Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHANDISI FATMA REMBO - APANIA KUFANYA MAKUBWA NDANI YA UWT MKOA WA IRINGA
Mjumbe wa Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa 2022-2027 Kutokea Mkoa wa Iringa Ndugu Eng. Fatma Rembo amefanya ziara maeneo mbalimbali Mkoa wa Iringa na kushiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Katika ziara ya tarehe 09 Machi, 2023 Wilaya ya Kilolo, Eng. Fatma Rembo amechangia Shilingi 1,000,000 kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba ya Katibu wa UWT Wilaya ya Kilolo na kuahidi kununua Pikipiki Kwa ajili ya shughuli za UWT huku akionya vikali vitendo vya Ukatili na Unyanyasaji wa kijinsia wa Watoto wa kike na watoto wa kiume.
Eng. Fatma Rembo mnamo tarehe 08 Machi, 2023 aliadhimisha Siku ya wanawake Duniani kwa kutembelea Wodi ya Wanawake (wakina mama waliotoka kujifungua) katika hospitali ya Mkoa wa Iringa huku wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego. Maadhimisho kimkoa yaliadhimishwa Wilaya ya Kilolo.
Aidha, Eng. Fatma Rembo tarehe 04 Machi, 023 alishiriki Baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) la Wilaya ya Iringa Vijijini ambapo alichangia Matofali 1000 na Mifuko 100 ya Saruji kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba ya Mtendaji wa UWT wa Wilaya.
Pia, Uongozi wa UWT Wilaya ya Iringa Vijijini walimpatia Eng. Fatma Rembo Hati ya Pongezi pamoja na zawadi nyingine mbalimbali kutokana na mchango wake katika Chama Cha Mapinduzi na jamii inayomzunguka.
Eng. Rembo akizungumza katika baraza hilo, alisisitiza na kuhimiza Umoja na Mshikamano katika utendaji wa kazi za UWT katika wilaya ya Iringa Vijijini.
Vile vile, tarehe 03 Machi, 2023 Eng. Rembo alishiriki Kongamano la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Wilaya ya Iringa Mjini la kupinga vitendo vya Unyanyasaji wa Kijinsia, Ubakaji na Ulawiti kwa watoto, Kongamano lililoanza kwa matembezi kutoka ofisi za CCM Wilaya ya Iringa Mjini na kuhitimishwa katika ofisi za CCM Mkoa wa Iringa ambako kongamano hilo lilifanyika.
Aidha, tarehe 10 Februari, 2023 Eng. Rembo alipata fursa ya kushiriki Baraza Kuu la UWT la Mkoa wa Iringa chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Zainab Mwamwindi. Eng. Rembo alichangia hoja mbalimbali zilizojadiliwa zinazohusu masuala ya Umoja wa Wanawake wa Mkoa wa IRINGA.
Pamoja na wajumbe wengine, alikuwepo ni Mkuu wa Mkoa wa IRINGA, Mhe. Halima Dendego, Katibu wa CCM wa Mkoa wa IRINGA Ndugu Rukia Mkindu, Viongozi na Wajumbe wengine wa Mkoa wa Iringa.
#UWTImara
#WanawakeJeshiKubwa
#KaziIendelee