Mhadhiri NIT akiri kumuomba rushwa ya ngono Mwanafunzi wake

Mhadhiri NIT akiri kumuomba rushwa ya ngono Mwanafunzi wake

Unaweza kuta huyo binti kamnyima dingi mzigo....alafu huko kitaa badoboda anakula kiulaini tigo ya binti....
hatar sana....
 
Kama alikua ana upendo wa mke..mke shurti asamehe...!km mume alikua mbinafsi hehehehee (in mama ima voice)..shit happens!inategemea na mume alikuajalikuaje kwa mkewe!...mke akisimama imara itamsaidia asijidhuru bure baba wa watu
Kwa ujinga huo....atabeba mzigo wake mwenyewe....
Ndio hapewi kabisa.. ..au ashawaka huyo mzee..
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imemhukumu mhadhiri wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Samson Mahimbo (69), kulipa faini ya Sh. Milioni tano au kwenda jela miaka mitatu baada ya kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) ikiwamo kuomba msamaha na kukiri kutenda kosa la kuomba ya ngono.

Kadhalika mshtakiwa huyo ameshailipa serikali fidia ya Sh.milioni mbili baada ya makubaliano na DPP.

Hukumu hiyo ilisomwa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya mshtakiwa kuandika barua ya kukiri kosa kwa DPP dhidi ya kesi ya Uhujumu Uchumi namba 80/2019.


=====
Mhadhiri wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Samson Mahimbo (69), amehukumiwa kulipa faini ya Sh. Milioni tano au kwenda jela miaka mitatu baada kukiri mashtaka yaliyokuwa yakimkabili likiwemo la kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi wake.

Hukumu hiyo imesomwa leo Novemba 26,2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya mshtakiwa kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) ikiwamo kuomba msamaha na kukiri makosa yake.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema tabia ya rushwa ya ngono imekithili na ni gumzo katika vyuo hapa Nchini na kwamba inapaswa kukemewa.

Amesema, kitendo cha wanafunzi kuonyeshwa majibu kunapelekea kupata wataalamu wasiokuwa na viwango vinavyostahili hivyo njia sahihi ya watu kama mshtakiwa ni kukomesha vitendo Kama hivyo kwa kuwafikisha mahakamani na kuwapatia adhabu chungu.

"Utalipa faini ya Sh.milioni tano au kwenda jela miaka mitatu" amesema Hakimu Shaidi.

Hakimu Shaidi ameongeza kuwa, kitendo alichofanya ni mshtakiwa huyo ni cha aibu kwa umri wake kwani mtu wa taaluma yake alipaswa kuwa mfano wa kuigwa lakini akaamua kujiingiza katika mapenzi na watoto wadogo ambao si hadhi yake.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo ameshailipa serikali fidia ya Sh.milioni mbili baada ya makubaliano hayo.

Mapema, Wakili wa Serikali Mkuu, Zakaria Ndasco amedai kuwa Jamhuri haina kumbukumbu ya makosa ya zamani ya mshtakiwa na kwamba tayari ameshalipa fidia ya Sh.milioni mbili.

Akitoa utetezi wake, kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo, Wakili wa utetezi, Claudia Msando amedai mshtakiwa ana umri mkubwa na kwamba ameshaanza kupata maradhi yaa uzee ikiwamo kutokusikia na kuona vizuri na pia ni mstaafu na ana familia inayomtegemea.

Katika kesi ya msingi inadaiwa mshtakiwa ambaye alikuwa akifundisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza 2015/16 aliomba rushwa hiyo kutoka kwa mwanafunzi Victoria Faustine.

Mwendesha Mashtaka wa taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukutu), Vera Ndeoya alidai kuwa Januari 12, mwaka 2017 katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Camp David, iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam mshtakiwa aliomba rushwa ya ngono.

Ilidaiwa kuwa mshitakiwa huyo akiwa mwajiriwa wa NIT katika kozi ya Usimamizi wa Barabara na Usafirishaji namba LTU 07101 kwa kutumia mamlaka yake alimlazimisha mwanafunzi huyo kutoa rushwa ya ngono.

Ilidaiwa kuwa, aliomba rushwa hiyo ili aweze kumfaulisha katika mtihani wake wa marudio katika kozi ya Usimamizi wa Barabara na Usafirishaji anayosomea ya Januari 5, mwaka 2017.

Chanzo: Michuzi Blog

Pia soma


Ngono mbaya sana
 
Biashara
Kumbe mahakama sasa wamebadili hukumu hiyo kukubaliana na mwendesha mashtaka nilijua ni mafisadi tu kumbe mpaka kwenye ngono.kwa hiyo nikimtia mimba mtoto wa shule nikakubaliana na mwendesha mashtaka nikakubali kosa nikalipa fine naachiwa?
 
Shemu usitete ujinga huu, mkufunzi kula dent wake ni aibu na ni kuvuruga mfumo wa elimu, pia tunapata wahitimu wasiokuwa na sifa
Kuna mtu alimchoma!mi hata sishangai!aliyemsafi na aanze kumrarua huyu baba!shit happens!
Pole dingilai kwa kichafuka!maisha lazima yasonge!
 
Huyo binti bora angempa tu, ona sasa serikali inatia kibindoni milioni 5 huku binti haambulii kitu!
Yaani angekubali kuuza utu wake kwa hicho kizee?? Je angemfia kifuani mngemuelewa binti??? Mnaongea kama vile hamna watoto wa kike au hamna madada.
 
Ngono ni ulevi kama ulevi mwingine, mlevi akiona pombe koo hukereketa, vivyo hivyo wanaume tuonapo sina flani ya wanawake wanaogusa mioyo hali hubadilika
Mpaka uombe rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi,una ukame kiasi gani wakati una mke ndani?
 
Kosa lake tukumbuke ni rushwa ya ngono, na sio swala la tofauti ya umri kati yao
 
Back
Top Bottom