06 December 2024
Tanzania yapigwa jeki kwa ajili ya ujenzi wa kipande cha kilometa 411 cha SGR Tabora hadi Kigoma.
Benki ya Maendeleo ya Afrika ADB Yaongoza kutia fedha kapu la Ufadhili wa Dola Bilioni 1.2 kwa Mradi wa Reli ya Tanzania wa Standard Gauge SGR
Benki ya Maendeleo ya Afrika imetia saini barua ya uratibu na Benki ya Deutsche na Société Générale kuanzisha upigaji debe mkakati wa mashirikiano ya kukusanya hadi kuchangisha dola bilioni 1.2 kwa ajili ya mradi wa Reli ya Tanzania ya Standard Gauge (SGR).
Makubaliano hayo, yaliyotiwa saini wakati wa Jukwaa la Uwekezaji la Afrika huko Rabat (the African Investment Forum’s 2024 Market)Morocco, yanasisitiza jukumu la Benki ADB kama Mratibu Mkuu wa Awali Aliyepewa Mamlaka na jukumu nyeti katika kuhamasisha ufadhili wa mradi huo wa kimkakati wa reli ya SGR.
Wizara ya Fedha ya Tanzania inataka kutafuta fedha kutoka katika Masoko ya Mitaji ya Madeni ya Kimataifa (the international debt capital market) ili kufadhili ujenzi wa njia ya reli yenye urefu wa kilomita 411 kati ya Tabora na Kigoma.
Mradi huo wenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 2.3 utaunganisha bandari ya Tanzania ya Dar es Salaam kwenye Bahari ya Hindi na bandari ya Mwanza kwenye Ziwa Victoria. Kutoka huko, itaenea hadi nchi jirani za Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Uganda.
Hii itafungua uwezo wa kiuchumi kwa kuunda maeneo mapya ya uchimbaji madini na bidhaa za kilimo katika Afrika Mashariki na Kati.
Max Ndiaye, Mkurugenzi Mwandamizi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa Syndications, Cofinancing, na Africa Investment Forum, alitia saini barua ya uratibu pamoja na Myriam Ouazzani, Mkurugenzi Mkuu wa Deutsche Bank kwa Afrika, na Randolph Fotso, Mkuu wa Société Générale Mkuu wa DFI Solutions, Development and Structured Export Finance.
Ufadhili huo utapangwa katika awamu mbili, huku Benki ya Maendeleo ya Afrika ADB ikiratibu awamu ya pili kwa michango kutoka taasisi za fedha za maendeleo, Wakala wa Mikopo ya Mauzo ya Nje, wakopeshaji wa pande mbili (bilateral) , na benki za maendeleo za kutoka vyanzo vyingi (multilateral development banks)
Habari zaidi :
20 December 2024
Siku ya Soko la Mnada Rabat Morocco
Siku za Soko za 2024 huko Rabat, Morocco ziliwaleta wawekezaji, wafadhilii wa miradi ya ubia wa pamoja katika vyumba vya bodi vya majadiliano 41 kusikiliza wenye miradi kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika iliyoletwa kujadiliwa na jinsi iliyopigiwa upatu kwa hoja za kuwa ni miradi inayotekelezeka pia kuweza kuleta mageuzi kiuchumi, kibiashara na kijamii.
Wenye mitaji ya miradi walipitia na kuvutiwa kujifunga kuingia ubia katika miradi 37 ya Barani Afrika kuleta mageuzi inayohusisha usafiri, nishati, nishati, biashara ya kilimo, madini, dawa, utalii, miundombinu ya mijini, usimamizi wa maji, na zaidi.
Baada ya siku tatu kali za majadiliano na mazungumzo, Jukwaa lilirekodi dola za marekani bilioni 29.2 za kuweza kuvutia wawekezaji wapya