Ni hivi wanaJF,
Wawekezaji kama Barrick, Vodacom, Resolutte, Symbion or anyone else are not our lost cousins, na hivyo hawakuja Tanzania kutafuta ndugu zao waliopetea. Wako hapa kwa sababu moja tu - to make 'money'. Hili ni muhimu kukumbuka siku zote. Sasa kama wako hapo kusaka pesa/faida watafanya kila wawezalo wafanikiwe. Na katika msako huo wa pesa wamechora ramani inayoonesha njia za kupita na vikwazo vyote vinayoweza kuhatarisha msako wao. Na hapa wamepata mambo matatu.
Mosi, Policy makers - kwa maana ya wanasiasa. Wawekezaji wamejitahidi sana kuwa karibu na wanasiasa wetu ili kujua 'thinking' yao kwenye policies na kama kuna athari zozote kwao (kumbuka mnuso wa ubalozi wa Canada kwa wabunge wetu July 2011). Lakini wawekezaji hawa wamekuwa karibu zaidi na wanasiasa wenye ushawishi mkubwa ndani na nje ya ulingo. Hapa ndio linakuja swala la CSR Social Corporate Responsibilty - CSR pia inatumika zaidi nitaeleza hapo chini). Kama mwanasiasa ukishapata madawati, au cement, au mabati au vyote kwa pamoja, ni vigumu sana kubaki na 'uhuru' na moral authority' ya kuhoji mapungufu ya mwekezeji aliyekusaidia. Whether you are a 'full grown' politician or a 'rookie' it is practically impossible to continue questioning the very same people who are supporting you politcally. impossible. Kwa hiyo hata kama watachezea vitabu vyao vya mahesabu wanajuwa wa kunyanyua fimbo atakuwa tayari kwa 'dialogue' = profit secured.
Pili, Noise makers - media, NGOs, vyama etc. Kama policy makers watafunga ndoa haramu na wawekezaji basi watu muhimu wa kuibua mambo ni hawa noise makers. Angalia hapa Tanzania kwa sasa. Huu mtindo wa u-matonya sio tu uko kwenye serikali kuu bali pia umeanza kuota mizizi kwenye organisation kama Media councils. Hivi mwandishi wa habari atamchambuaje mfadhili aliyempeleka kwenye 'training' Washington au Toronto au London? how? na utaandika kwenye gazeti la nani? Ukiachilia mbali TAMWA na NGOs nyingine kama mbili hivi, hizi NGOs zingine sina hakika wanafanya nini? Kwa hiyo kama wawekezaji watacheza na vitabu, policy makers wakashindwa kugundua/wakazembea na hawa noise makers wakaa kimyaa = profit secured. Sasa twende kwenye mother of all the tricks hapo chini.
Tatu, mdundiko - sega. Ni hivi. Ni kawaida kabisa unapopanga nyumba ukakuta ina kasoro za msingi, na ukakubaliana na mwenye nyumba kuwa utalipia gharama za matengenezo lakini mtajuana wakati wa kodi. Hivyo wakati wa kulipa kodi ukiwadia, utachukua kilicho chako na mwenye nyumba atachukia balance (after gharama za matengenezo) na hapa unaweza uka-inflate (ukazidisha) gharama halisi, lakini maadam mwenye nyumba alishasema sawa anatakiwa akubaliane na matokeo (good or bad). Cha muhimu hapa kutambua ni kuwa mpangaji anatafuta sehemu ya kuishi/kuendeshea shughuli zake na si kazi yake kurebisha ufa, kupaka rangi, au kuezeka nyumba.
Barrick, Vodacom, Symbion, Songas au mwekezeji mwingine yoyote hawakuja Tanzania kujenga shule, kutengeneza barabara, kuchimba visima, au kutununulia madawati. Wako hapa kutumia rasilimali zilizo ndani ya mipaka ya nchi kwa makubaliano kuwa watalipa KODI. Serikali (kama mpangisha nyumba) ana jukumu la kujenga shule, kununua madawati, kutengeza barabara n.k. Na anatakiwa achukue kodi kufanya kazi hizo. Hivi Barrick wana ujuzi gani wa kuchimba visima? Au Vodacom ni wataalam wa mawasiliano au wa madawati? Kuna mkorogo wa fikra hapa. Serikali inasahau au inaacha kwa makusudi kufanya kazi zake na badala yake wanategemea wachimba madini au watoa huduma za mawasiliano wafanye kazi za serikali! Hiki ndio kiini cha matatizo tuliyonayo, kwamba wananchi wanadai huduma muhimu toka kwa wawekezaji na sio serikali. Na wawekezaji wamegundua ili wawe na maisha mazuri na marefu basi no bora wakafanya kazi za serikali kwenye maeoneo ya uwekezaji.
Matokeo yake ni nini? Unapofika wakati wa kulipa kodi, mpangaji (mwekezaji) anakata gharama zake (inflated) na serikali inabakia na whatever. Angalieni orodha ya walipa kodi wakubwa iliyosomwa mwaka huu bungeni. Hivi kuna mwekezaji yoyote amenunua madawati kama Vodacom? Na ni kampuni gani inaongoza Tanzania kwa kuwa na wateja wengi? Inakuwaje wauza CHIBUKU wanalipa kodi kubwa kuliko VODACOM? Mimi nadhani watu kama vodacom, Barrick etc wamegundua kutoa misaada ni (a) cheaper kuliko kodi kamili; (b) inampa sifa nzuri mbele ya jamii maana kila leo ataonekana kwenye luninga na magazeti (noise maker) akisaidia jamii; na (c) inapunguza kelele toka kwa wananchi na serikali yenyewe - 2 for the price of 1.
Maoni yangu:
CSR sio kodi - period. Toa madawati au usitoe kodi ibakie pale pale.
Wabunge watambue kuwa kazi yao ya kwanza (main job) ni kusimamia serikali katika utendaji wake wa kazi wa kuwahudumia wananchi. Sio kazi ya mbunge kujenga shule, ila mbunge anaweza kushirikiana na wanajamii kujenga hiyo shule. Kama wabunge wangefanya kazi inayotakiwa ya kusimamia serikali tusingekuwa na Meremeta, Deep Green, Dowans, Ndege za Qartar wa vitu vya namna hiyo. Hivyo $10,000 ya kununulia mabati is peanut kwa kuangalia hela zinazofuja huku bunge likisema ndiyooo. Tanzania pamoja na hiki wanachosema ni 'umasikini' hatushindwi kununua mabati, au kununua madawati. hatushindwi hata kidogo. Ila tunaomba kwa sababu hela zimeenda siko. Na unless wabunge wetu watambue hilo watakufa barabarani wakiomba pesa toka ubalozi huu, au kampuni ile etc ili mradi ni maisha ya kibakuli. Na inabidi wafanye hivyo kwa sababu kama mbunge hakuleta 'maendeleo' anakosa kura. Kumbe ni kusema kama wabunge wangekuwa 'serious' wasingekubwa na hii fedheha ya kuwa omba omba.
Asubuhi upate uji toka kwa Mandawa halafu kesho yake asubuhi useme mandawa ni mtu mbaya? haiwezekani.
NB: Zitto wala simlaumi na wala hana haja ya kujieleza zaidi ya kuweka mambo wazo - it is the system stupid!