Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,197
- 128,160
Kuharibu vipi mkuu?mzee kakosa ila natafakari mpaka kafika umri huo kashaharibu wanafunzi wangapi haya mazee aibu sana..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuharibu vipi mkuu?mzee kakosa ila natafakari mpaka kafika umri huo kashaharibu wanafunzi wangapi haya mazee aibu sana..
tema mate chini ngono haina uzee wala ujanamzee kakosa ila natafakari mpaka kafika umri huo kashaharibu wanafunzi wangapi haya mazee aibu sana..
Mtoto wa shule wa umri gani?Kumbe mahakama sasa wamebadili hukumu hiyo kukubaliana na mwendesha mashtaka nilijua ni mafisadi tu kumbe mpaka kwenye ngono.kwa hiyo nikimtia mimba mtoto wa shule nikakubaliana na mwendesha mashtaka nikakubali kosa nikalipa fine naachiwa?
Vic unauliza swali gani hilo bhana?Hili liwe fundisho,miaka 69 du kwani hana mke?
Kwani zitakua zinafanana?Hili liwe fundisho,miaka 69 du kwani hana mke?
Huyo binti bora angempa tu, ona sasa serikali inatia kibindoni milioni 5 huku binti haambulii kitu!
Tuyakate..!Hebu fikiria mke wake na watoto wake kwa aibu hii. Haya madushe yetu ni ya kulaani kweli
Binti atakaziwa probably gpa yake 2Huyo binti bora angempa tu, ona sasa serikali inatia kibindoni milioni 5 huku binti haambulii kitu!
uyo lecture ni mpuuzi kabisa shame on himMahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imemhukumu mhadhiri wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Samson Mahimbo (69), kulipa faini ya Sh. Milioni tano au kwenda jela miaka mitatu baada ya kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) ikiwamo kuomba msamaha na kukiri kutenda kosa la kuomba ya ngono.
Kadhalika mshtakiwa huyo ameshailipa serikali fidia ya Sh.milioni mbili baada ya makubaliano na DPP.
Hukumu hiyo ilisomwa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya mshtakiwa kuandika barua ya kukiri kosa kwa DPP dhidi ya kesi ya Uhujumu Uchumi namba 80/2019.
=====
Mhadhiri wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Samson Mahimbo (69), amehukumiwa kulipa faini ya Sh. Milioni tano au kwenda jela miaka mitatu baada kukiri mashtaka yaliyokuwa yakimkabili likiwemo la kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa mwanafunzi wake.
Hukumu hiyo imesomwa leo Novemba 26,2019 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya mshtakiwa kuingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) ikiwamo kuomba msamaha na kukiri makosa yake.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema tabia ya rushwa ya ngono imekithili na ni gumzo katika vyuo hapa Nchini na kwamba inapaswa kukemewa.
Amesema, kitendo cha wanafunzi kuonyeshwa majibu kunapelekea kupata wataalamu wasiokuwa na viwango vinavyostahili hivyo njia sahihi ya watu kama mshtakiwa ni kukomesha vitendo Kama hivyo kwa kuwafikisha mahakamani na kuwapatia adhabu chungu.
"Utalipa faini ya Sh.milioni tano au kwenda jela miaka mitatu" amesema Hakimu Shaidi.
Hakimu Shaidi ameongeza kuwa, kitendo alichofanya ni mshtakiwa huyo ni cha aibu kwa umri wake kwani mtu wa taaluma yake alipaswa kuwa mfano wa kuigwa lakini akaamua kujiingiza katika mapenzi na watoto wadogo ambao si hadhi yake.
Hata hivyo, mshtakiwa huyo ameshailipa serikali fidia ya Sh.milioni mbili baada ya makubaliano hayo.
Mapema, Wakili wa Serikali Mkuu, Zakaria Ndasco amedai kuwa Jamhuri haina kumbukumbu ya makosa ya zamani ya mshtakiwa na kwamba tayari ameshalipa fidia ya Sh.milioni mbili.
Akitoa utetezi wake, kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo, Wakili wa utetezi, Claudia Msando amedai mshtakiwa ana umri mkubwa na kwamba ameshaanza kupata maradhi yaa uzee ikiwamo kutokusikia na kuona vizuri na pia ni mstaafu na ana familia inayomtegemea.
Katika kesi ya msingi inadaiwa mshtakiwa ambaye alikuwa akifundisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza 2015/16 aliomba rushwa hiyo kutoka kwa mwanafunzi Victoria Faustine.
Mwendesha Mashtaka wa taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukutu), Vera Ndeoya alidai kuwa Januari 12, mwaka 2017 katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Camp David, iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam mshtakiwa aliomba rushwa ya ngono.
Ilidaiwa kuwa mshitakiwa huyo akiwa mwajiriwa wa NIT katika kozi ya Usimamizi wa Barabara na Usafirishaji namba LTU 07101 kwa kutumia mamlaka yake alimlazimisha mwanafunzi huyo kutoa rushwa ya ngono.
Ilidaiwa kuwa, aliomba rushwa hiyo ili aweze kumfaulisha katika mtihani wake wa marudio katika kozi ya Usimamizi wa Barabara na Usafirishaji anayosomea ya Januari 5, mwaka 2017.
Chanzo: Michuzi Blog
Pia soma
Mtego wa TAKUKURU wamnasa Mhadhiri NIT akiomba rushwa ya ngono
Mhadhiri Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Samson Mahimbo (66yrs) akamatwa na TAKUKURU Wilaya ya Kinondoni baada ya kunaswa katika mtego wa rushwa ya ngono kwa mwanafunzi. Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni, Denis Manumbu ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo...www.jamiiforums.com
Mhadhiri NIT afikishwa Mahakama ya Kisutu kwa tuhuma ya kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi ili amfaulishe
Mhadhiri wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Samsoni Mahimbo (68), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake ili amfaulishe ktk mitihani wa marudio (Supplement), Kesi imeahirishwa hadi September 17. Mshtakiwa...www.jamiiforums.com
![]()
TAKUKURU: Tulimkuta Mhadhiri wa NIT guest akiwa mtupu akiomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake
Takukuru leo Jumatano Oktoba 9, 2019 imeieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jinsi ilivyomkuta katika nyumba ya kulala wageni mhadhiri msaidizi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Samson Mahimbo (68) akiwa mtupu. Mahimbo anakabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wa...www.jamiiforums.com
alishaga kufaHili liwe fundisho,miaka 69 du kwani hana mke?
mhuuuumalishaga kufa
mzee kakosa ila natafakari mpaka kafika umri huo kashaharibu wanafunzi wangapi haya mazee aibu sana..
Anataka damu changa bestHili liwe fundisho,miaka 69 du kwani hana mke?
Hahaa na ukute ni 1st yr alofanya upupu huu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kumbe mnafahamiana watu wa huko!Ukimwangalia vizuri usoni utagundua kuwa lazima mzee huyu atakuwa Mngoni wa Songea kama sio Madaba basi atakuwa wa Mfaranyaki, Wangoni bwana~!