na kukimbilia TBC.

2.Alikuwa mkari sana kwenye Issue ya CEO wa Mwananchi lakini kumbe ilkuwa kwa kwaajiri ya ilo gazeti kumuungezea reputations na baada ya siku nne gazeti liliandika kuwa Zitto pekee ndie aliye kataa posho.!!

3. Amekataa posho wakati bunge lilopita alizikwapua zote. Km kweli si mnafki arudishe na Vxi km Mboye.

4. Anapenda sina pia ni corrupt person.

Aliyekutuma mwambie akupe point kwanza maana umeandika pumba tupu!

Kwa hili na kwa siasa za sasa kama ni kweli ingejulikana mapema saana,. Mh. jitokeze

Wabunge wanapotaka kuwa tendaji ni kosa kubwa.
• Mbunge akiwa mtendaji lazima kutakuwa na conflict of interest
• Mbunge akinzisha na kumanage NGO hata kama nia yake ni nzuri tayari atajikuta kwenye mamtatizo sababu NG zinahitaji misaada
• Mbunge kupewa Fund ya CDF na serikali n kuimanage ni kosa. Subirini labda CAG afunike funike akiazna kukagua pesa za hiyo mifuko
Nawachowashauri wabunge wakizidi kujisahu watajikuta wao ni version B ya sirikali.

Wabunge wengi washafikia huko. Kelele zao bungeni zimewasaidia kujilimbikizia mali. Na kwa mtaji huu tanzania haiwezi kufika popote. Wooooote ni wezi tu

Mimi simu amini Zitto hata siku moja kwasababu nimnafki kupitiliza .
1. Alipokuja i
Iringa kwenye maandamano alisema ana muheshimu sana Mboye kwani yeye ndiye aliye mjenga kisiasa na kama kuna matatizo wanayamaliza ndani ya vikao lakini ni yuleyule aliye wapinga wabunge wenzie na kukimbilia TBC.
2.Alikuwa mkari sana kwenye Issue ya CEO wa Mwananchi lakini kumbe ilkuwa kwa kwaajiri ya ilo gazeti kumuungezea reputations na baada ya siku nne gazeti liliandika kuwa Zitto pekee ndie aliye kataa posho.!!
3. Amekataa posho wakati bunge lilopita alizikwapua zote. Km kweli si mnafki arudishe na Vxi km Mboye.
4. Anapenda sina pia ni corrupt person.

Zitto is corrupt like most of CCM wabungez

Jamani tusipende kupotosha watu kwa ushabiki, mimi nafikiri kwa mtazamo wako waTZ ndio tutabaki maskini daima. Wewe kama mtu anapigania haki za wananchi kwa uchungu wote halafu unadiriki kusema akitoka anapiga simu kuomba msamaha, ili anufaike na nini? Na wewe unakua wapi anapozipiga hizo simu mpaka ukayajua haya!? Mnataka wabunge wote wawe kama wa CCM kazi kusema tu ndioooooo bungeni na kulala? Msiogope challenges

Mkuu ukweli ndo huo, ukubali au ukate

Ability may get you to the top, but it takes character to keep you there.

Sioni suala hapa zaidi ya chuki kwa Zitto. Mwenyewe kaja kaeleza nini kilitokea, Sasa haya mengine ni chuki tu bila sababu ya msingi.TICTS walipeleka mradi wa maji Karatu, Iliandikwa kwenye magazeti na hakuna aliyesema! hivi kosa la Zitto kuwaombea watoto shule kijijini na la mbowe kuuza magari chakavu ya 400m tshs kwa chama, lipi la kupigiwa kelele?Kama kuna mtu ana ushahidi wa Zitto ku benefit personally Au kama kuna ushahidi wa Zitto kuwatetea barrick kwa namna yeyote autoe hapa.

Mkuu,
Ukitaka kuuuona uharamu wa hili tendo inabidi usome au upitie nyaraka zifuatazo;
i)Local Government Finances Act, 1982
ii) Public Leadership Code of Ethics Act, 1995
iii) Proceeds of Crime Act, 1992.....Bila kusahau,
iv) Constitution of The United Republic of Tanzania.
La sivyo, utakuwa unabwabwaja tu kama walivyofanya waliotangulia........mwaga nodozz au data,la sivyo kila neno litakuwa ni opinion,siyo fact.

Ni hivi wanaJF,

Wawekezaji kama Barrick, Vodacom, Resolutte, Symbion or anyone else are not our lost cousins, na hivyo hawakuja Tanzania kutafuta ndugu zao waliopetea. Wako hapa kwa sababu moja tu - to make 'money'. Hili ni muhimu kukumbuka siku zote. Sasa kama wako hapo kusaka pesa/faida watafanya kila wawezalo wafanikiwe. Na katika msako huo wa pesa wamechora ramani inayoonesha njia za kupita na vikwazo vyote vinayoweza kuhatarisha msako wao. Na hapa wamepata mambo matatu.

Mosi, Policy makers - kwa maana ya wanasiasa. Wawekezaji wamejitahidi sana kuwa karibu na wanasiasa wetu ili kujua 'thinking' yao kwenye policies na kama kuna athari zozote kwao (kumbuka mnuso wa ubalozi wa Canada kwa wabunge wetu July 2011). Lakini wawekezaji hawa wamekuwa karibu zaidi na wanasiasa wenye ushawishi mkubwa ndani na nje ya ulingo. Hapa ndio linakuja swala la CSR Social Corporate Responsibilty - CSR pia inatumika zaidi nitaeleza hapo chini). Kama mwanasiasa ukishapata madawati, au cement, au mabati au vyote kwa pamoja, ni vigumu sana kubaki na 'uhuru' na moral authority' ya kuhoji mapungufu ya mwekezeji aliyekusaidia. Whether you are a 'full grown' politician or a 'rookie' it is practically impossible to continue questioning the very same people who are supporting you politcally. impossible. Kwa hiyo hata kama watachezea vitabu vyao vya mahesabu wanajuwa wa kunyanyua fimbo atakuwa tayari kwa 'dialogue' = profit secured.

Pili, Noise makers - media, NGOs, vyama etc. Kama policy makers watafunga ndoa haramu na wawekezaji basi watu muhimu wa kuibua mambo ni hawa noise makers. Angalia hapa Tanzania kwa sasa. Huu mtindo wa u-matonya sio tu uko kwenye serikali kuu bali pia umeanza kuota mizizi kwenye organisation kama Media councils. Hivi mwandishi wa habari atamchambuaje mfadhili aliyempeleka kwenye 'training' Washington au Toronto au London? how? na utaandika kwenye gazeti la nani? Ukiachilia mbali TAMWA na NGOs nyingine kama mbili hivi, hizi NGOs zingine sina hakika wanafanya nini? Kwa hiyo kama wawekezaji watacheza na vitabu, policy makers wakashindwa kugundua/wakazembea na hawa noise makers wakaa kimyaa = profit secured. Sasa twende kwenye mother of all the tricks hapo chini.

Tatu, mdundiko - sega. Ni hivi. Ni kawaida kabisa unapopanga nyumba ukakuta ina kasoro za msingi, na ukakubaliana na mwenye nyumba kuwa utalipia gharama za matengenezo lakini mtajuana wakati wa kodi. Hivyo wakati wa kulipa kodi ukiwadia, utachukua kilicho chako na mwenye nyumba atachukia balance (after gharama za matengenezo) na hapa unaweza uka-inflate (ukazidisha) gharama halisi, lakini maadam mwenye nyumba alishasema sawa anatakiwa akubaliane na matokeo (good or bad). Cha muhimu hapa kutambua ni kuwa mpangaji anatafuta sehemu ya kuishi/kuendeshea shughuli zake na si kazi yake kurebisha ufa, kupaka rangi, au kuezeka nyumba.

Barrick, Vodacom, Symbion, Songas au mwekezeji mwingine yoyote hawakuja Tanzania kujenga shule, kutengeneza barabara, kuchimba visima, au kutununulia madawati. Wako hapa kutumia rasilimali zilizo ndani ya mipaka ya nchi kwa makubaliano kuwa watalipa KODI. Serikali (kama mpangisha nyumba) ana jukumu la kujenga shule, kununua madawati, kutengeza barabara n.k. Na anatakiwa achukue kodi kufanya kazi hizo. Hivi Barrick wana ujuzi gani wa kuchimba visima? Au Vodacom ni wataalam wa mawasiliano au wa madawati? Kuna mkorogo wa fikra hapa. Serikali inasahau au inaacha kwa makusudi kufanya kazi zake na badala yake wanategemea wachimba madini au watoa huduma za mawasiliano wafanye kazi za serikali! Hiki ndio kiini cha matatizo tuliyonayo, kwamba wananchi wanadai huduma muhimu toka kwa wawekezaji na sio serikali. Na wawekezaji wamegundua ili wawe na maisha mazuri na marefu basi no bora wakafanya kazi za serikali kwenye maeoneo ya uwekezaji.

Matokeo yake ni nini? Unapofika wakati wa kulipa kodi, mpangaji (mwekezaji) anakata gharama zake (inflated) na serikali inabakia na whatever. Angalieni orodha ya walipa kodi wakubwa iliyosomwa mwaka huu bungeni. Hivi kuna mwekezaji yoyote amenunua madawati kama Vodacom? Na ni kampuni gani inaongoza Tanzania kwa kuwa na wateja wengi? Inakuwaje wauza CHIBUKU wanalipa kodi kubwa kuliko VODACOM? Mimi nadhani watu kama vodacom, Barrick etc wamegundua kutoa misaada ni (a) cheaper kuliko kodi kamili; (b) inampa sifa nzuri mbele ya jamii maana kila leo ataonekana kwenye luninga na magazeti (noise maker) akisaidia jamii; na (c) inapunguza kelele toka kwa wananchi na serikali yenyewe - 2 for the price of 1.

Maoni yangu:
CSR sio kodi - period. Toa madawati au usitoe kodi ibakie pale pale.
Wabunge watambue kuwa kazi yao ya kwanza (main job) ni kusimamia serikali katika utendaji wake wa kazi wa kuwahudumia wananchi. Sio kazi ya mbunge kujenga shule, ila mbunge anaweza kushirikiana na wanajamii kujenga hiyo shule. Kama wabunge wangefanya kazi inayotakiwa ya kusimamia serikali tusingekuwa na Meremeta, Deep Green, Dowans, Ndege za Qartar wa vitu vya namna hiyo. Hivyo $10,000 ya kununulia mabati is peanut kwa kuangalia hela zinazofuja huku bunge likisema ndiyooo. Tanzania pamoja na hiki wanachosema ni 'umasikini' hatushindwi kununua mabati, au kununua madawati. hatushindwi hata kidogo. Ila tunaomba kwa sababu hela zimeenda siko. Na unless wabunge wetu watambue hilo watakufa barabarani wakiomba pesa toka ubalozi huu, au kampuni ile etc ili mradi ni maisha ya kibakuli. Na inabidi wafanye hivyo kwa sababu kama mbunge hakuleta 'maendeleo' anakosa kura. Kumbe ni kusema kama wabunge wangekuwa 'serious' wasingekubwa na hii fedheha ya kuwa omba omba.

Asubuhi upate uji toka kwa Mandawa halafu kesho yake asubuhi useme mandawa ni mtu mbaya? haiwezekani.

NB: Zitto wala simlaumi na wala hana haja ya kujieleza zaidi ya kuweka mambo wazo - it is the system stupid!

Back
Top Bottom