Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,524
- 13,682
Bila shaka yo yote huyu Mhandisi John Nzulule aliyetenguliwa na Rais si mara yake ya kwanza kutupiga katika ununuzi wa ndege za serikali. Nadhani ametupiga katika ununuzi wa ndege serikali na pia ndege za ATCL ambazo zimekuwa zikinunuwa na serikali kukwepa kukamatwa na wadeni wa ATCL huko majuu.
Kwa uzoefu wake wa kutupiga sasa aliamua kutupiga kwa kipigo cha mbwa koko kwa kuweka cha juu cha mzigo wake wa dola 49 milioni katika ununuzi wa ndege ya mizigo ya ATCL. Fikiria badala ya kulipa dola milioni 37 akataka serikali ilipe dola milioni 86! Hii nadhani amevunja rekodi sijui tuite ya nchi au dunia!
Lakini bado natafakari kuwa ufisadi huu hafanyi peke yake. Lazima kuna mtu au genge la watu anashirikiana nao. Nashauri vyombo vinavyohusika na uchunguzi vimuhoji kwa kina mpaka ataje wenzake wanaohujumu nchi hii. Vinginevyo kundi hili litaendelea na ufisadi wake hadi nchi hii ifilisike kabisa!